Simba, kama timu, mwaka huu haiko vizuri. Hili limeonekana kwa muda mrefu na kupigiwa makelele sana. Msemaji akaja na usemi kuwa eti timu inacheza objective football.
Nadhani ingekuwa vizuri kama nguvu zingeelekezwa kwenye kuiimarisha timu kwa kutafuta wachezaji sahihi badala ya kuanza kutafutiana lawama maana hili likifanyika hakuna marekebisho yatakayofanyika na timu itaendelea kucheza papatupapatu utafikiri wanacheza Rugby
Sent from my SM-G781U using
JamiiForums mobile app
Naungana na wewe mkuu..
Simba ni mbovu tangu muuza mbilimbi wa brazil apewe kuifundisha. Simba mechi zote tunashinda kwa bahati na mda wote tumekuwa tukishambuliwa.
Hata mechi ya ngao ya hisani Tanga, ni kuwa Yanga haikuwq na bahati tu, walipata chance Kibao ila hawakufunga.
Kocha ndio mzigo, kocha hajui anataka nini, kocha sub zake mara zote za kijinga. Timu ikipata goli ama ikisawazisha, basi ina relax. Ikipoteza mpira basi, wanakabia kwa macho.
Hizi goli 5 ana zaidi ilikuwa ni swala la muda tu.
Timu haileweki inacheza mfumo gani, timu inacheza kama watoto wa shule wamekusanywa Pahali wanacheza gombania goli. Team haina fitness. Kwahiyo kusema wamehongwa sioni mantiki, maana hata bila kuhongwa Yanga ni nzuri mara 100 ya Simba.
Tunachojiuliza ni kwann uongozi unaendelea kumnangania kocha ambaye hana maajabu. Kocha anayeshindwa kujua Wazee awachzeshe mechi ipi, waanzie sub au waanze. Chapombe, amechoka kabisa lakn kila mechi anaanza. Boko umri haufai tena kuchezea Simba. Mechi na al Ahly, kila mpira aliopewa Boko alipoteza ana alishindwa kukontrol, lakn muuza mbilimbi wa brazil hakuna.
Mohamed Hussein kila mechi anaanzishwa, hatikatai ni mzuri sana, ila lazma na wengine wacheze kwny nafasi yake ili siku akiumia au akiwa na kadi Pengo lake lisionekane.
Kimsingi timu inacheza mpira papatu papatu, haina maarifa. Hilo la rushwa ni kuwaharibia tu watu ili kuwajengea chuki. Otherwise ushahidi uwekwe.