Chuo cha Uhasibu Arusha chadaiwa kudahili Wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, wengine wasomea na kuishi Hoteli ya Ngurdoto

Chuo cha Uhasibu Arusha chadaiwa kudahili Wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, wengine wasomea na kuishi Hoteli ya Ngurdoto

vyovyote iwavyo lakini 5 star Hotel kuwa hostel ya chuo duni kama cha uhasibu Arusha sijawahi kuona
kingekuwa chuo duni kisingetambulika na serikali kwa maana ya TCU, na hotel ya nyota tano Ngurdoto isingekubali kuwapokea na kuwapa hostel wanafunzi waishi hapo... tena nimpongeze sana huyo mkuu wa chuo kwa kujiongeza kuwatafutia wanafunzi wake hostel zenye viwango vya kimataifa kwa gharama nafuu mno.
 
Kwani Mzee Mengi yuko hai? Yeye mbona biashara zake hazijafa na kuna ugomvi wa kifamilia huko? Acha upumbavu jamaa.
Je kuna management yenye kuweza kuendesha hiyo hotel, kwa Marehemu Machache umesikia Mabadiliko yoyote kwenye Management?? Je unajua maanuzi ya Mahakama juu ya Management ya biashara za Machache???
Acheni uzuzu wenu huko huko kwa mazuzu wenzenu
 
Though I can't feign knowledge of what exactly had transpired to Ngurdoto leading to this abysmal end, however, comparing with other businesses I know which had met the same end, they share one common denominator- a heavy burden of government taxes and other tozos kill businesses. In short, business climate in Tanzania at the moment is awfully unfriendly.....only a fool will plunge in head on!
Kuna ujinga na upumbavu, moja akieleweshwa habadilika mwingine hubaki hivyo hivyo .
Chagua moja kubaki hivyo hivyo au kukubali kuelemishwa na kujadiliwa.
Nenda shule ujue hizo kodi zinatozwa vipi ns jinsi gani zime athiri hiyo biashara.
 
Kila kona, watu kibao... Hii inanikumbusha mwaka 2005 wakati nimekwenda kujiandikisha kusoma ADA pale IFM.... Tulikuwa nyomii.. Nafasi zilikuwa first come, first served.. Nilichelewa kujiandikisha kutokana na kukosa tuition fee... Kuja kuipata siku mbili baadaye, nakuta nafasi zimejaa.. Ikabidi nikasome tu Banking n Finance!
 
Hiki hunifanya nipende biashara ya majengo.. Ukiwa na biashara ya magari, yakifa, unapotea kwenye ramani.. Lakini ukiwa na majengo, ni rahisi kubadili biashara... Hupotei kwenye ramani, mazima!
Awamu pendwa ikishapita tu Hali nzuri itarejea uchumi utakuwa unaondoa hostel inakuwa hotel.
 
Hao waswahili wakikaa humo watavunja mabomba na masink ukarabati wake utakuwa gharama hapo baadae.
Waangalie sana uamuzi huu
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
Pengine wenye hotel yao wameamua kubadili biashara, sioni sababu ya kulalamika hapo.
 
Hii hotel ilikuwa inategemea watalii kutoka nje. Sasa ni kipi serikali imekifanya kika zuia watalii kuja. Kuzuia bunge kurushwa live, kuzuia mikutano ya siasa. Naomba kueleweshwa?
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
Kwa kweli inasikitisha na kukatisha tamaa! Hii ndo kazi ya mikono ya Jiwe! Hatari sana!
 
Fanya 10 kabisa Somalia itakuwa na afadhali na kule hazina kweupeeee na BEBERUS wamesusa na misaada yao na mikopo. Mambo Kizimbambwe Zimbabwe tu mkate million huna una chanja mbuga.
Utasubiri sana hilo litokee na halitatokea nchi itasonga mbele tu hakuna nchi inaweza kupata maendeleo ya maana kwa kutegemea misaada.
 
Duuuh aiseee, hiyo yote ni tamaa ya pesa, bora system irudi kama zamani, TCU Ndio iwe kila kitu.
TCU bado ni kila kitu... Na inahusika na upuuzi huu kuvipendelea vyuo vya serikali...
Wakati wanafunzi wanalundikana huko utakuta vyuo vya private vyenye kozi almost sawa vikikosa wanafunzi na kujiendesha kwa mbinde...!!
Quality education is a lost cause in this country!!
 
Weka mkataba, pengine wenye hoteli wamebadili dira kutokana na Cocid-19. Wewe unafahamu watalii wamepungua, sasa pengine ni bora wapate kidogo kuliko kukosa kabisa. Bring the true story hatupo hapa kujadili majungu.
Kwahiyo watalii wamepungua kwenye hotel moja tu tena ya 5 [emoji93]?

Halafu Tanzania hatuna corona hao watalii kwanini hawaji na anga zilishafunguliwa kitambo.
 
View attachment 1638380
Chuo cha Uhasibu Arusha – Institute of Accountancy Arusha (IAA) kimedaiwa kufanya udahili kwa idadi kubwa ya wananafunzi kuzidi uwezo wake, jambo linalosababisha uongozi wa chuo kuhamishia wanafunzi wa baadhi ya kozi katika hoteli ya Ngurdoto.

Baadhi ya Wanafunzi hao ambao wamepelekwa Ngurdoto kusoma na kuishi ni kutoka katika kozi za:
•Bachelor in Business Management (BBM)
•Basic Technician Certificate in Business Management (BTCBM)
•Ordinary Diploma in Business Management (ODBM) mwaka wa 1
•Bachelor of Accountancy (BA) mwaka wa 1 & 2
•Basic Technician Certificate In Accountancy (BTCA)
•Ordinary Diploma In Accountancy (ODA) mwaka wa 1 & 2

Baadhi ya Wanafunzi wamelalamikia suala la kupelekwa Hotelini kwani awali waliomba kusomea Main Campus ambapo walishakodi vyumba karibu na chuo na kununua mahitaji ya kujikimu kama vile magodoro, majiko nk.

Wamesema sasa wanalazimika kulipa kiasi cha Tsh. 400,000 kama malipo ya Hosteli (huko hotelini)

“Kama chuo kimejaa kwanini wanachukua idadi ambayo wao hawawezi kumudu na kuanza kutusumbua wakati tumeomba main campus?”, amehoji mwanafunzi mmoja.

Wanafunzi wameomba kama Idadi imezidi ni bora baadhi ya Wanafunzi wahamishiwe Vyuo vingine.
Mh! Ninachojua ni kuwa watalii hakuna kwa hio ngurdoto haina wateja
 
Utasubiri sana hilo litokee na halitatokea nchi itasonga mbele tu hakuna nchi inaweza kupata maendeleo ya maana kwa kutegemea misaada.
Jaribu kumwambia spika wa bunge, kalamagamba kabugi na jpm kuhusu hilo uone watakwambia kitu... Hiyo misaada wanaikataa kwa maneno lakini kwa matendo wanaendelea kuipokea...
 
Back
Top Bottom