Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Chuo Kikuu cha Iringa kimelazimika kuwafukuza wanafunzi zaidi ya 50 baada ya kudukua mfumo wa malipo ya ada na kugoma kulipa ada ya kozi ya teknolojia ya habari (IT).
Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Ndilirio Urio amesema wanafunzi 256 walifanya udanganyifu wa malipo na Chuo kiliagiza matokeo ya wanafunzi wote yafutwe. “Seneti ilikaa jana wale ambao wamekubali kulipa ada, kukiri na kuomba msamaha tumewasamehe,” amesema wakati wa mahojiano na waandishi wa habari. “Wale wachache waliokaidi kulipa wamefukuzwa.”
Habari leo
Pia soma > Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wadaiwa kuingilia Mfumo na kuonekana kama Wamelipa Ada