Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru chamtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), leo Oktoba 10, 2023

Hongera kwake.

Kwa wivu wa machadomo na Sukuma gang watasema ameuza Bandari 😂😂😂

Nawakumbusha tuu Samia ameungana na Putin , Shinzo Abe Kuwahi kupata hiyo degree.

Aliyepewa na Mungu kapewa tuu ,mapovu mengine wayapeleke kupambania familia zao.
---
Chuo Kikuu maarufu nchini India cha Jawaharlal Nehru, leo Oktoba 10, 2023 kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa shahada hiyo na chuo hicho.

Rais Samia anapokea shahada hiyo ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kumtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari kutambua mchango wake katika kuboresha sekta ya elimu, uchumi, demokrasia, na usawa wa kijinsia nchini.

Chuo hicho kilianzishwa Aprili 22, 1969 na kupewa jina la Waziri Mkuu wa kwanza wa India, Jawaharlal Nehru, na kuwa moja ya vyuo vikuu bora nchini India na duniani kwa ujumla kikijivunia kuwa taasisi ya elimu ya juu ambapo watu maarufu wa India walipata elimu yao ya juu.

Baadhi ya majina maarufu yaliyoandikishwa katika chuo hicho ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Bw. Subrahmanyam Jaishankar, na Waziri wa Fedha, Bi. Nirmala Sitharaman, huku kikitoa Shahada ya Heshima kwa viongozi wawili pekee akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Hayati Shinzo Abe.

Shahada hiyo ya heshima imetolewa kwa kutambua juhudi za Rais Samia katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na India, kutokana na mafanikio yake katika uwanja wa kidiplomasia, haswa diplomasia ya kiuchumi, na mafanikio katika kuchochea maendeleo yanayojikita kwa watu nchini Tanzania.
 
[emoji736]Kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India

[emoji736]Diplomasia ya Uchumi

[emoji736]Mchango wake katika maisha ya kila siku ya Wananchi wa Tanzania


[emoji736]Mafanikio yake Kikanda na Kimataifa
 
Jamaa wajanja
 
LUKUVI! Kama nimemuona Lukuvi, au macho yangu yana ukungu? Nijulisheni wakuu.
 
Hongera Mheshimiwa Rais. Hongera sana Mama Yetu Mpendwa. Msukuma na Babu Tale sijui walihudhuria?
 
Vyeti vya kijinga ile mbaya. Akiwa huko wanamuuliza anataka cheti Cha aina gani kisha wanampa kama anavyotaka. Halafu bila aibu utasikia chawa wananza kumtaja kwa hicho cheo bortion.
Wala usijali watamuuliza Mbowe 🤣🤣
 
Sidhani kama Mbowe ana muda wa na hivyo vyeti vya kiduwanzi. Na ikitokea na yeye akashobokea vyeti vya aina hiyo, na yeye atakuwa mshamba fulani tu.
Angekuwa hana.mda nyie chawa wake msingekuwa mnahangaika
 
haya majamaa ni kama wameshajua weakness yetu!
Unaonekana wanampamba kama walivyofanya wale waarabu wa depi wedi ila nao watupige na kitu kizito kichwani.
Hata watu unaondamana nao dunia inajua hawa watu hawako serious!
Kweli tunatumia pesa za walipa kodi kwa watu kama steve nyerere! hapana!
 
Tangu Jakaya Kikwete atunukiwe PhD ya mashaka na kuanza kujiita daktari wakati hata master's hakuwa nayo, umeibuka mchezo mchafu wa kuwapa shahada za heshima honoris causa marais wetu ambao elimu zao kama si za kuunga au kughushi, zinatia shaka. J

e hii kama siyo kuwafanya vijana wetu wakose motisha wa kuzihenyekea mbali na kudhalilisha shahada hizi ni nini? Je wanazistahiki?

Je wanapaswa kujiita madaktari wakati wengi ni vihiyo? Je ni kwanini hawaoni aibu hii au ni kwa vile ni vihiyo? Je kuna namna wanafanya nyuma ya pazia ili kupewa shahada hizi chafu? Je kwanini tusitunge sheria za kuzuia jinai hii ya kiakili na kimaadili?
 

Attachments

  • PhD ZA AIBU NA AJABU.jpg
    26.2 KB · Views: 2




Swali la msingi kwanini hicho chuo hakika mpa heshima hyo waziri mkuu Wai ndugu naendra mondi hyo heshima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…