CLOUDS: Mishahara ya walimu inadhalilisha utu wao

Wengi wao hata kula Yao ni Mara moja Kwa siku
 
Mkuu basi uwe na adabu hata kidogo na changamoto wanazopitia walimu. Chochote kile unachojivuna nacho wewe hivi sasa kuhusu suala zima la elimu uliyokuwanayo ni zao la walimu.
 
akili kisoda
 
jamani waacheni walimu hawana fursa bali wanategemea hiyo mishahara tu.hawana posho hata hivyo vishikwambi kama hawatawekewa bando bado itakuwa ni vigumu kuvitumia.yatakuwa ni mapambo tu ya mkononi.
 
Mnazurula = mnazurura, madaftali = madaftari. Watu wengine ni kama vile mna laana au hamkupata malezi mazuri.
 
Mie niliandika Uzi humu kuhusu Hali mbaya ya walimu,nikashambuliwa na kuonekana mwongo,maisha ya mwalimu ni mabaya sana,mwalimu anazidiwa na muuza mchicha ambaye anauhakika wa kupata hata 2000 daily,
 
Inaonesha wazi wewe ilikosa hii ajira. Waalimu hawa hawa au wengine ? Unafika shule ya Msingi kumefurika. Magari ndani ya parking ya Waalimu utafikiri showroom pikipiki hazina idadi .

Hebu hiyo media ituambie kwanza mwalimu wa certificate diploma na degree wanalipwaje?

Tuanzie hapo kwanza halafu tufananishe na kada zingine kama vile manunuzi,utumishi,uhasibu,kilimo,mifugo n.k

Vinginevyo wana ajenda yao nyuma ya pazia
Hauna uelewa wote kuhusu kipato,mwalimu Hana kipato nje ya mshahara,hao wote wengine Wana allowance kibao na wengine zinazidi mshahara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…