Club Africain 0-1 Young Africans | CAFCC Playoff | Yanga yatinga hatua ya makundi

Club Africain 0-1 Young Africans | CAFCC Playoff | Yanga yatinga hatua ya makundi

Mnapangiwa lini wa kucheza nao ili tujue kama tunainua tanga kumbe marehemu hakufa alizimia tuu au tuendelee kusubirisubiri labda atadedi kabisa kwenye hatua ya makundi?
Anaitwaje marehemu ikiwa huna uhakika kama kakata roho?
 
FULL TIME: Yanga inafanikiwa kufuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

90' Zinaongezwa dakika 4 za nyongeza
89' Bakari Mwamnyeto anaingia anatoka Morrison
88' Wenyeji wanaonekana kama wamkata tamaa, wanapata kona
80' Yanga wameanza kucheza vizuri zaidi, wanamiliki mpira
Azizi Ki anaipatia Yanga goli kwa shuti la mbali akimalizia mpira wa kichwa wa Mayele
78' GOOOOOOOOOOOOOOOOO

72’ Mabadiliko kwa Yanga, Moloko anatoka anaingia Farid Musa
69’ Morrison anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
68’ Mabadiliko kwa Yanga, Azizi Ki anaingia anatoka Aucho
64’ Kipa wa Yanga, Diarra yupo chini akitibiwa, mwamuzi anampa njano akiamini anapoteza muda
62' Azizi Ki anapasha misuli, anaonekana anajiandaa kuingia
60' Mabadiliko ya wachezaji wawili wa Club Africain yanafanyika
55' Utulivu bado ni wa kiwango cha juu kwa Yanga
50' Wenyeji wanaongeza kasi lakini ukuta wa Yanga bado ni mgumu kupitika
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

45' Shuti kali langoni mwa Yanga lakini Diarra anadaka
40' Kasi ya mchezo imepungua
33' Khalid Aucho anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
27' Yanga wanaonesha utulivu na ndio wanamiliki mpira muda mwingi
25' Yanga wanafanya shambulizi kali lakini kipa wa Club Africain anaudaka
15' Yanga wanaonekana kuwa na utulivu na kupiga pasi kadhaa
10' Wenyeji wanajaribu kuongeza kasi ya mashambulizi
5' Presha ya mchezo ni kubwa, Yanga wanaonekana kuupoozesha mchezo
Mchezo umeanza



Leo ndiyo ile siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu huku wengine wakiisubiri kwa hofu kubwa. Mechi itakuwa saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki!

Mechi itakayoamua nani anaenda makundi CAFCC. Ikumbukwe kuwa matokeo ya mchezo wa kwanza uliisha kwa sare ya bila kufungana uwanja wa B. Mkapa-Lupaso.
Wewe Mpuuziiiiiii uso wako utauweka wapi?!!!!!!
 
Kila nikijaribu kuiombea yanga kuna sauti inasema ndani yangu kwamba "USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO". Basi naamua kuitii hiyo sauti mana staki dhambi mimi. Wachezaji wa Yanga wanatamani wangepata ajali kama ile ya precision air ili kuficha aibu yao kwa taifa .
Endelea kuitii hivyohvyo
 
Back
Top Bottom