Club ya Rio-De-Janeiro iliyopo bukoba mjini sio salama tena kuelekea mvua za Elnino

Club ya Rio-De-Janeiro iliyopo bukoba mjini sio salama tena kuelekea mvua za Elnino

Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko dhidi ya club ya Rio De janeiro iliyopo BuKoba Mjini mali ya Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Bukoba Mjini JOAS MUGANYIZI ZACHWA @ PEDESHEE kwamba imejengwa karibu kabisa na Mto Kanoni kinyume na sheria za NEMC.

Mara zote walioleta hoja hii wameonekana wabaya kwa wafuasi wa ZACHWA, Wametukanwa na wakati mwingine kudhalilishwa kupitia mitandao ya kijamii.

NEMC wameshatembelea eneo hilo na hakuna lolote lililofanyika licha ya club hiyo kumwaga maji taka kwenye mto huo.

Wakati wa ujenzi wa daraja la kanoni siasa ilitumika jengo hilo halikubomolewa sasa muda umefika ukweli unaanza kuonekana wazi kingo zimetanuliwa kurusu maji kupita kama sehemu ya maandalizi ya mvua za Elnino ukuta wa club hiyo kwa sasa ndio kingo jambo ambalo ni hatari wa usalama wa watu mana tayari foundation ya jengo hilo ipo uchi kabla ya mvua kunyesha.

Zachwa kwa sasa anatafuta mchawi bila kujua lilikua swala la muda tu.

Sitashangaa akiendelea kuwepo hapo licha ya hatari iliyopo kwa sababu tu ni mwana CCM.

VIONGOZI WA WILAYA YA BUKOBA NA MKOA WA KAGERA KWA UJUMLA TIMIZENI WAJIBU WENU AU SUBIRINI MAAFA NDIO MSTUKE.

View attachment 3683162View attachment 3683170View attachment 3683164View attachment 3683163
Aisee! Hapo ni kilabuni panapouzwa pombe za kienyeji au ni club watu wenye pesa zao wanaenda kula bata? Mbona panaonekana panatoa harufu ya uozo muda wote kutokana na hayo maji ya mto!
 
We nae

We nae unalako jambo na huyo kada mwenzio, karibu dar uone mito na watu walivyojenga
Sawa Mkuu ila Dar sio sehumu ya kuhalalisha uovu.... sio kwa sababu Kuna mashoga wengi Dar basi ni sawa bariadi pia wawepo wengi
 
Aisee! Hapo ni kilabuni panapouzwa pombe za kienyeji au ni club watu wenye pesa zao wanaenda kula bata? Mbona panaonekana panatoa harufu ya uozo muda wote kutokana na hayo maji ya mto
Mkuu eneo pendwa sana hilo mkuu ulichosema ni matusi kwa watu.
 
concern ilikua yanayoendelea nje na ndo mana hata upande wa mbele haujapigwa picha.
 
Haya mabanda ndo klabu za huko Bukoba?
 
Mbona pachafu, hiyo klabu imekaa kama machinjio ya kuku pale Tandale sokoni.
 
Back
Top Bottom