Code number ya simu ya Zanzibar ni +259 , hii +255 tunayotumia ni ya Tanganyika

Bora wabaki na ka nchi kao.
Zanzibar yenye ukubwa sawa na wilaya ya Rufiji wamezeza mpaka kumweka Rais madarakani huku Tanganyika, huku Tanganyika tumeshindwa hata kumweka Mwenyekiti wa mtaa mwembe togwa kule Zanzibar.
Msiwabeze tuwasaidie wajikomboe kumbuka ndo nchi ya kwanza east Africa kuwa na shilingi yake 1800
 
Muungano unashida zake. Kwangu Mimi nakerwa sana na mgawanyo wa maeneo ya kiutawala na nafasi za kisiasa.
Tanzania ikiwa na ukubwa wa eneo mraba 945087 na mikoa 31 , eneo kule Zanzibar lenye mikoa 5 (16%) ni kilomita mraba 2461(0.2%) sawa na tarafa moja ya wilaya ya Urambo. Idadi ya watu ni kama million 1.5 (2.5%) ya 60mls Tanzania
Eneo hili na watu hao wana wabunge 70+(majimbo, viti maalum, wabunge wa toka baraza la wawakilishi), mawaziri kadhaa, mabalozi kadhaa watumishi waandamizi, wakuu wa taasisi nk.
Yaani baadhi ya majimbo yana wapiga kura 5,000 tu..!!
eti kila baada ya 6km by 6km kuna mbunge!!??
kwamba misaada na mikopo wapewe 4%..!! Wakiwa na Eneo LA 0.2% na watu 2.5% tu.
Bado watu hawa wanalia na ajira za ualimu!?
Bado hawataki muungano!!! Tunawabembeleza!!
Nafikiri tujitafakari upya.
Nadhani Hata sababu kuu ya mzunguko mkubwa wa pesa ni hizi fursa

Watu wenye fursa hizi ndio kwanza wanazingua.
Tutafakari
 
Kumbe ni issue ya muda mrefu. Nadhani Mheshimiwa ameamua kutumia platform ya position yake kujipatia political milage.
Issue ya Muungano huwa ni hoja ya kubakia relevant Kwa wanasiasa wa kutokea Zanzibar hivyo si ajabu hata yeye kuitumia ili abakie relevant.
 
Haipendezi kuwa sehemu ya wanaosimamia Sheria halafu unatetea mtuhumiwa openly huko ni kuvuruga mchakato mzima wa mamlaka ya kutoa haki,

Ni kuinfluence outcome ya hukumu.

Jambo ambalo ni kinyume Cha taratibu za Utawala Bora.
 
Nitajie nchi (kisiwa) mojawapo duniani ambayo inamiliki sehemu ya nchi kavu.
 
Mara nyingi wajinga huwa hawana hoja, jaribu kuwauliza Canada kwanini dialing code yao ni +1. Kama unadhani JF imejaa mambumbumbu utakuwa unakosea sana, ujinga kama huu unatakiwa kuupeleka vijiweni.

Kuna issues nyingi sana zinazomsumbua mzanzibar dialing code haipo kwenye orodha, hata kama ungetumia dialing code ya Oman reception au ujumbe kwenye simu usingebadilika.
 
Zanzibar halisi ilikuwa ni serkali ya Muungano wa Oman na Zanzibar, ikawa Zanzibar was the richer brother (shauri ya watumwa na meno ya tembo, Muscat ilikuwa na tende tu). Ilikuwa ni Muungano wa serikali 2 siyo 3.

Mwaka 1882 makao makuu yakatoka Muscat yakahamia Zanzibar, lakini Serkali ya Muungano, yaani Zanzibar, ikatoa Indian Rupees milioni 3 kufidia (hiyo ndiyo ilikuwa forex account ya Sultan), Kaka mtu Sultan Seyyid Sayid akampa mdogo mtu Sultan Seyyid Thuweini kufidia, from his personal pocket, mdogo mtu akabaki Muscat na serkali yake. Muungano ukaendelea, Oman na haluwa yake, Zanzibar na watumwa wake, hadi mwaka 1963.

Mwaka 1963 makubaliano ya Lancaster House yaliyozaa "Uhuru" wa Sultan Zanzibar yalifikia muafaka wa Uhuru uwe 1963 (na kweli uhuru ukapatikana lakini kina Karume hawakufurahi), lakini swala la kilometa 20 za Bara liliachwa "pending" naona sasa Makamo anataka kulifufua.

Kumbuka kuwa "Zanzibar" ilijumuisha Unguja, Pemba, Mafia, Lamu, Malindi, Mombasa, Sofala, na kilometa 20 za pwani ya Tanganyika (yaani Muheza hadi Nachingwea) na Kenya. Hizo ndiyo Country Code +259 iliyotolewa na ITU na ndiyo maana haijatumika. Kama anaitaka code +259, mpeni Makamo zisaidie kuwachangia (kwa M-Pesa) magaidi wa UAMSHO, wengi asili yao ni Waarabu wa Oman.

Huyo Makamo wa Kwanza wa SMZ anaelewa "M" stands for what and why?
 
Hizo ni ndoto za Alinacha! Eneo la Zanzibar ni visiwa viwili tu vikubwa! Unguja na Pemba! Hizo ni Hekaya za Abunuwasi za mikataba ya Wazungu na yule Sultan wa Oman, hazituhusu Watanganyika.
Mdau ana hoja usibeze, fuatilia ujue kwenye ukanda wa uchumi wa bahari ( exclusive economic zone EEZ) tukivunja Muungano Watanganyika tunabaki nanini?
Fuatilia kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…