COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Tatizo unadhani kila unachoona kizuri au kinachoonekana kizuri ni kizuri kwa kila mtu au kwa idadi kubwa ya watu,ngoja nikupe tukio lililotokea wala sio siku nyingi ....

Mahali ambapo nimepanga kwa maana ya kuishi kuna jamaa aliwahi kukaa siku mbili bila kula wala kutoka nje,kabla ya kutimiza siku mbili akiwa ndani,kuna jamaa yetu ambae tunaishi nae hapa nyumbani alikwenda kumuuliza kulikoni baada ya kumuona siku moja nzima hajatoka nje na kufanya mambo yake kama alivyozoeleka

Jamaa huyu alikwenda na kumuuliza kulikoni lakini jamaa alimuambia "ana mambo yake tu" hivyo hakuna tatizo lolote,alimuuliza kama hajala jamaa akamuambia kwamba hajala,jamaa alitoka na kwenda kumletea chakula,lakini jamaa aliekjuwa ndani akamuuliza kama amemuambia kama anahitaji chakula,alieleta chakula akamuambia kwamba amemuambia kwamba hajala tangu jana hivyo atajidhuru kwa kukaa muda mrefu bila chakula

Kisha akampa chakula,jamaa alikipokea na kumwagia chakula yule aliemletea na kumuambia asimsumbue tena

Mfano wa tukio hilo unaweza tu kuona kwamba sio kila chekundu ni red na ukifikiri kwa makabala huo ni hatari sana na ndio maana Mungu akaweka free will,kama unahitaji kuponywa mwambie,kwa Munmgu kujua tu kwamba wewe unaumwa na unahitaji kuponywa sio tiketi ya kukuponya kwasababu unaweza kusema na ukaponywa

Lakini pia unapaswa kujua kwamba hata maradhi ambayo mtu anaweza kuugua au anaugua ni matokeo ya uchaguzi wake mwenyewe na anajua kabisa ni mabaya,sasa mtu ulichagua mwenyewe,unatakaje tena uponywe tu bila kusema hitaji lako?
 
Majibu ya maswali yako haya hapa chini ......

 
Sasa wewe unaeona "kashindwa" hebu tupe creation yako yoyote ile uliyo i create so far.

Unachanganya mambo.

Sikusema mimi mungu ninayejua yote na kuweza yote.

Nimesema mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote asingeweza kuumba kitu ambacho hakima hata energy efficiency.

Mambo mawili tofauti.

Usichanganye.

Umekubali kwamba binadamu hana optimal energy efficiency na hivyo hana markings za kuwa kaumbwa na mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote?
 

Hujalijibu, weka link hapa kama umelijibu.

Mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote ameimbaje binadamu ambaye hana hata energy efficiency?
 

Hapa kinachoendelea ni cognitive dissonance tu.

Watu washakunywa maji ya dini na kuamini mungu kwa muda mrefu sana, sasa hata wakiona imani yao hawawezi kuitetea kimantiki watabisha tu.

Ni kama mtu anavyoweza kuibishia DNA test baada ya kuonyeshwa majibu kwamba mtu aliyefikiria ni baba yake wa kibaiolojia aliyemlea kwa miaka 50, kwa kweli kibaiolojia si baba yake.

Mambo mengine magumu sana kukubali.
 

Freedom of choice ipi hiyo?

Mie hata sikuulizwa kama nataka au sitaki kuzaliwa, nimejikuta tu nimezaliwa. Sasa hapo nimepewa freedom gani kuanzia mwanzo kabisa?

Pia nataka uwezo wa kurudi nyuma katika muda, sijapata ywezo huo na kwa fizikia yabuumbwaji wa ulimwengu huu siwezi. Freedom iko wapi hapo?

Kama uumbaji wa binadamu ndiyo kilele cha ubira wa uumbaji wa mungu, basi kapata big fail.

Binadamu hana optimal energy efficiency, imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba binadamu bila ya kuweka optimal energy efficiency?
 
bagamoyo Dr. Stenger nimemsoma articles zake. Nitatafuta hivyo vitabu. Ameelezea vizuri sana.Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Hujalijibu, weka link hapa kama umelijibu.

Mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote ameimbaje binadamu ambaye hana hata energy efficiency?
Haya jisomee hapo.........
 

Kwa hiyo ujuzi wa mungu wako ni sawa na ujuzi wa mpangaji mwenzako kuhusu mpangaji mwingine?

Kwamba mungu anaweza kumpa mwanadamu kitu akifikiri kwamba mwanadamu anakihitaji, halafu ikawa mwanadamu hakihitaji na hivyo mungu akawa kakosea?
 
Haya jisomee hapo.........

Jibu lako linazidi kum contradict mungu.

Unaanza kwa kuandika kwamba kumpa mtu kile anachotaka ni upendo.

Binadamu wengi hawataki kufa, mungu ana uwezo wa kuondoa kifo, hajafanya hivyo. Hivyo, kwa mujibu wako, mungu hawapendi binadamu.

Pia.

Kwa nini mungu anapenda sana binadamu wamtii?
 
Kwa hiyo ujuzi wa mungu wako ni sawa na ujuzi wa mpangaji mwenzako kuhusu mpangaji mwingine?

Kwamba mungu anaweza kumpa mwanadamu kitu akifikiri kwamba mwanadamu anakihitaji, halafu ikawa mwanadamu hakihitaji na hivyo mungu akawa kakosea?
Hii inasikitisha sana .....

Kwanza ungesoma kile ambacho Ngabu aliniandikia halafu ukasoma kile ambacho nimemjibu ndio ungeelewa sababu ya mimi kumpa huo mfano wangu

Lakini pia cha ajabu ni kwamba umeshindwa kabisa kuelewa logic ambayo nimeitumia kujenga hoja ya mfano wangu na atokeo yake umeubeba mfano mzima mzima,hili ni tatizo lako na mara nyingi sana limeonekana wakati wa mijadala ya aina hii

Hapa bila kutoka huko kwenye box na kuamua kujifunza ukiwa huru bila kuweka hisia zako ambazo naona ndio zinakuongoza kujibu,hutaweza kuelewa kamwe

Inaonekana kuna jambo ulishalifanya au ulishayafanya sasa unaona njia sahihi ya kutokuumia ni kutafuta wa kumsingizia ili ujiridhishe.pole sana hapo umeongeza tatizo na sio kulitatua .....!
 
Jibu lako linazidi kum contradict mungu.

Unaanza kwa kuandika kwamba kumpa mtu kile anachotaka ni upendo.

Binadamu wengi hawataki kufa, mungu ana uwezo wa kuondoa kifo, hajafanya hivyo. Hivyo, kwa mujibu wako, mungu hawapendi binadamu.
Unafurahisha sana ....

Unarukia kwenye kufa bila hata kujiuliza aliesababisha kifo kikawepo ni nani ...
Pia.

Kwa nini mungu anapenda sana binadamu wamtii?
Kutii sio hitaji la Mungu bali la binadamu,elewa kwanza hilo .....!!
 
Lahaula, wazungu na matheory yao yanawapeleka watu kubaya..
Hivi kwa nini kiranga unapenda kutumia akili za ki binaadamu kudhibitisha uwepo wa mungu?

Kwanza kabisa, elewa tofauti ya kudhibitisha na kuthibitisha.

Pili kabisa, mimi ni binadamu, unataka nitumie akili gani? Za Pundamilia?


Hujathibitisha kwamba mungu yupo. Hao hao unaowasema wamekuletea internet unayoitumia leo kuwatukana. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Kama nimeweza kukuuliza maswali ambayo huwezi kuyajibu bila hata ya kutumia 10% ya ufiiri, nikifikisha 50% utakimbilia wapi?

Kwahyo sishangai siku moja hapa, tukiwa hai maana uhai nayo ni fate tutakuja kuona hapa mnageuza kiswahili kua mungu yupo!

Siku moja tukiwa hai maana yake nini? Leo hatuko hai?


Hujajibu maswali, na unaongeza maswali tu.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao unaweza kuwa na viumbe wake wasiokamilika katika elimu ya mungu?


Kwa sababu mungu wako alishindwa hii kazi, au siyo?


Kwa nini mungu wako mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote atake kusaidiwa kazi yake ya uumbaji na binadamu wasio na ujuzi wote, upendo wote wala uwezo wote?

Otherwise punguza bla bla zako, na mwisho usijekupata hasara ya kukufuru kama waliotangulia.

Kati yangu mimi ninayekuuliza maswali usiyoweza kuyajibu, na wewe ambaye sio tu huwezi kujibu maswali ninayokuuliza, bali pia kila unapojaribu kuyajibu unazalisha maswali mengine ambayo huwezi kuyajibu, nani analeta bla bla hapa?
 
Unafurahisha sana ....

Unarukia kwenye kufa bila hata kujiuliza aliesababisha kifo kikawepo ni nani ...

Kutii sio hitaji la Mungu bali la binadamu,elewa kwanza hilo .....!!

Aliyesababisha kifo kikawepo ni nani?

Na kutii ni hitaji la binadamu kivipi?
 

Logic gani uliyotumia?

Umetoa mfano wa mpangaji kuonyesha kwamba kumpa mtu kitu bila kuombwa kwa kufikiri anakihitaji kunaweza kuwa si kitu kizuri, kwa sababu anaweza kuwa hakihitaji.

Unaweza kumpa mtu chakula kwa kuona hatoki ndani, kumbe mwenzako kafunga na hataki kusumbuliwa.

Mfano huu unatuambia kwamba unamlinganisha mungu anayejua kila kitu na mpangaji asiyeweza hata kuona ndani ya chumba kilichofungwa seuze mawazo ya mtu tofauti.


Mfano wako umeujenga katika msingi mbovu, wa kulinganisha visivyolingana.

Mungu wenu kwa kumpa uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, mnamfanya awe rahisi zaidi kukanushwa uwepo wake.
 
Aliyesababisha kifo kikawepo ni nani?
Ndio maana nakuambia either husomi nilichokuwekea hapo juu aua umesoma hujaelewa

"Aliechagua dunia ikawa kama ilivyo leo ni binadamu" hujaona hii kauli?

Najua kuna maswali meengi yametiririka kichwani mwako baada ya kusoma hapa,nakushauri rudia kusoma tena nilichoweka hapo juu kuna majibu ya maswali hayo
Na kutii ni hitaji la binadamu kivipi?
Unapomtii baba yako kwa kumsikiliza anapokuelekeza inakuwa ni kwa faida ya nani?

Baba yako au wewe?
 

Hili la huu mfano limekuzidi uwezo wako wa kutafakari na hutaweza kulielewa,achana nalo...

Nilishajaribu kukuelewesha sana na nikawa kama napigia mbuzi gitaa tu!
 

Binadamu angewezaje kuchagua dunia iwe kama ilivyo leo kama uwezekano wa dunia kuwa kama ilivyo leo usingekuwapo kabla ya binadamu kuwepo?

Kumtii baba wa mtu si kwa faida ya mwana. Kuna mababa mabazazi wanabaka watoto wao, hao nao unataka kusema watoto wawatii?

Unamfananisha mungu na baba wa kidunia?

Your thinking is authority based, and therefore outdated.
 
bagamoyo Dr. Stenger nimemsoma articles zake. Nitatafuta hivyo vitabu. Ameelezea vizuri sana.Thanks.

Mkuu,
Nimeona nitupie ''articles'' za wachambuzi toka sehemu nyingine ili sisi wana-JamiiForums tuone wadau ambao wapo ktk mitandao mingine uchangiaji wa ''arguements'' zao ktk mada unaweza kutoa ''changamoto'' kwetu sisi kutoa michango ya hoja iliyokuwa na hoja zilizojaa angalau sources za kukufanya ufikirie na kujiuliza.

Kiranga mie hufurahia kuona jinsi unavyotoa changamoto ktk mada kisayansi zaidi ukiweka ''imani'' pembeni kwanza na husikitishwa sana kuona watu wa ''imani'' wakijenga hoja nyepesi wakati hata ktk ''imani'' pia wanaweza kuja na hoja nzuri tu wakitulia na kujisomea toka source mbalimbali.

Mkuu, Kiranga endelea kutoa changamoto ili watoa mada wa kutetea/kupinga hoja waje wakiwa na hoja kamilifu iliyofanyiwa kazi au kama wana maswali basi waulize iwe ya kisayansi au kiimani tupate ufahamu au sababu gani wanaifagilia mada yao.
 
Hili la huu mfano limekuzidi uwezo wako wa kutafakari na hutaweza kulielewa,achana nalo...

Nilishajaribu kukuelewesha sana na nikawa kama napigia mbuzi gitaa tu!

Sitaweza kulielewa mimi wakati wewe ndiye umelikoroga kwa kufananisha visivyofanana?

Umevunja the number one rule of analogy, do not compare apples to oranges.

Kama kwenye hesabu hapo tungesema umegawanya kwa sifuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…