Tetesi: Col Joseph Karegire wa Jeshi la Rwanda auawa huko DRC Congo

Wale Wakimbizi waliokimbilia Benako Ngara walisharudi kwao hata wale waliokimbilia Goma wengi wamerudi kwenda kulijenga taifa lao la Rwanda.
Vipi kuhusu hao waliopo huko Drc, Msumbiji, Zimbabwe, Africa kusini na nchi zingine za ulaya magharibi wao hawana haki ya kurejea kwao Rwanda?
 
Define Kabila
Hawa jamaa kinachowafanya kuwa wa makabila tofauti nini?......

Lugha moja....mfumo wa utawala toka zama mmoja....dini za tamaduni moja....tofauti tu muonekano na mmoja mfugaji mwingine mkulima.
 
Kwa nini Kagame hataki kukaa na hao FLDR meza moja waasi ila anataka Congo ndo ikae na waasi meza moja?
 
Vipi kuhusu hao waliopo huko Drc, Msumbiji, Zimbabwe, Africa kusini na nchi zingine za ulaya magharibi wao hawana haki ya kurejea kwao Rwanda?
Wengine walihusika kwenye Genocide sasa wanajiona na hatia na wengine nimewakuta huko Zambia na Malawi wanamaisha mazuri sana na wanasema hawataki kurudi mpaka Jamii yao itakapotwaa madaraka.

Wengine tuko nao hapa Tanzania hawataki hata kuisikia Rwanda na ndio maana kwa sasa Waha na Wahangaza ni makabila yanayokuwa kwa kasi,hata Kenya.
 
Vipi wale wengine ambao hawakuhusika na genocide ila wapo uhamishoni kwa sababu za kisiasa?
 
Vipi wale wengine ambao hawakuhusika na genocide ila wapo uhamishoni kwa sababu za kisiasa?
Hao kila Nchi za Kiafrika wapo mfano mzuri ni akina Lissu na wenzake mpaka Wazungu walipotishia kukata misaada ndio lakini Magufuli angelikuwepo mpaka leo wangelikuwa nje ya Nji.
 
Genocide ni neno ambalo wanyarwanda wanafichama na kudekea Ili wahalalishe uhuni wao.

..tusidharau machungu waliyoyapata, na wasiwasi walionao kuwa genocide inaweza kujirudia.

..vilevile tuwahimize wasiwe sehemu ya mauaji na mateso dhidi ya jamii nyingine, na majirani zao wa DRC.
 
Upuusi
 
Hao kila Nchi za Kiafrika wapo mfano mzuri ni akina Lissu na wenzake mpaka Wazungu walipotishia kukata misaada ndio lakini Magufuli angelikuwepo mpaka leo wangelikuwa nje ya Nji.

..Kagame asiposuluhishwa na wapinzani wake walioko DRC kila siku atakuwa anatafuta kisingizio cha kuivamia nchi hiyo.

..pia tusisahau kwamba Kagame aliuwa wakimbizi wengi wa Kihutu kwa tuhuma za kuhusika na genocide wakati wa kumuondosha Mobutu, na wakati walipomvamia Kabila Snr.

..Zaidi kuna operation za RPF kuwafuatilia Fdlr zimefanyika ndani ya DRC wakati Kabila Jnr alipokuwa madarakani.

..Vita katika ardhi ya DRC imesababisha vifo kwa mamilioni, mateso, na uharibifu wa kila aina. Ni wakati sasa mahasimu katika vita hiyo wakaweka silaha zao chini, na kuridhiana kupitia mazungumzo ya amani.
 
Vipi kuhusu huyu mwamba aliyekuwa anawapiga mabanzi wazungu pori, bado yupo...?


 
Hao kila Nchi za Kiafrika wapo mfano mzuri ni akina Lissu na wenzake mpaka Wazungu walipotishia kukata misaada ndio lakini Magufuli angelikuwepo mpaka leo wangelikuwa nje ya Nji.
Kagame anawaua hata wakiwa huko ukimbizini.
 
Kabisa mkuu, raia waliokufa Drc ni wengi karibia mara 5 ya waliokufa kwenye genocide ya Rwanda mwaka 1994.
 
Kagame asiposuluhishwa na wapinzani wake walioko DRC kila siku atakuwa anatafuta kisingizio cha kuivamia nchi hiyo.
Majeshi ya Uganda hata sasa hivi tunavyoongea yako Kongo ya Mashariki yakipigana na Waasi.

Sasa ni kwanini Kagame asiruhusiwe kwenda kuwapiga FLDR na kuwatokomezea kwenye mapori ya Kongo?

Mbona Burundi wako DRC wanapigana na Waasi.

Lakini akifanya Kagame inakuwa ni Nongwa.
 
.Zaidi kuna operation za RPF kuwafuatilia Fdlr zimefanyika ndani ya DRC wakati Kabila Jnr alipokuwa madarakani.
Hizi operation zimefanyika mara nyingi mno toka mwaka 1996 hata watu kama kina Bosco Ntaganda, Laurent Nkunda walipewa kazi hii na Rwanda ya kuwawinda FDLR lakini bado FDLR wameendelea kuwepo......

Hili la kwamba askari wengi wa FDLR ni watoto wa wakimbizi wa kihutu waliozaliwa huko Drc baada ya genocide limekuwa halitajwi kabisa.

zitto junior Tresor Mandala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…