#COVID19 Corona iko maeneo gani Tanzania?

#COVID19 Corona iko maeneo gani Tanzania?

Ni sawa mkuu, Hata mimi nashangaa. Huku Mtaani maisha yapo normal ila ukisikiliza kauli za viongozi unaweza dhani hali ni ya kutisha. Nafikiri viongozi wanafanya hivyo kutufanya tuchukue tahadhari,ila kiuhalisia si kiiiivo!!!.Tuendelee kuva barakoa na kusanitaizi.
Utafiti wako umeufanyia mtaani kwako tu?
 
Acha kwenda Hospitali,wamekufa watatu.
Tena hii ya sasa hata unaweza kupuuzia kwenda Hospitali,ila ikakubananisha ghafla,usipopata mtungi wa gas,umeisha ndugu.

Kibaya zaidi,unajisikia mnyonge kidogo,una homa kidogo na kibaridi tu.Ila unakuja kupata shambulizi kali mno la ghafla.Unakuwa kama umeminywa na chatu.Mbavu zote hazichezi tena,hapo unakufa huko ukijiona
Hivi unaelewa maana ya mtaa au unataka kusema nyumba zako za jirani?

Je katika mtaa wako unarecord za watu wangapi wamekwenda hospital leo?

Tusiwe na hisia za kijinga jamani!!
 
Mchana huu rafiki yangu tuliyesoma wote msingi na sekondari anazikwa makaburi ya kondo bahari beach kwa shida hizi hizi za covid.

Mleta uzi chunga sana uandishi wako wenye dharau.
 
Hii kitu haiitaji dhihaka, ulimwengu umetambua uwepo wa corona, serikali inatambua na inahubiri kila siku watu wajikinge kwa kuchukua tahadhari.

Wakuu tuendelee kuchukua tahadhari kila inapowezekana. Tuachane na keyboard warriors waliojua huu mtandao juzi juzi.

[emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Wazee wa kuchukulia kila kitu masikhara...

Hii makitu ni vile tu Mungu kasaidia haipo fatal kama maukimwi au makansa, just being an airborne ingetupukutisha sana Waafrika kwa sababu huwa hatujali sana tahadhari...
 
Lengo la kupiga hiyo picha ni nini?
Anakuonyesha mitungi ya gesi pale MSD iliyoletwa kwa ajili ya wagonjwa wa Korona. Wewe endelea kuamini unavyoamini na acha kuchukua tahadhari lakini tambua kuwa siku likikupata ni lako na familia yako. Na ukifa hasara ni kwa familia yako.
 
Back
Top Bottom