Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Hali halisi inajionesha vp? Unatakiwa utoe ushahidi kwamba Mungu anataka kuondoa magonjwa ila anashindwa wakati anadai ana uwezo wote au utupe ushahidi kwamba Mungu alitaka kuumba ulimwengu ambao hakutakuwa na magonjwa na mabalaa ila alishindwa,hapo ndio tutahoji madai ya Mungu kuwa na uwezo wote wakati kuna mambo yanamshinda. Sasa wewe unakupuruka kusema dunia ina mabalaa halafu et mbona tunaambiwa Mungu ana uwezo wote!

Huku kushindanisha dini na sayansi ni ujinga wenu lakini dini haifanyi kazi za sayansi mpaka tushindanishe,mbona hamsindanishi dini na tiba za asili au na mambo mengine?
Maisha yana mambo mengi yakiwemo hayo masuala ya tiba,sayansi na mengineyo na yote hayo yanafanywa na watu wenye dini na wasiokuwa na dini. Tatizo hapa ni kama vile dini ni kikundi cha watu fulani kimejitenga na jamii hakujihusishi na mambo ya ulimwengu.

Na ndiyo maana nakwambia hata huko kwenye sayansi wako watu wa dini,kwenye tiba tofauti tofauti wako watu wa dini kila sehemu watu wa dini wapo.
 
Masahihisho madogo : Mashehe na wachungaji walipata ukimwi wanachukua ARV bila kificho chochote , binafsi ninayo majina na ushahidi wa wazi wa watu hao kutumia dawa waziwazi , maombi wala ubani havikuwasaidia chochote
 

Ndugu yangu, wewe ulimpangia Mungu kukuleta wewe hapa duniani? Mbona haya yalikuwa maamuzi yake? Na uliwahi kujiuliza kwa nini alikuleta? Kama ambavyo hukumpangia kukuleta hapa duniani,

Vivyo hivyo huwezi kumpangia muda wa kutekeleza jambo lolote linalohusiana na maisha ya binadamu, iwe dhiki, faraja, magonjwa, n.k. Usiongee kama hayawani ambao hawajuwi uwepo wao umetokana na nini. Mungu hajatusahau, tupo naye muda wote, tuombe na kusali bila kuchoka. Mungu akujalie roho wake, apate kukuongoza katika njia zake.
 
Kwanza ulitakiwa ufafaune hiyo nguvu chanya ina sifa za uwezo, wote, ujuzi wote na upendo wote au ni kinyume chake?

Kama hiyo nguvu chanya ni mungu basi pia ulitakiwa kufafanua hiyo nguvu hasi imetokana na nini, yaani nini chanzo cha hiyo nguvu hasi mpaka ikawepo?

Kama nguvu hasi (shetani) imeumbwa na mungu wako (nguvu chanya) mwenye utimilifu wa hizo sifa nilizozitaja hapo juu inatakiwa uthibitishe ni kivipi mungu mwenye uwezo wote aumbe kiumbe chenye uovu?



Imani ni nini?

Pili matendo mema unayapimaje?

Mfano mdogo waislamu kwao kuoa wake wanne kwao ni tendo jema, lakini ukija kwa wakristo jambo hilo sio jema.

Sasa ikatokea mtu amefanya jambo hilo utatumia dhana gani kuhalalisha au kubatilisha kua ni jema au sio jema?

Upi mzani sahihi kupima jema au lisilo jema?

Imani na Matendo yako yakiwa ni ya giza,huitaji tena kuubiriwa,NGUVU hasi itashuka tu na matokeo yake ndio yatakufungua ufahamu kwamba uligusa kwa imani na matendo sehemu inayovuta nguvu hasi.
Skiliza wewe

Hayo matendo ya giza kimsingi wa dini yenu siwezi nikayafanya bila kushawishiwa na huyo shetani. Infact ni kua kila jambo baya linapotendeka basi kwa namna yeyote ile shetani lazima ahusike.

Vile vile mungu akitaka mimi nisifanye hayo mambo ya giza anaweza kwasababu uwezo wote anao na sababu yakufanya hiyo anayo kwasababu yeye ni mwenye upendo wote.

Lakini hata hivyo ukiangalia hiyo kazi ya shetani kama ni kosa ambalo linamchukiza mungu basi tutahitimisha kwa kusema mungu ni mnafki. Kivipi? Kwasababu kabla hajamuumba shetani, huyu mungu kwa uwezo na ujuzi wake wote aliweza kujua impact itakayofanywa na huyi shetani siku za usoni. Inamaana mpaka anafikia hatua anamkamilisha kumuumba shetani, mungu alikwisha jua shetani atachoenda kukifanya.

Sasa huyu mungu kujilalamisha kwamba hapendi matendo anayoyafanya shetani huoni kwamba kunamfanya mungu aonekane mnafiki?

Haya tuseme kwamba ni kweli anachukizwa na uovu wa shetani, sasa anachukua uamuzi upi ku-fix hilo tatizo? Mbona uwezo wote anao kulikua na haja ya yeye hata ku-delay?

Kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote anaishia kunung'unika tu pasipo kufanya chochote kivipi ategemee sisi tumuepuke shetani?


Nguvu ya umeme uliotengenezwa na binadamu bado sio efficiently kwasababu malengo yao hayaendi kama wanavyotaka kwasababu hawana uwezo wote.

Aliyetengeneza umeme alikua hana uwezo wote wa kuufanya umeme usiweze kudhuru watu au miundombinu ya watu.

Huyu mungu ambaye anasifa ya "neno" yani akitamkacho ndicho kinachoenda kufanyika alikua na uwezo wa kusema "uovu usiwepo" na ikawa kweli uovu ukatokomea. Kwasababu kila kitu kipo chini yake


Corona na Magonjwa mengine ni matokeo ya imani na matendo hasi ya mwanadamu.

Na mataokeo hasi yamesababishwa na mungu kwa kosa alilolifanya kumuumba shetani ambaye anatushinikiza sisi kufanya uovu.

Utagundua baada ya nguvu hii kushuka,Matendo hasi yamezimwa kwa muda ingawa ni kwa kutumia sheria lakini pia watu wamejua kuna MUNGU.Juudi za kipindi kifupi za kuzima uhasi,zimeanza kuvuta Nguvu Chanya,amani na utulivu baadhi ya miji imeanza kurejea.
Hakuna muda sahihi wa mungu kudhihirisha ukuu wake kama kipindi hiki cha matatizo.

Hiki kipindi ndio kipindi ambacho mungu angeibuka warrior, lakini imekua tofauti yani kipindi hiki tumegundua ni namna gani hizi dini zimekua zikituongopea kuhusu mungu

Kwanini umtolee sadaka halafu kwenye matatizo kama haya akuache?

Mekka na vatican wanapiga hela za kuhiji lakini kipindi hiki wote wamefunga milango hawawataki muende.



Kwanini ubaya wa shetani alaimiwe shetani na sio mungu aliyemuumba shetani huku akijua kua atakuja kufanya ubaya?


Shetani kushindwa kufanya matakwa yake ni sawa kwasababu aliyemuumba hakumpa uwezo wote.

Sasa mungu muweza wa yote lakini bado ulimwengu umezagaa uovu inakuaje anashindwa kudhibiti haya mabaya?

Kazi ya wachungaji na Dini ni kukutadharisha usiguse nyaya za umeme .

Ndio maana wanatuhamasisha kuvaa mask

Watu wote wangejua kwa hakika kua huu ulimwengu sio makao yetu. Na kuna maisha baada ya hapa ambayo ni mazuri kuliko haya ya hapa, basi tusingeona maka na vatican wakipiga marufuku watu kwenda kwao kwa hofu ya kufa kwa corona


Vitabu vitakatifu wewe unajuaje kua vimesema ukweli?

It's Scars
 
Mungu haonekani kwa macho, "nyie wapaganinndio mnasema mara kamtokea fatima, mara yupo chanika, mara kamtokea sijui babu mtakatifu nani? yupo na alikuwepo na ataendelea kuwako
Sijasema nataka kumuona mungu kwa macho, makinika vizuri na contents zangu

It's Scars
 
 

Attachments

  • FCAA19B8-2628-4B92-B0FF-5AB820F2603E.jpeg
    70.8 KB · Views: 3
Masahihisho madogo : Mashehe na wachungaji walipata ukimwi wanachukua ARV bila kificho chochote , binafsi ninayo majina na ushahidi wa wazi wa watu hao kutumia dawa waziwazi , maombi wala ubani havikuwasaidia chochote
Hakika

It's Scars
 

Kwani mimi nimeletwa na mungu au juhudi za wazazi wangu?

Unanilazimisha niwakane wazazi wangu kisa mungu ambaye ni hadithi tu?

Inamaana wewe hujazaliwa na mama yako?



It's Scars
 
Kwani mimi nimeletwa na mungu au juhudi za wazazi wangu?

Unanilazimisha niwakane wazazi wangu kisa mungu ambaye ni hadithi tu?

Inamaana wewe hujazaliwa na mama yako?



It's Scars

Kwa maelezo haya uliyoandika, sitakuwa na msaada mwingine kwako zaidi ya kukuombea kwa Mungu.
 
Hali halisi inajionesha vp?
Hali halisi inajionesha kua hakuna ugonjwa ambao umefanikiwa kupata suluhu kwa njia ya maombi

Uwepo wa haya magonjwa yanayoua waumini mpaka viongozi wa dini ni ushahidi tosha kua mungu hayupo. Na dhana nzima ya dini ni uongo kama jinsi ambavyo kichwa cha mada kinavyosadifu


Huku kushindanisha dini na sayansi ni ujinga wenu lakini dini haifanyi kazi za sayansi mpaka tushindanishe,mbona hamsindanishi dini na tiba za asili au na mambo mengine?
Wapi nimeshindanisha dini na sayansi?


Wewe kalubati kua mwelewe shirikisha ubongo

Nimekuuliza hao wanasayansi ambao wanadini wanatumia njia gani kutafuta tiba dhidi ya magonjwa?

Hao wanasayansi Wanatumia maombi na kufunga ambavyo dini zimekua zikisisitiza tufanye pale ambapo tutapopata shida ?

Na ndiyo maana nakwambia hata huko kwenye sayansi wako watu wa dini,kwenye tiba tofauti tofauti wako watu wa dini kila sehemu watu wa dini wapo.
Wewe sidhani kama nacho kiandika unakisoma na kukielewa


It's Scars
 
Mmekaa,mnajaribu kusumbuka na mtu ambae yupo frustrated na kama walivyo wengi kajaribu kutafuta wa kumlaumu. Mungu halaumiwi na wala uwezo wake hauwezi chunguzwa.
Kuna kipindi alisema waache wapumbavu waendelee na upumbavu wao. Kuna kipindi wana wa Israel aliwaacha waendelee na njia zao. Na pale walipomrudia aliwaokoa.
Huyu anaemdihaki Mungu hapa jukwaani,wakati wake utafika pia. Atatambua ujinga wake na kumrudia Mungu. Siku akija soma haya anayoandika kwa upofu atajuta sana.
Mungu ni wa haki,hafanyi mambo kwa matakwa ya wanadamu.

Huyu Scar anahitaji kumuombea,upofu umtoke. kubishana nae kwa hali aliyonayo ni kupoteza muda!!
 
Kwa maelezo haya uliyoandika, sitakuwa na msaada mwingine kwako zaidi ya kukuombea kwa Mungu.
Maombi yako hayatakua na msaada wowote kama wenzako walivyogundua kua maombi hayana msaada wowote katika harakati za kuzuia corona, na njia pekee ya kuzia ni kupiga marufuku msiende kuhiji

It's Scars
 
Ujumbe murua kabisa mkuu..Mungu yupo atajibu tu..umeongea kwa hisia sana..Mungu akutue nguvu kipindi hili cha Kwaresima,nimehisi kitu fulani jipe Moyo yana.mwisho...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…