Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Matatizo yote huwa yanatatuliwa na sayansi au kwamba maradhi yote hutibiwa na hospitali ama tiba za kisayansi?

Mfano hawa watu wenye matatizo ya mapepo(ambayo wataalamu husema ni matatizo ya magonjwa ya akili) mbona tunaona hawa watu hupona haya maradhi kwa kuombewa dua pasina kupelekwa hospitali na wanapona.

Huo mfano ambao hauna tabu kila mtu anajua ila ukija huku mitaani utakuta kuna shuhuda za watu waliyotibiwa maradhi mbalimbali kwa kutumia dua.
 
nawashangaa sana hawa wanaojiita manabii, mitume na wachungaji kwa kuvuliwa nguo na COVID-19.

corona ndio ilitakiwa iwe kitu ya kuchukulia point tatu za kiubwete katika nyakati hizi.
Wanunue sanitaiza na mask,waweke malangoni,ntaweka ka.Msalaba tuuuuuuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maombi yako hayatakua na msaada wowote kama wenzako walivyogundua kua maombi hayana msaada wowote katika harakati za kuzuia corona, na njia pekee ya kuzia ni kupiga marufuku msiende kuhiji

It's Scars
Hata huko kuzuia watu kwenda kuhiji kutokana hali ilivyo ni mafundisho kutoka kwenye dini,ndio maana nakwambia wewe unataka kuifanya dini kama sijui kidubwasha gani vile cha kufikirika.
 

Mapepo ni nini?

Wenye matatizo ya ugonjwa wa akili mbona wako milembe kwanini hawakupelekwa misikitini au makanisani kama unachokisema wewe ni kweli?

It's Scars
 
Kwanza nakushukuru, huyo uliyemtaja hapo siyo yule tunaye Mwabudu.

Sisi tunayeMwabudu anaitwa Mungu ambaye ni Muweza wa Yote.

Huyo wako aitwaye mungu siyo Muweza wayote.

Kila Jambo, Kila ugonjwa Kila kitu Mungu wetu anakileta duniani kwa dhamira yake.

Jambo uliloliandika kwa ukweli ni lile ambalo "Mkiwa na imani " Basi haya unayoyaona ni mahangaiko ya kizazi chetu kwa kukosa Imani.

Mungu hatendi kazi zake Kama tunavyofikiria sisi. Tuko kwenye shida na dhiki kubwa Tumkimbilie yy naye atatuponya.

Majaribu haya yasikufanye ukakufuru, maonyo na maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya vyote hivyo ni ufahamu wa akili toka kwa Mungu siyo fahari yao.

Kudharau sauti ya serikali Mungu atakuadhibu na utalia ukisema amekuacha.

Virusi vimeumbwa na Mungu, tiba na tahadhali Mungu amewapa wanadamu.
 
Neno 'MUNGU' lilitoka wapi kwani...? 1;


Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ni neno lililotokana na lugha ya kiswahili nadhani lugha ya kiswahili unaielewa chimbuko lake

Lakini hata hivyo uwepo wa "neno" haimaanishi hicho kitu kipo kweli

Mfano tuna neno Spiderman, batman, Superman, unicorn, zombies, vampires ghost,nk

Uwepo wa hayo majina haimaanishi kua character wa hayo majina wapo kihalisia

It's Scars
 
Umeamua ukufuru tu ili ujithibitishie side yako... bon voyage "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Capital letter zisikuchanganye, shabaha yangu iko pale pale

Kwanza inabidi uelezee ni Mungu gani ambaye unamkusudia.

Sifa ya uwezo wote ni dhana inayotumiwa na kila dini kuelezea Mungu wao. Niambie wewe ni Mungu yupi ambaye unayemkusudia hapa?

Waislamu wana amini Allah ni muweza wa yote, wayahudi wakiwa na Mungu Yahwe, huku wakristo wakiwa na Mungu watatu mfululizo Mungu Mwana, Mungu Baba, na Mungu roho mtakatifu. Na dini zingine nyingi nazo zikiwa na Mungu wao

Sasa wewe umemkusudia Mungu gani hapo?



It's Scars
 
Mapepo ni nini?

Wenye matatizo ya ugonjwa wa akili mbona wako milembe kwanini hawakupelekwa misikitini au makanisani kama unachokisema wewe ni kweli?

It's Scars
Sio mie nayesema hivyo bali wataalamu wa magonjwa ya akili ndio huweka hayo matatizo ya majini/mapepo kwenye kundi la matatizo ya akili. Ndiyo nakwambia wenye matatizo hayo hatuoni kupelekwa hospitali ili kupata tiba ila tunaona wanatibiwa kwa dua na wanapona.
 
Hao madaktari wameumbwa na Mungu,,,
Je si ni vema kuwatumia hawa madaktari kuliko kusubiri muujiza?
Mungu ametupa akili ili tuzitumie ,,lakini bado unadoubt uwezo wake.
Look at the patterns of your body , akili yako ikuonyeshe kuwa zimedizainiwa.
Na Mungu akusamehe.[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Usipotoshe

Madaktari wamezaliwa kwa uchungu waliopata mama zao baada ya kubebwa miezi tisa na sio mungu

Kama mungu amekupa akili ya kuitumia kwanini unashindwa kuitumia kujibu maswali yangu hapo juu?

Mungu amekupa akili halafu huitumii ipasavyo kufanya reason za msingi katika mambo yamhusuyo yeye ili umuelewe vizuri. Huoni kwamba hayo ni matumizi mabaya ya akili?

It's Scars
 
Nimekuuliza swali

Kama kweli matatizo ya akili yanatibiwa kwa maombi kwanini mpaka muda huu tuna hospitali za watu wenye matatizo ya akili ambao wako chini ya uangalizi ya madaktari wakati inafahamika maombi ndio njia madhubuti ya kuponya watu hao?

It's Scars
 

 
Saudis already banned pilgrimage to mecca and Catholics have already banned use of holy water in their churches in Italy. Seems all eyes are on science for solution to corona virus, not on God

People slowly realizing that real problems can't be solved by imaginary solutions

It's Scars
 
Matatizo ya akili yapo ya aina nyingi hata wewe unaweza kuwa na matatizo ya akili bila kujua japokuwa unajiona mzima na unafanya shughuli zako kama kawaida,sasa mimi nimezungumzia matatizo ya majini/mapepo kama ambavyo wengi tunaamini hivyo ila wataalamu wa magonjwa ya akili wanatuambia hayo matatizo ni magonjwa tu ya akili hivyo ni kinyume na sie tunaoamini kuwa matatizo husababishwa na majini.

Ndiyo nasema hayo matatizo ya akili(majini/mapepo) tunaona hutibiwa kwa dua na watu hupona au kupata nafuu hapelekwi hospitali.

Kuna siku kwenye daladala binti mmoja alipatwa na hilo tatizo na kuanza kufanya fujo akanikosa ngumi ya uso,ikabidi wanaume tumshike kumzuia maana angeumiza watu na hata yeye pia angeweza kujiumiza na alikuwa na nguvu kwa hali ya kawaida asingekuwa na nguvu kiasi kile.

Hayo ndiyo matatizo nayozungumzia ambayo hayapelekwi milembe wala hospitali zetu hizi.
 
Unahitaji, uvuvio wa roho Mtakatifu kulijua fumbo la utatu Mtakatifu vinginevyo utaambulia hewa Kama ulivyo Sasa.

Nakupongeza Sasa kwa kuanza Kumtambua Mungu wa kweli.

Waislam, Wakristo na Wayahudi hawa wanamuabudi Mungu Mmoja Muweza wa Yote.

Ambaye hata ww unamuabudu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…