Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Pamoja yote uliyoandika, huwezi kuvunja watu moyo wa kuamini.

Inaonyesha hujui neno maombi maana yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli mkuu hii imekuwa kama danganya toto tuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Best comment so far,naendelea kusoma nyingine...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Mungu aliweka nidhamu katika ulimwengu sasa kwanini corona inasumbua watu halafu tunaona wachamungu wakijihami kwa maombi wakati huu ugonjwa ni sehemu ya matokeo yanayotokana na nidhamu ya ulimwengu aliyoiweka mungu?
 
Pamoja yote uliyoandika, huwezi kuvunja watu moyo wa kuamini.

Inaonyesha hujui neno maombi maana yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hakuna mahali nimeandika kua mvunjike moyo msiamini

Neno maombi muda wake sahihi wakujidhihirisha ilikua ni huu hatutaki maana ya maneno ambayo haisadifu vitendo
 
Ona sasa mwingine huyu

Yani matatizo yanayoua ndugu zetu ikiwemo wachungaji na mashehe ndio njia madhubuti ya kuonesha ukuu wa mungu?
 
Ukweli ni kwamba
Huijui DINI vile ambavyo inatakiwa uijue
Usijidai unaijua dini kuliko wenzako wanao hubiri huku wamevaa mask

Na wala usijidai unaijua dini kuliko wale waliokuzuia usiende kwao kama ulivyozoea siku zote kuwafata ili kupata elimu ya dini

It's Scars
 
Mungu aliweka principles na anafanya Kazi kwa principles.

Huwezi kuwa na njaa halafu unaomba muujiza ushibe bila kula.Lazima kifanyike kitu ili chakula kionekane

Vivyo hivyo kwa magonjwa.Mungu amekupa akili uitumie na siyo mahali unapoweza kutumia akili ya kawaida uombe muujiza.Chumba choo, kitumie vizuri ili usipate kipindupindu.Sasa wewe unaenda kujichamba bila kunawa halafu unashika vyombo vya ndani ukiugua kipindu pindu unamlaumu nani?

Mwisho Mungu usimchukulie poa ndugu yangu unless wewe ni devil worshiper.Kama we ni mtu wa kawaida tu,ujue devil mwenyewe anamwogopa na kutetemeka.Anaweza kukushughulikia tu ili ajipendekeze kwa tabia yako ya kumdharau Mungu.

Tubu na nyenyekea kwa Mungu na acha kuangalia udhaifu wa watu wengine jiangalie wewe mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya sasa ndiyo madhara ya kuchanganya DINI, SIASA, UTAPELI, SAYANSI, HALF-KNOWLDGE na PREJUDICE.

Katika ukristu, sote tunajua kuna matepeli wengi, wanaotumia jina la Yesu kuishi mjini, kuwafanya wengine mazoba ili wao wapige dili, na hawa wameuumiza ukristu kwa sehem kubwa. Wanapaswa kulaumiwa sababu hawamuhubiri Yesu wa msalaba ila Yesu wa Harusini kana, wao ukristu ni kupata utajari, kupona magonjwa yote, kuishi kama uko peponi ilihali uko duniani.

Jibu rahisi tu ni kwamba hata Yesu mwenyewe, hakuponya wagonjwa wote aliokutana nao, aliponya wale tu ambao uponyaji wao unahusika moja kwa moja na lengo lake kuja duniani, ambalo ni kuokoa roho (na mwili akitaka Yesu, ila sio kwa kuamrishwa na mwanadamu)

Lengo la Yesu na Ukristu, sio kumfanya mwanadamu astarehe duniani, bali mwanadamu atambue maisha ya duniani kama matayarisho ya maisha ya umilele, hili ndilo lililomleta Yesu duniani, na ndiyo kwa mfano kanisa katoliki linafundisha.

Unadhani kwa nini wamisionari walikuja na dini mkono wa kulia na shule/hospitali mkono wa kushoto? je kuna wamisonari wa kikatoliki walikuja na kusema acheni hospitali njooni tuwaombee mpone?

Mungu anasikia kilio chetu na anaweza kutuponya kwa muujiza Corona endapo akitaka, sisi tunafunga na kusali kumuonesha haja na hitaji letu, japo analijua lakini ameshasema OMBENI NANYI MTAPEWA, BISHENI NANYI MTAFUNGULIWA....hakusema simama mlangoni, nitafungua kwa kuwa ninajua unataka kuingia!!!!

Tutumie utashi wetu wa kibinadamu, ambao ni zawadi ya Mungu, kukwepa corona, na tumuombe Mungu atuepushe na Corona kwa namna zile ambazo ziko nje ya uwezo wetu kama wanadamu, ila tusatake kumfanya Mungu shemeji yetu kuwa aje sasa aponeshe Corona ndo awe Mungu kweli.

Nawaambia hivi, hata Mungu akishuka leo hii akaponesha Corona dunia nzima, hamtamwamini, sababu Corona sio kipimo cha uwezo na mamlaka ya Mungu, Mungu hapimwi kwa uwezo wake wa kuponya Corona
 
Una hoja dhaifu sana.mbona yashawahi kupita magonjwa makubwa corona cha mtoto.watu walikufa na dawa ikapatikana,maisha yakaendelea..corona ni ugonjwa kama magonjwa mengine..sioni sababu yakukashifu dini.
corona ipo na itaondoka itabaki story.corona iuwe iwezavyo haiwezi fikia maleria na ambayo dawa zake zipo zakila aina na zinajulikana na inauwa kila siku.mbona hamzisemi dini?.corona ni gonjwa la mlipuko limekuja litaondoka maisha yataendelea.
 

Kama hili linajulikana kiujumla inamaana unataka kutuaminisha kua watu wadini ni wanafki?

Kama mungu yeye ndio ameamua watu wafe kwa korona na jambo hilo linatambulika kidini kwanini watu wadini wanafanya maombi ili wasalimike?


Halafu kama point ya mungu ni kuwadhuru watu kwa corona kwanini vatican na mekka wakataze watu wasiende kuhiji makwao kwa kuogopa kudhurika na ugonjwa?

Huoni kwa kuwazuia watu wasiende huko maana yake ni kuzuia watu wasidhurike jambo ambalo wanakua wanaenda kinyume na matakwa ya mungu?

Unaelewa kwa mujibu wako hao waliozuia nyinyi msiende huko wamefanya dhambi maana wanawanyima haki ya kusambaza ugonjwa ili watu wadhurike kama alivyokusudia mungu wenu??



It's Scars
 
Hso waebrania ulio wanukuu unahakika gani kama wamesema ukweli?

Unafikiri mapadre huko vatican hawajaona kua kuna nukuu za waebrania mpaka wameamua kupiga marufuku msiende?
Inafurahisha mtu ambaye humwamin Mungu kutaka kuhakikishiwa kama yupo .hicho ni kituko kwa sababu step ya kwanza unatakiwa umwamin Mungu yupo nje ya hapo huwez kumwamin wala kumwelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sahihi "ajabu" sio "hajabu" .

Sikujui kweli ila najadili ujinga wako juu ya jambo hili, kwa vile umeudhihirisha.
Kutokua sahihi wakati nikizungumzia mungu ambaye si sahihi ni sahihi pia

Hunijui ila umeweza kunijadili, hivyo umeonesha ujinga wako wa awali kua sio lazima kitu ukijue ndipo uweze kukijadili. Sasa ulipokua unasema simjui mungu ajabu namjadili nadhani umejiona ujinga wako ulipo

It's Scars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…