Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani dini imemzuia muafrika asifanye maendeleo? Mbona haya malalamiko tunayo sisi tu waafrika na wakati hizi dini zimeenea sehemu nyingi tu duniani lakini hatuoni wakilalamika hivi?Hizi biashara za dini inajulikana wazi kabisa kwamba zilikujaje hapa africa. Siku tukijikomboa kutoka kwenye janga la utumwa wa dini nadhani africa inaweza kuja kupiga hatua kubwa sana hapa duniani katika kila nyanja ili kutengeneza future nzuri kwa kizazi kijacho.
Ndio ujue HAKUNA MUNGU hapo! Ni fix tu za kale tulizolishwa na mapadri.
Asante sana...kama ulikuwa kichwani mwangu!Wewe jamaa bhana!!?
Unavyo mchukulia MUNGU ndivyo naye atakavyo kuchukulia ukimchukulia kwa uzito na yeye atakuchukulia kwa uzito ukimchukulia kikawaida basi ivyoivyo atakuchukulia wewe
Nauhakika na hili
[emoji91][emoji91][emoji91]Dunia yote imesalander! Hakuna mwenye nguvu, hakuna mwenye utaalamu, hakuna tajiri, hakuna teknolojia, hakuna silaha kali, hakuna usalama wa taifa, hakuna hakuna hakuna chochote. Kila nchi inalilia hali yake. Kila nchi inafunga mipaka yake, haijulikani tena nani anamfungia nani. Hakuna nchi inayohurumia nchi nyengine, kila moja inapambana kivyake... yote yamesababishwa na kidudu kidogo-virus.. wala hakionekani kwa macho!!!! Unahitaji nini kukubali kuwa Mungu yupo? ambaye akitaka lake hakuna nguvu yeyote inayoweza kulizuia?!!
Ameleta corona akitaka ataiondoa hakutaka ataiacha iendelee kutia adabu watu. Hapangiwi ampe nani na nani ni maamuzi yake tu!!! Watu wa dini yeye ndo anawajua zaidi kuliko wewe kama ni wa kweli au waongo! Sisi tunaomuamini uwepo wake na nguvu zake tunamuomba atunusuru na hili lkn hatuna haki ya kumlazimisha. Tunaomba, anaweza akatukubalia au akatukatalia! Hakuna mwenye guarantee ya maamuzi ya Mungu!
Swali langu lijibiwe then ntajibu lenuWakati wewe unataka kujua Mungu yupi ni wa wakweli kuna wengine wanataka kujua kama huyo Mungu kweli yupo?
Wewe unaweza kujibu hilo swali kuwa kweli Mungu yupo?
Jana nimesikia Mch.mmoja akisisitiza watu watoto wasitoke nje kwa kutumia mfano wa Wanaisrael walivoelekezwa wasitoke nje huko Misri.
Kwanza hayo maandishi ya biblia unahakika gani kwamba yamezungumza ukweli?Kwa hiyo ukimwi, kansa, ebola, presha etc yalikuja ili kuthibitisha MUNGU hayupo? Utasema vilema viwete vipofu kn wapo kwasababu Mungu /nguvu ya maombi imeshindwa?......
Kina ayubu walipigwa magonjwa mazito pamoja na kuwa alikua mcha Mungu sana lkn yote ili idhihirike kua Mungu yupo.....
ndugu acha kukufulu haya yote yapo ili wanadamu mkumbuke ukuu wa Mungu.....
Mswali mepesi sana. Sijakna hoja inayohitaji majibu ya kufikirisha kwa sababu vyote ulivyondika ni lugha za kawaida za wapofu wa imani. Jifunze kwanza imani ni nini na inatendaje kazi ndipo uje na hoja za kueleweka. Pole sana mkuuPoleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya