The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 21,281
- 49,313
Maneno peke yake hayatasaidia. Kuna vitu ambayo serikali inatakiwa kufanya mpaka sasa haijafanya. Mfano moja ni kuendeleza kuruhusu mikusanyiko isikuwa ya lazima.
Nipo pamoja na wewe na nnakuelewa sana unachokisema. Nilikua najibu hoja kwamba Rais hatambui uwepo wa hili janga.
Tukirudi kwenye hoja yako ya msingi, hili ni jambo pana linalohitaji umakini na uangalifu wa kina kabla ya kufanya maamuzi kwa vile linaathiri maisha ya kila mmoja wetu. Lakini pia ikumbukwe hakuna njia moja au namna ambayo imeonekana kuwa bora zaidi na ikafaa kwa nchi zote.
Naamini serikali kwa kupitia taratibu zake watakuja na maelezo zaidi kama ulivyopendekeza.
Lakini cha muhimu kwa sasa ni kila mmoja wetu kuchukua tahadhari na kuzingatia kanuni zinazoepusha au kupunguza maambukizi.
Sijasikia raia amewekwa ndani kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono, kujiepusha na mikusanyiko isiyona ulazima au kutumia vitakasa mikono.