Corona: Meneja wa Diamond na Mwana FA watangaza kuugua Corona baada ya kupimwa

Upo sahihi kabisa mkuu. Mbona hasemi mtu akijitangaza kua ameathirika na UKIMWI nae achukuliwe hatua?

Hayo matangazo ni muhimu kwa sababu yanasaidia ku rise awareness na pia kuondoa unyanyepa kwa walioathirika
 
Tunzo, Nadhani si jambo baya kama wamepimwa na kuthibitika kweli wana virusi vya korona, kwasababu kuna taharuki kubwa sana mijini na vijijini kuhusu huu ugonjwa. Watu wanafikia hatua ya kutimka mbio wakisikia fulani anahisiwa kuwa na ugonjwa wa korona, mfano jana katika Star tv habari wananchi huko Musoma walitimua mbio walipopata taarifa za uwepo wa mtu mwenye ugonjwa huo hadi madaktari walikimbia yote hii ni taharuki ya kutokua ta taarifa sahihi za ugonjwa huo.

Hivyo basi hao wanaoposti wanaweza kusaidia kupunguza taharuki iliyopo nchini kwa sasa, ikapelekea watu kujua kuwa ni ugonjwa kama magojwa mengine. Juzi huko huko Mara wilaya ya Rorya kijiji cha Kirongwe kulitokea msiba, wale wafiwa walikamatwa na kuwekwa ndani na mkuu wa Wilaya kisa walikusanyika makaburini kwenye maziko.

Sasa kama hao wafiwa wangekuwa na maambukizi si wangemuambukiza yeye (DC) na askari wake pamoja na mahabusu pale selo ya Shirati?

Elimu inahitajika, na hao wagonjwa wanaojiposti kwa maoni yangu wapo sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi utasikia amber rutty na Mwijaku nao wanatangaza Wana Corona
Ugonjwa wa kutafuta kick ni mbaya kuliko Corona
Hahahaaaaaaaa a.mpwaaa.pataaaaaaaa kvant billyakoo nakujakulipaa
 
MI NASUBIRIA TAR 1 APR
NA MM NAPATA CORONA LIVE
 
Je, wewe ukisikia msanii fulani ana corona unapata taharuki?
 
Katika video yake aliyojirekodi anasema baada ya kuhisi joto lisilo la kawaida alienda kupima akakutwa na korona lakini maajabu baada ya kupimwa video inaonyesha yupo kwenye chumba cha hoteli

Kwanini yupo hotelini na sio mloganzila sehem iliyotengwa kwa wagonjwa wa corona, yupo serious kweli au anatutania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awe anaumwa au haumwi tatizo litakuwa ni kwa wenye dhamana ya afya zetu na vyombo vya dola. Kama kweli anaumwa wenye dhamana ya afya wangehakikisha anapelekwa sehemu salama ambapo ni Mloganzila Hospital kwa manufaa yake binafsi na raia wengine ambao hawajaugua ugonjwa huo.

Na kama alidanganya wawili hao niliowataja walitakiwa kumchukulia hatua za kisheria kwa kujitangaza kwamba anaumwa kumbe ni ulaghai wa kutafutia au kujiongezea umaarufu.
 
Watalii sasa wataziogopa Hotel zetu.......alianza Mwambapa na sasa mwanafa!
 
Kuna Kikundi cha watu wakubwa kwa kutojua wanajaribu kuitengeneza Jamii ione huu ugonjwa ni wa kawaida ili shughuli za Uchumi zisisimame

Ni sawa na kile kituko cha BOT kutangaza kuwa sarafu yetu inaji sanitize automatic

Hii si sawa na ni hatare sana

Tunisia walifanya Mzaha tunaoufanya, sasa hivi sio tu kufunga mipaka ya nchi, bali hata Anga limefungwa rasmi kwa kudhania hata ndege zikipita zitawaletea Corona, the same to Italy walichukulia poa

Huu ugonjwa ni hatare sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…