China imeua watu wengi Sana wenye korona hao wote hawajajumuishwa kwenye idadi wazungu wanathaminiana mno kwao safety ni first priority , taarifa zao zinaweza zikawa accurate , si rahsi kumuua mwenzao , Ila China na Irani wagonjwa wengi Sana wamepigwa mass grave , korona haina impact Africa mana ni magonjwa ya kawaida Sana Kwa ngozi nyeusi , watu weupe mafua kwao ni critical disease
Watu wa magharibi hasa wamarekani wamefanikiwa sana kuaminisha watu wengi kwamba wachina hawathamini maisha ya binadamu, wanasema uongo daima, na vitu kama hivyo.
Unaweza kujiuliza China kuna vikundi kama vya KKK wale white supremacy ambao hata sasa wanauwa wenzao sababu za kibaguzi?
Inaingia akilini mtu (A) ambae ana aminika hathamini maisha ya binadamu anahukumu mtu aliye tengeneza maziwa ya watoto yenye sumu?
Inaingi akilini kusema mtu(B) ana thamini maisha ya watu lakini mtu huyo anavamia nchi flani na kuuwa mamia kwa maelfu ya watu akisingizia kiongozi wao ana silaha za maangamizi za kibaolojia ambazo baadae wanakiri hazikuwa taarifa za kweli?
Utasemaje
Unaweza kusema mtu B ni msema ukweli hawezi kutoa taarifa za uongo kama anaongopa jambo kubwa ili mradi uongo wake umpe uhalali wa kuvamia nchi flani na kuuwa maelfu ya watu kwa sababu zake za manufaa ya kiuchumi?
Jambo kubwa lililo wazi ni kuwa watu wagonjwa wa COVID-19 waliozidiwa iasi cha kufa hawafichiki hivyo lazima waonekane tu wanakufa ovyo.
Mawazo kama yako yananikumbusha kisa cha hayati Field Marshal Fidel Castro alipotembelea Marekani kuhudhuria mkutano wa UN akafanyiwa fitina na kukosa mahali pa kujihifadhi yeye na msafara wake akapokelewa na watu weusi wakazi wa Harlem City chini ya uratibu wa mwenyeji wake Hayati Malcom-X.
Jinsi alivyopokewa na umati mkubwa tena kwa shangwe akasema huku akistaajabu "ninyi ndio marafiki wa kweli, mpo ndani ya Amerika lakini hamkuamini propaganda za kuonesha Castro ni mtu mbaya na adui ili hali mpo ndani ya Amerika ambako media zote zinarusha uzushi (propaganda) kuhusu Castro na Cuba!"
Baada ya ziara hiyo Malcom X ktk moja ya mazungumzo yake na wanahabari akasema "Fidel Castro ndio kati ya mtu mweupe pekee ninaye weza kumuamini".
Jiulize kwanini mtu aliye ishi na kukua pamoja na wazungu hawaamini hata kidogo na wewe uliye zaliwa Afrika unawaamini sana kuliko weusi wenzio au watu wa bara la Asia (wachina) kwamba wazungu ni watu wakweli. Huoni kwamba hawa ni wanafiki wazuri wanaoweza kuficha ubaya wao na kuwatangaza wengine kwa mabaya?