Corona: Meneja wa Diamond na Mwana FA watangaza kuugua Corona baada ya kupimwa

Corona: Meneja wa Diamond na Mwana FA watangaza kuugua Corona baada ya kupimwa

Hii kitu inazua sintofahamu sana kwa kweli. Wanapitaje pale Airport?
La ajabu hawa wote wametoka nje ya nchi na kwenda kupima wenyewe..
Hakuna aliezuiwa airport na kupimwa..
Wagonjwa wote wanaingia tu
 
kuna kitu hakiendi mbna wanajitangaza wenyewe, ndo mfumo ulivyo kwa sasa, kila mtu anajifanyia vipimo vyake na kujitangazia anaumwa, tutafika kwa style hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kwamba wamejipima wenyewe mtaani na kujitangaza.
Wamepimwa hospital kama wengine, kwa taratibu na sheria serikali haiwezi kutangaza majina ya mgonjwa na ugonjwa wake.

Kinachotokea wagonjwa wenyewe ndio huchukua hatua kujitangaza kwa kufichua hali za afya zao.
Serikali inatoa taarifa bila kutoa utambulisho wa wagonjwa. Hao wagonjwa wawili wapya waliotangazwa na serikali leo ndio Sallam (toka Ubelgiji, Ufaransa na nchi nyingine ya Ulaya) na Mwana FA(toka Afrika Kusini).

Mnakuza mambo na kujitisha au kuwatisha watu bila sababu za msingi.
Acheni serikali ifanye kazi punguzeni woga utasababisha vifo vya woga na gharama za maisha kuwa kubwa sana.
 
Huu ugonjwa ulikuwepo toka last year Dec na wizara husika haikujua ni ugonjwa gani zaidi ya kusema tuu kwamba ni homa kali na itaisha. Nadhani kuna mchina aliupeleka huko Wuhan
Inawezkana kweli last December niliumwa homa Kali sana na mafua nikapima vipimo vyote hola!! Nikanywa Panadol tu vikapotea

Hadi leo sijagusa dawa yeyote

Usikute huu ugonjwa uliukuwepo hapo muda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Practically hilo litakua gumu mkuu, kama vipi wafute safari zote za ndege na kufunga mipaka ili wageni wasiingie kabisa Tanzania.

Itawezekana vipi kwa mfano wageni zaidi ya mia kwa uchache kabisa wanaingia nchini kupitia viwanja vya ndege au mipaka ya barabara na bahari uwazuie uwaweke mahali kwa siku 14! Hata nchi zilizoendelea haziwezi kufanya hivyo
Shida ni kwamba serikali yetu imeonyesha wazi kuwa hatuwezi kuzuia wageni kuingia Tanzania, kwa muda mfupi (sijajua kwa nini inawezekana uchumi ukayumba sana) ndio maana kama wageni ni muhimu sana basi tuwahifadhi kwenye uangalizi sehemu moja kabla ya kuwaruhusu kujichanganya na watu wengine. Hizi ni hatua nchi za Afrika zilizochukua kudhibiti ugonjwa huu.
IMG_20200319_190203.png
 
Juzi nilisema lazima kuna kitu katika hili sakata la corona
Maana ukiangalia data za wagonjwa duniani na wanaokufa hutapata mwafaka.
Kuna kasiri ndani ya corona .

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba kuuliza hao watu sita(6) wote walijitangaza kabla ya kutangaza serikali kuhusu kuuguwa kwao?
Au kwasababu serikali haikuwataja kwa majina?
Hao watu wanakipimo wenyewe tofauti na cha serikali kilichopo maabara ya MNH?

Acheni kuwatisha watu na hisia na habari za uzushi.
 
Walichobakiza ni kuisifia serikali ya awamu ya 5 kwa kukabiliana na corona ndio breaking news zinazofuatia
 
Huu ndio ukweli haswa,nov-dec kulikuwepo na hali ya ajabu sana haswa dar na Arusha watu wamelazwa sana na homa haijulikani ni nini malaria si malaria wala dengue.
Mi pia nna wasiwasi na huu ugonjwa kuwa ulikuwepo coz mwezi ulopita katikati niliandamwa na kikohozi na mafua ambayo yalinisababishia homa mpaka kwenda kupima bt as you know hospital zetu ni mwendo wa malaria ukizingatia kichwa kilikuwa kinaniuma ndo kabisa.

Nilipewa dozi ya pilton na syrup kwa ajili ya kikohoz lakin wapi na mbaya zaidi wife na mtoto pia walikuwa attacked mpaka nilpokutana na mmama mmoja kitaa akanambia nichemshe malimao plus tangawizi na asali. Hali kama hii nlikuwa sijawai kuipitia mpaka nlihisi nmelogwa coz nlidum nayo takriban mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natazama CNN sasa hivi Rais,mganga mkuu,sijui FDA chief wote wanaongea jinsi gani wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha hili janga linaisha! Huku Tz kila siku watu wanaonesha jinsi huu ugonjwa ulivyo 'mwepesi'. Hizi sifa na kujimwambafai za nini? Tusije kulia baadae wakati wenzetu wametulia wanafanya shughuli zao.

Hawa USA na Europe walimwona Mchina kilaza sasa hivi wao ndio wanahangaika. Tuombe Mungu atuepushe
 
Ms Rose Marie Compaore, who was the first-vice president of the parliament of Burkina Faso

Burkina Faso's records first COVID-19 death in sub-Saharan Africa | Africanews
The authorities say the patient was a diabetic woman aged 62 years. Some reports on social media say it is a top lawmaker, Ms Rose Marie Compaore, who was the first-vice president of the parliament.

Mama alikuwa mgonjwa wa kisukari kwahiyo si unajua sukari haipendi stress, stree ya woga wa korona, hyperglycemia then kifo kwahiyo mama kafa kwa sukari!
 
Ndebile,
That's the whole point about this virus. It is more dangerous for those with pre-existing conditions. The advantage that Africa has over other continents is that we have the youngest population in the world. It's more likely the young and fit can wear it off without the highest risks.

But what about the older generation and those with existing health complications, do we put them at risk because they are the minority? Kingine, mtu bado anaweza kuusambaza tena kwa kasi tu akiwa anaonekana ana afya yake, which is different from most other viruses and bacteria.

Ni kweli hatutakiwi kupanic, lakini bado tusipuuzie how dangerous it can be.
 
Back
Top Bottom