Kutisha au kutishwa maana yake nini?
Unatishwa vipi na taarifa za ukweli ewe mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kwenye red si wajibu wako?
View attachment 1717458
Ukweli haujawahi kutisha. Sana sana ukweli ni mchungu. Ukweli huuma na msema kweli ni mpenzi wa Mungu!
Au nasema uongo ndugu zangu?
1. Sio kweli kwamba takwimu za vifo vya Corona zingetolewa watu wasingekufa kwa ugonjwa huo. Marekani na nchi zingine zilizoendelea wanatangaza kila siku na vifo vinaongozeka. Takwimu zinahitajiwa na Wanasayansi kwa ajili ya utafiti na kuchukua hatua zinazopaswa. Kutangaziana vifo hakumsaidii mwananchi wa kawaida, bali kunamuongezea hofu ambayo inapelekea matatizo mengine. Hakuna ushahidi kwamba huko wanakotangaza vifo kila siku, hilo limesaidia wananchi kuongeza umakini katika kujikinga na Corona. Ila kuna ushahidi wa ongezeko la matatizo ya afya ya akili (mental health) na mengineyo yanayoendana na hofu, wasiwasi n.k.
2. Hakuna ushahidi kwamba hadi leo sisi tuna vifo vingi saaaana vinavyotokana na COVID-19, kuliko zinatangaza takwimu za vifo kila siku. Ila kuna ushahidi kwamba bara la Afrika halijaathiriwa sana na Corona kama ilivyo kwa mabara mengine. Hadi sasa vifo vilivyoripotiwa Afrika nzima si zaidi ya 120,000 ukilinganisha na ukilinganisha na karibu vifo 2,600,000 ulimwenguni. Kumbuka sio rahisi kuficha vifo kwa Waafrika kwa sababu kifo ni tukio muhimu la kijamii.
3. Hakuna nchi yoyote Afrika yenye uwezo wa kudhibiti kikamilifu maambukizi ya Corona. Ugonjwa huu ni mafua makali ambayo yanaambukiza kwa urahisi mno, kiasi kwamba hata wale ambao 'hygiene' yao iko vizuri sana bado wanapata maambukizi. Takwimu za maambukizi hapa Afrika sio sahihi, kuna uwezekano zaidi ya asilimia 70 ya watu walishaambukizwa na kupona. Aidha kuna uwezekano nchi nyingi za Afrika zinapika takwimu kwa sababu za kisiasa.
4. Je, tusichukue hatua zozote kujikinga? Hapana! Tuchukue hatua zinazowezekana kama kunawa, kukaa mbali na wengine ikiwezekana, kuvaa barakoa n.k, naamini zinapunguza kwa kiasi. Lakini tusiilaumu sana serikali maana haina uwezo wa kudhibiti maambukizi wala vifo vinavyotokana na COVID-19 hata kama ingependa kufanya hivyo. Kwenye janga hili, Tanzania na Afrika kwa ujumla inapona kwa neema ya Mungu tu. Hatuna uwezo wa kupambana COVID-19 hata kwa asilimia 1 ya ufanisi.
kwanini umezinguana naye?Nadhani sirikali inataka tufike huku!
Leo mtaani kwangu Kuna misiba mitano,yaani mpaka nmezinguana na shemeji yenu!
alikuwa mtu mzima?Hapa nipo kwenye msiba wa rafiki yetu baada ya kufariki kwa changamoto ya upumuaji na kesho mida ya saa saba marehemu anatarajiwa kusafirishwakuelekea Mbeya kwa maziko. Nashukuru wahudhuriaji wamechukua tahadhali zote za kujikinga na Corona kwa kuvaa barakoa na kukaa mbalimbali kila sehemu kukiwa na ndoo za maji tiririka.
Mungu aliepushe taifa letu katika hii kadhia ambayo viongozi wetu baada ya kusa wafariji wakuu wamegeuka kuwa wauwaji. Narudia tena kusma kula wamegeuka kula wauaji
Alikuwa na umri wa miaka 58 na bado alikuwa na nguvu zake tu.alikuwa mtu mzima?
nadhani korona ipo zaidi huko DSM, mikoani hakuna misiba mingi Kama inavyosemwa
Umejichanganya vilivyo kwenye bandiko lako. Haieleweki kwa nini ukweli ulete hofu badala ya kuwa ukweli utaleta umakini zaidi.
1. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuwadanganya watu kuwa ugonjwa haupo wakati upo haiwasaidii kujikinga nao. Bali ni wazi kuwa uwepo wa taarifa sahihi kunasaidia watu kuchukua tahadhari zaidi.
2. Ushahidi wa kiwango cha vifo kwetu unataka uupate vipi wakati kwa makusudi taarifa zinafichwa? Wewe hujasikia ugonjwa huu ukibatizwa majina tokea changamoto za kupumua, pneumonia, kujisikia vibaya, mafua, kubana mbavu, ajali nk?
3. Hakuna nchi Afrika yenye uwezo wa kuudhibiti ugonjwa huu? Hii si kweli. Kwenye red kuna husika:
View attachment 1717812
4. Hatua tunazochukua ni zile tu tunazo ziweza, una maana ni kama hizi za latra za kukaa mita moja stendi na kushonana kama magunia kwenye madala dala na ma ferry?
View attachment 1717813
Kwanini msimamo huu ni muafaka sana kwenu?
View attachment 1717815
Si mseme tu kuwa mmetutelekezea janga na mnaukimbia wajibu wenu. Kuwa wenye kufa shauri yetu na wenye kuishi shauri yao?
Kama yamewashinda si mpishe wengine waongoze vita hivi? Kwa nini kutusakizia na kututelekezea vifo vinavyoweza kuepukika?
Nilipoona tu mambo kuibiwa kura, nikajua post nzima ina jicho la kisiasa. Kwa mkao huo huwezi kuona mambo kwa mtazamo tofauti.
Tuchukue Tahadhari!
Analala msiban mkuu,najikuta Kuna vitu navikosa!kwanini umezinguana naye?
Sasa unangojea nini kujikinga? Huu ugonjwa ulo kila mamhali. Chukua tahadhari. Sasa inmlalamikia nani? Magufuli ndiy aliyeleta huu ugonjwa?Mapadri, watawa, kina Maalim, madaktari bingwa kadhaa, nk. Wote wameshindwa kuchukua tahadhari?
View attachment 1717837
Hapa kwenye red bila utayari wa serikali tunapenya vipi?
View attachment 1717838
Mchawi wetu yuko humo.
Au nasema uongo ndugu zangu?
Sasa unangojea nini kujikinga? Huu ugonjwa ulo kila mamhali. Chukua tahadhari. Sasa inmlalamikia nani? Magufuli ndiy aliyeleta huu ugonjwa?