Umejichanganya vilivyo kwenye bandiko lako. Haieleweki kwa nini ukweli ulete hofu badala ya kuwa ukweli utaleta umakini zaidi.
1. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuwadanganya watu kuwa ugonjwa haupo wakati upo haiwasaidii kujikinga nao. Bali ni wazi kuwa uwepo wa taarifa sahihi kunasaidia watu kuchukua tahadhari zaidi.
2. Ushahidi wa kiwango cha vifo kwetu unataka uupate vipi wakati kwa makusudi taarifa zinafichwa? Wewe hujasikia ugonjwa huu ukibatizwa majina tokea changamoto za kupumua, pneumonia, kujisikia vibaya, mafua, kubana mbavu, ajali nk?
3. Hakuna nchi Afrika yenye uwezo wa kuudhibiti ugonjwa huu? Hii si kweli. Kwenye red kuna husika:
View attachment 1717812
4. Hatua tunazochukua ni zile tu tunazo ziweza, una maana ni kama hizi za latra za kukaa mita moja stendi na kushonana kama magunia kwenye madala dala na ma ferry?
View attachment 1717813
Kwanini msimamo huu ni muafaka sana kwenu?
View attachment 1717815
Si mseme tu kuwa mmetutelekezea janga na mnaukimbia wajibu wenu. Kuwa wenye kufa shauri yetu na wenye kuishi shauri yao?
Kama yamewashinda si mpishe wengine waongoze vita hivi? Kwa nini kutusakizia na kututelekezea vifo vinavyoweza kuepukika?