Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Alikuwa na akili Sana,Ina maana hakuenda kwake,badala yake akajufungia hotelini kusikilizia dalili,alipoona Hali Tata akajisalimisha hospital
Kwanini hakupima huko huko? Na alijua ameishi na mtu mwenye corona!
 
Wamevumilia na kujitahidi kuficha ila wameshindwa kuficha zaidi.
OMBI NA USHAURI WANGU KWA MAMLAKA HUSIKA, WASIWACHANGANYE WATU/WAGONJWA WANAOHISIWA PAMOJA KWANI KUNA WENGINE AMBAO WANAUMWA MAGONJWA YA KAWAIDA,

SASA WATAKAPOWACHANGAJI, WAGONJWA, YULE MWENYE CORONA ATAWAAMBUKIZA HAO WENGINE, HIVYO WAJITAHIDI KUWATENGA KWA KADRI ITAKAVYO WEZEKENA.
 
Mnamo tarehe Machi,15, msafiri huyo aliiingia Tanzania majira ya saa kumi jioni.

Mgonjwa aliyetangazwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, ambaye aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda.

Msafiri huyo aliondoka nchini tarehe 3,Machi 2020 ambapo kati ya tarehe 5-13 Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji.

Msafiri huyo alipita uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Waziri Ummy Mwalimu amesema msafiri huyo alipofika KIA alifanyiwa ukaguzi na maafisa wa afya na kuonekana kutokuwa na homa.

Baadae alianza kujisikia vibaya akiwa hotelini na kwenda hospitali ya mkoa ya rufaa ya Mount Meru Arusha ambapo sampuli ilichukuliwa na kupelekwa maabara ya taifa ya afya ya jamii iliyoko Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi.

"Vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyo ana maambukizi ya ugonjwa wa corona, covid -19, Mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu."

Waziri Ummy ameongeza kusema," Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kwamba ugonjwa huu unathibitiwa ili usisambae nchini.
 
Wamevumilia na kujitahidi kuficha ila wameshindwa kuficha zaidi.
OMBI NA USHAURI WANGU KWA MAMLAKA HUSIKA, WASIWACHANGANYE WATU/WAGONJWA WANAOHISIWA PAMOJA KWANI KUNA WENGINE AMBAO WANAUMWA MAGONJWA YA KAWAIDA, SASA WATAKAPOWACHANGAJI, WAGONJWA, YULE MWENYE CORONA ATAWAAMBUKIZA HAO WENGINE, HIVYO WAJITAHIDI KUWATENGA KWA KADRI ITAKAVYO WEZEKENA.
Na bila yule mama wa WHO asingetangaza huyu waziri wenu
 
Mkuu embufikiria hii, mgonjwa kapimwa KIA kaonekana hana maambukizi kabisa ni mzima wa afya lakini yeye mwenyewe anajihisi kbs mgonjwahayiposawa ndiomaana akaamua kwenda Hotelini kujiweka kizuizini kwa hiyari yake, baadae anaamua kwenda hospitali na anagundulika ana maambukizi.

Hii ndio serikali ya awamu ya tano, nguvu kubwa kuwavunja vunja mikono wapinzani lakini kumtambua mgonjwa wa corona uwanja wa ndege hawana ila mgonjwa mwenyewe anajitambua ni mgonjwa. Hakimu Mfawidhi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namna CCM na policcm wanavyojitahidi kupambana na Chadema sasa ni wakati mwingine wakupambana na covid-19

Natumaini mtaivunjilia mbali hiyo covida hata kwa risasi inayokata kona
 
Na bila yule mama wa WHO asingetangaza huyu waziri wenu

YAWEZEKANA NI KWELI MAANA MPAKA SASA WANALITANGAZA KISIASA SIASA TU.

NB:
YAPASA WAJUE HUU UGONJWA SI WA MASIKINI TU BALI UNAMKUTA KILA MTU HIVYO WAACHE SIASA KWENY HILI JAMBO.
 
Naona kuna tatizo kubwa. Waziri wa afya amesema mgonjwa alipimwa mara alipowasili na kuruhusiwa! Mgonjwa kwa busara zake alijitenga mwenyewe hotelini badala ya kwenda nyumbani! Kwa majibu wa Waziri! Na ndiko ugonjwa ulipoanza kuonekana. Wizara ya afya haijawa makini bado!!!!!
 
Ndio upumbavu wa wanawake. Mwanamke hata awe na elimu,lakini anakuwa kama mtoto tu. Mpaka wasaidiwe kujiongoza. 1. Yeye kasikia huko ulaya kumewaka moto,mpaka nchi kama USA imezuia hizo nchi za ulaya zisiende USA. Lakini bado akapanda ndege kuufuata ugonjwa tena kwenda nchi zile zile zilizozuiliwa. Kama haitoshi akaanza kulanda landa huku na kule,mbwiga kabisa. 2. Amejua kabisa anaweza akawa amenasa kwa nini asibaki huko huko,akaona tena apande ndege atuletee na huku. Haya sasa familia yake imepona hapo?.

Sent using Jamii Forums mobile app


Mkuu alokuaminisha wanawake huwa ni wapumbavu ni nani?? Hebu kuwa na adabu
 
Daaah! Kapimwa kakuta hana akaamua yeye mwenyewe kujiweka karantini
Siamini hili, uwezekano upo alishafahamu Hali yake ndio maana akajifanya kujiweka karantini. Nawaza huenda hata hapo airport vipimo vilionuesha tatizo lakini Kama kawaida ikatembea rushwa ili asitupwe karantini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom