Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Naona kuna tatizo kubwa. Waziri wa afya amesema mgonjwa alipimwa mara alipowasili na kuruhusiwa! Mgonjwa kwa busara zake alijitenga mwenyewe hotelini badala ya kwenda nyumbani! Kwa majibu wa Waziri! Na ndiko ugonjwa ulipoanza kuonekana. Wizara ya afya haijawa makini bado!!!!!
HUYO MGONJWA NI MUUAJI MKUBWA. ITAKUWA ALISHAJUA AMEUNGUA. ALITAKIWA ASIRUDI ABAKI HUKOHUKO ULAYA HADI ATIBIWE NA KUPONA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe watu mko waoga eeh 🤣

Majuzi hapa kuna watu walikuwa wanajidai eti corona ni mafua tu.

Sasa hivi washaanza kujiharishia baada ya kusikia kirusi kishatia timu.

Kwanza si ajabu kilikuwepo muda wote tu ila watu hawajui.
hhhhhhhh corona sio masihara
 
Mshaurini binti huyu anapotangaza suala serious kama hili her body language should indicate so kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mzaa afanye nje ya kamera na pale waandishi wasipokuwepo.
get something to do my friend!
 
Nakwambiaje, hii story kuna sehemu haiko sawa. Instinct zangu zinaniambia hivyo na huwa ziko sahihi 9/10.
1- Mgonjwa katoka ubelgiji kwenye inchi yenye wagonjwa wa COVID-19
2- Mgonjwa amekili kujua kuwa baba mwenye nyumba huko ubelgiji alikuwa mgonjwa wa COVID-19
3- Screening test pale KIA ilikuwa negative
4- Mgonjwa moja kwa moja akaenda Hotel na akajiwekea Isolation
5- Mgonjwa akaripoti hospitali kwa ajili ya sample /confirmatory? Na kweli ikawa positive....

"I'm missing my ass"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tovuti ya Wizara ya Afya Tanzania https://moh.go.tz/en/

Tovuti ya Shirika la Afya Duniani WHO Home


Omba kwa Mungu wako unayemuamini akulinde wewe na uwapendao.

Punguza / acha kabisa tabia ya kujishika maeneo ya usoni (macho, pua, mdomo) maana virusi hivyo vya COVID-19 humuingia binadamu kupitia viungo hivyo. Kwa ulazima wa kujishika sehemu hizo, hakikisha umenawa mikono vizuri kwa maji na sabuni.

Punguza / acha kabisa tabia ya kusalimiana kwa kupeana mikono au kukumbatiana.

Epuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Ikitokea mikusanyiko ya ulazima, basi nunua face mask (zinauzwa katika hardwares, maduka ya dawa n.k) kisha kabla ya kuvaa, nawa mikono yako kwa sabuni na maji, kisha ivae ikifunika pua yako na mdomo.

Utokapo katika mikusanyiko au nje ya unapoishi, nawa mikono yako vizuri kwa maji yanayotiririka na sabuni.

Ripoti katika hospitali au ongozi wa unapoishi kama uonapo dalili za ugonjwa huo wa COVID-19 kwako, au kwa mtu unayemfahamu.

Dalili za COVID-19 na taarifa zingine kuhusu ugonjwa huu zinapatikana katika tovuti za Wizara ya Afya Tanzania pamoja na Shirika la Afya Duniani WHO.

Tovuti hizo nimeziambatanisha mwanzo wa comment hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu kwa jinsi ilivyotangazwa haionyeshi 'seriousness'.. Imekaa kama 'spin' vile.. Tunaingiza sana siasa kwenye mambo ya msingi mpaka kila kitu kinakuwa mzaha.. au Walitaka ku-'overshadow' 'press- conference' ya Mbowe?

Wangejua kuwa sasa hivi SA iko katika 'lockdown' na wametangaza hali ya hatari pia wageni wanakuwa 'discouraged' hasa wanaotoka katika maeneo yenye huu ugonjwa.... na pia wamefunga mashule na baadhi ya 'border' zao kadhaa... Kenya vilevile..

Nafikiri kwa kutangaza hivi kuna maandalizi ya kutosha ya kisaikolojia na kiuchumi.. vinginevyo ..😳
 
Hii taarifa tunayopewa haikukamilika na i hope waandishi wetu wa habari hawatosikiliza tu na kuchapisha wanachoambiwa bila ya kuuliza masuali mengi tu.

Nashindwa kuelewa imekuwaje huyu mama ameweza kurudi nyumbani bila ya kuwa katika karantini ya siku 14 huko ubelgiji ilhali alishakuwepo mgonjwa katika nyuma alokuwa akikaa? Sheria/muongozo katika nchi zote za ulaya kwa sasa ni kuwa kila mgonjwa na kila ambae anajua kuwa amekuwa karibu na mgonjwa ni kujiweka katika self isolation kwa siku 14. Imekuwaje huyu akaweza kutoka nchini ubelgiji bila kukamilisha siku 14 za karantini? Haiingiii akilini kuwa mtu ambae ameshakuwa exposed na mgonjwa wa coronavirus ulaya aamue kuondoka huko bila ya kutimiza siku 14 za karantini na kwenda Africa. Zidharau huduma za afya Africa lakini nchi za ulaya na marekani wako mbele zaidi katika kupata solution ya ugonjwa huu na pia kuna huduma bora za wagonjwa wa ugonjwa huu kuliko afrika kwa kipindi hiki.

Ikiwa (ingawa siamini hata siku moja) kama alitimiza siku 14 za karantini kabla ya kupanda ndege kurudi huku Tanzania na still amejikuta amepata huu ugonjwa, itabidi serikali ya Tanzania iujulishe ulimwengu kuwa karantini ya siku 14 haisaidii kitu ili muda uongezwe.
 
Sikutegemea hata wewe ukose akili kiasi hiki, hivi wanavyofanya wenzetu Ni kwamba hawawapendi wananchi wao walioko nje?

Uganda tu hapo ametoa tamko hapo juzi ukiwa unatoka nje ya nchi yao ukirudi unakaa karantini uwe navyo usiwe navyo..


Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakuambia watu walikuwa hawapimwi?...unataka namna yako ya kuwapima kuwa rais utawapima ambavyo unaona inafaa zaidi wewe.
 
Back
Top Bottom