Uchaguzi 2020 Corona virus: Uchaguzi 2020 kuahirishwa?

Uchaguzi 2020 Corona virus: Uchaguzi 2020 kuahirishwa?

Nadhani tuahirishe, hii ni faida hata kwa upinzanii kwani wengi hawawezi rudi bungeni mwaka huu kama uchaguzi utakuwepo, hivyo ni bora uahirishwe ili hata wao waendelee kula bata
 
Naunga mkono, uchaguzi uahirishwe hadi 2025, hadi Corona iishe duniani kote. Sababu sasa hivi hata maendeleo yatarudi nyuma sababu ya Corona hivyo Mh. Rais wetu apewe miaka 5 ya ziada.
 
Hawajaahirisha Uchaguzi Mkuu bali wamesogeza mbele kupiga kura za maoni ya mapendekezo ya mabadiliko ya katiba itakayo muwezesha kugombea tena.

Mambo yanazidi kuwa mengi huku muda ukiwa mchache.

Kama wababe Russia wanahairisha uchaguzi sababu ya Corona sisi ni nani hadi tufanikishe?

Najiuliza tu makamanda, tuvumiliane.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ninafikiri inawezekana Bunge likae kujadili uwezekano wa kuufuta uchaguzi huu wa mwaka 2020, ukizingatia uwepo wa maradhi ya COVID-19 pamoja na ukosefu wa pesa ili angalau tuweze kujikongoja katika kuendelea na kumalizia miradi tulioianzisha, maana hata demokrasia yenyewe siioni. Tuendelee tu na viongozi waliopo.

Naomba msinielewe vibaya, ni upendo tu kwa nchi yangu Tanzania.
IMG-20200401-WA0017.jpeg


Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Alie kuambia kuwa kuna ukosefu wa pesa nani? Unajua ugonjwa utaisha lini??
Ninafikiri inawezekana Bunge likae kujadili uwezekano wa kuufuta uchaguzi huu wa mwaka 2020, ukizingatia uwepo wa maradhi ya COVID-19 pamoja na ukosefu wa pesa ili angalau tuweze kujikongoja katika kuendelea na kumalizia miradi tulioianzisha, maana hata demokrasia yenyewe siioni. Tuendelee tu na viongozi waliopo.

Naomba msinielewe vibaya, ni upendo tu kwa nchi yangu Tanzania.View attachment 1405795

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app

Zala Na Nga
 
Tumemsikia Rais wetu na Tume ya uchaguzi. Ninashauri, uchaguzi Mkuu 2020 usitishwe na ikibidi itangazwe mapema. Nina sababu za msingi.

1. Hivi sasa tunashghulika na janga baya la Corona, hatuna uhakika na mwisho wake.

2. Vyama vya siasa ukiacha Ccm, vilizuiwa kufanya mikutano hasa ya hadhara hadi mwaka wa uchaguzi. Kama ilikuwa ni kweli, mwaka walioahidiwa umebakia nusu bila kufanya mikutano. Na hii ni coincidencial na janga la corona pia.

3. Tume ya Uchaguz na Taasisi nyingine za umma na binafsi hazitaweza kwa hali hii kuwazungukia na kuwaandaa vyema wananchi kwa uchaguzi. Hadi sasa hao wote wameshachelewa.

4. Nchi wahisani ikiwemo na wale waangalizi,chumi zao zimeyumba,wengine hali ni tete sana,sina uhakika wataacha kwa muda wa karibuni kupambana na covid- 19 waje kwetu.

5. Kama ambavyo nimemsikia Waziri wetu wa fedha,huenda uchumi wetu ukayumba kwani nguvu kubwa itaelekezwa kupambana na corona.

Nia ya wazo hili ni njema, niombe wadau tuendelee kuliboresha kwa manufaa ya Taifa letu.
 
kama Uchaguzi unakuwa suspended basi Mzee Makomeo apashwi kuendelea kuongoza roli hadi Uchaguzi utakapoisha.
 
Kama uchaguzi ukiahirishwa nashauri jeshi ndio liongoze nchi mpaka hapo uchaguzi mwingine utakapotokea!
 
Kididimo,
Mimi nina mtazamo tofauti, uongozi uliopo ukifika mwisho wake Octoba 2020 iundwe Serikali ya Mpito itakayohusisha vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni na hiyo Serikali ipewe jukumu moja tu la kuhakikisha inasimamia mchakato wa uundwaji wa katiba mpya na taasisi zake (Strong Institutions)

zitakazozungumzwa kwenye hiyo katiba ili ifikapo 2025 uchaguzi ufanyike kukiwepo taasisi huru zinazotambuliwa na katiba kama vile Polisi, Mahakama, Tume ya Uchaguzi, nk.
 
Kama hali ya corona ita endelea hivi ni bora uhairishwe au kusogezwa mbele ila ningeshauri kwa hiki kipindi unasogezwa mbele basi wafanye marekebisho ya katiba na pia kuundwe tume huru ili tutakapoanza uchaguzi basi tuwe na tume huru.
 
Back
Top Bottom