Juzi nimeenda kamanga feri kwenye kivuko cha Kamanga Feri, kuna mtu pale nilimkuta ameshika kipima joto
Mtu mwenyewe ukimtazama ni kama kachukuliwa kibarua mmoja kutoka kwenye site za wachina akifanya kazi za udongo, mchafu eti anamulika watu na ka kifaa.
Kama mtu hafanyi hata personal hygiene, hivi kweli huyu anajua kile anachokifanya na kina maana gani? Anajua risk iliyopo?
Ninaamini wapo madaktari, manesi, wafamasia wasiokuwa na ajira na serikali itoe mwongozo kuwatumia hawa.
Hawa wakisikia habari zinazoendelea maeneo kama Italia, Spain ambako wanasema wameanza kuchagua nani atibiwe nani asitibiwe watajua risk iliyopo na watajiongeza katika kazi hii kuliko kumuweka mtu hajui anachokifanya ili mradi kucheki temperature tu.