Mpaka sasa, Serikali haijafanikiwa kuwapa mafunzo watu mbalimbali juu ya kujikinga na virusi vya corona.
Jana nilikuwa Mwanza. Sehemu ya kuongilia, kwenye mlango kuna metal detector box ambapo mtu hupita. Vitu ulivyo navyo, kama simu, vitabu, saa, n.k.; kama ilivyo airport unaweka kwenye chombo ambacho kinasukumizwa na walinzi ili uvichukue upande wa pili. Walinzi wamevaa gloves.
Cha kushangaza, wanaoingia wote ni lazima vitu vyao vipite ndani ya zile containers. Maana yake ni kwamba kama kuna yeyote ana maambukizi, na vitu vyake vipo contaminated, na wale wengine wote watakuwa contaminated kupitia vyombo ambamo wanatumbukiza simu zao na vifaa vingine.
Mimi niliwakatalia. Bahati nzuri walinzi wale hawakuwa wabishi. Waliniruhusu lakini wengine waliendelea kama yalivyo mazoea.
Inaonesha bado maandalizi yetu ni hafifu.