Miongoni mwa familia hii kubwa ya virus iitwayo "Coronaviridae" ni aina saba tu za "coronavirus" zimebainika kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu.
Aina nne za coronavirus zimebainika kusababisha madhara ya wastani yananayofanana na mafua lakini aina tatu zinaonekana kusababisha madhara makubwa kwenye mfumo wa upumuaji na kinga wa binadamu "Severe and acute respiratory syndrome SARS Cov,The Middle east respiratory syndrome(MERS Cov), na sasa SARS Cov-2 ambayo ndiyo aina ya virusi vinavyosababisha ugonjwa uitwao kitaalamu COVID-19.
SARS Cov-2 ni binadamu wa Coronavirus wanaosababisa madhara katika upumuaji na kinga (SARS) virusi hivi vimeangaliwa na kuonekana kufanana jini zao kwa asilimia 79.Ingawa vinafanana bado siyo vya aina ileile moja na udhihirikaji wa magonjwa ya virusi hivi unatofautiana.