Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Aliyekuambia swala la imani halina ujinga nani?

Watu wamekufa kwa kunyweshwa jiki kwa imani kwamba inaponya matatizo yao halafu we unasema swala la imani sio ujinga?

King leopold II kaua waafrica zaidi milion 10 kwa kutumia biblia, halafu mtu anajitokeza anazema swala la imani sio ujinga

Naweza kushawishika ukiniambia imani sio ujinga endapo utasema imani ni upumbavu
 
Understood sir
 
Zingatia maelekezo ya Afya juu ya Korona then Utubu. kuomba Korona iishe pekee wakati mnaendelea na mambo yenu yamchukizwayo Mungu ni kazi bure na mnamtia hasira Mungu.......Tubuni kwanza alafu muombe......
Una hoja ya msingi sana ndugu, kwenye haya maombi, toba ni msingi! Kwa wasomaji wa Bible 2Nyakati 7:14 β€œ ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
 
Watashindana sana lakini hawatashinda, Mungu atabaki kwenye enzi yake milele na milele!
 
Mmetenda wema gani kwa Mungu hata asikie maombi yenu! mnadanganya..mnapoteza watu...mnachukia wenzenu Mungu yupi atasikia labda mungu baali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu Mwenenzi Muumba wa mbingu na nchi huwahurumia watu na kuwasamehe dhambi zao! Hasikilizi Kwa sababu ya matendo yetu Mema, bali Kwa sababu ya Wema wake! Kinyume chake β€œmungu baali” huwashinikiza na kuwatesa wafuasi wake!!
 
Na Tundu Lisu na majeraha yake ya risasi za wasiojurikana!
Kama aliye fanya tukio hilo yumo humu atubu pia! Toba yake aelekeze kwa Mungu na kwa Tundu Lisu, alafu baadaye Mungu atamwelekeza kutubu kwetu, sisi wapendwa wa Tundu Lisu. Mimi kama mmoja wa wanao mpenda Tundu Lisu, namsamehe ili maombi yangu yapokelewe.
 
Una maana gani kusema kipekee ambaliki Mh.Rais. Hivi kwa akili yako mkuu unadhani Mungu anabagua katika baraka na kuponya.
Mwisho,tujiulize ni kitu gani kimetufanya watanzania tugawanyike huku adui yetu akiwa mmoja? Sitaki kwenda mbali bali tujifunze kua sote tu halali mbele za Mungu..
 
Nakuelewa sana mkuu, pia Upo sahihi kabisa, mbele za Mungu watu wote ni Sawa!
 
Kuna kauli inabidi zitoke mahala husika..., Hivi wewe ukiwa kitandani hoi hospitali alafu daktari akasema tunamuachia Mungu si utakata tamaa au kujaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji...,

Kuomba kila mtu aombe (iwe mizimu, mababu zake au hizi dini..), ila kauli inayotoka kwa Amiri Jeshi Mkuu iwe ni mikakati.., Kauli ya madaktari iwe ni wamefikia wapi kwenye kupima na kutafuta chanjo au madawa yapi yanapunguza symptoms as well as ushauri wa kujikinga...,

Kauli za Kuomba na kututia moyo na Imani zibaki kwa viongozi wa roho, kila mtu kwa nafasi yake..., sio nifike hospitali badala ya Daktari kuanza kuangalia medical chart aanze kufungua kitabu na kusoma vifungu...
 
Hopless😈😈😈😈😈😈
 
Hii kitu ni ngumu sana mkuu, hata wale wenye utaalamu wa hali ya juu, wamekwama! Sisi tunaomba, madaktari wapige kazi, pamoja tutaitokomeza corona!
 
Hii kitu ni ngumu sana mkuu, hata wale wenye utaalamu wa hali ya juu, wamekwama! Sisi tunaomba, madaktari wapige kazi, pamoja tutaitokomeza corona!
Nani amekwambia wamekwama ? Mkuu research takes time muda bado, virus hawajamjua vizuri ili kutengeneza chanjo.., Virus haina dawa ni mwili ndio unatengeneza kinga ya kupambana na virus..., na kupata chanjo ni kuwezesha wale ambao hawajapata ugonjwa ili mwili uweze kutengeneza kinga kabla ya kupata ugonjwa..., sadly all those things takes time...

Time ambayo watu wasipofuata ushauri ili ugonjwa usisambae zaidi huenda wakawa ni historia by the time chanjo imepatikana..., Kumbuka pia sidhani kama kifo ni adhabu, na kama kila mtu atakufa na kwa imani yako unaamini Mungu anajua muda na saa, sasa kwanini umpangie akuache uendelee kukaa duniani (au nimekosea Imani yako haisemi hivyo ?)
 
Kipindi mmemshambulia Lisu tulitaka kufanya maombi ya pamoja mkatukataza. Leo hii mnajifanya malaika mnaotambua umuhimu wa maombi wanafki wakubwa nyie.
 
Wakristu wa Afrika wanaongoza duniani kwa uvivu wa kufikiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…