Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Mimi nilijua katika hili msioamini Mungu mtatusumbua sana na wale wasanii ila wanasema wanadini zao lakini ni wanafiki watatusumbua,dini ya kweli yenye mafundisho sahihi haijawahi kuwa ujinga.Hili ni suala la imani sasa kama huna imani waache wenye imani zao,hata wengine wanalindwa na mizimu na wao ni imani na wanaamini wanalindwa.Linapokuja suala la Mungu huwa ni shida ila ingekuwa mambo ya kishetani mngeunga mkono.Dini ya kweli haijawahi kuwa ujinga isipokuwa ninachojua "mambo ya imani kwa wasioamini ni kama upumbavu".Kwa hiyo kama huna imani ni kweli kwako dini ni ujinga na uko sahihi kwa mtazamo wako.
Tatizo haya mambo ni level ya juu kuliko wengi wanavyotamani, kwa hiyo kwa sababu imani Mungu anaangalia utii na siyo akili za darasani au kiwango cha elimu(sisemi tusisome) wengi baada ya kupata vielimu wanaona sayansi ni kila kitu na dini ni ujinga.
Aliyekuambia swala la imani halina ujinga nani?

Watu wamekufa kwa kunyweshwa jiki kwa imani kwamba inaponya matatizo yao halafu we unasema swala la imani sio ujinga?

King leopold II kaua waafrica zaidi milion 10 kwa kutumia biblia, halafu mtu anajitokeza anazema swala la imani sio ujinga

Naweza kushawishika ukiniambia imani sio ujinga endapo utasema imani ni upumbavu
 
Ok,then it is an opinion and not fact,thanks for your view point,we do not become what people say we are if we do not allow to be what they say we are.In communication avoid generalization,they are women who hate men and there men who hate women if you ask them they have a story to tell for their view point but we can not generalize and say men are bad or women are bad.It is called perception a.k.a. Mtazamo.
Understood sir
 
Zingatia maelekezo ya Afya juu ya Korona then Utubu. kuomba Korona iishe pekee wakati mnaendelea na mambo yenu yamchukizwayo Mungu ni kazi bure na mnamtia hasira Mungu.......Tubuni kwanza alafu muombe......
Una hoja ya msingi sana ndugu, kwenye haya maombi, toba ni msingi! Kwa wasomaji wa Bible 2Nyakati 7:14 “ ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
 
Dunia ya leo ina wacha Mungu wa kweli wachache mno. Nao wapo ktk kila dini na matendo yao huthibishwa kupitia uadilifu, maadili na hata ibada zao.Tunaishi nao pamoja ktk jamii zetu, huwa ni wenye bidii ktk ibada ili kumtafuta Mola wao, wawazi na wakwelii.

Na kutokana na hilo baadhi yao wakihukumiwa pasipo makosa yoyote yale, na hata wengine wakiwajibishwa pale wanapotofautiana kimsimamo na watu dhalimu na waovu. Ni ukweli kwamba vipo vyama vya kisiri vyenye kutaka kuitawala dunia yote kwa matakwa yao, ikiwemo ya kiunabii kupitia kuwa na dini moja.

Naam! Vyovyote vile iwavyo, wengi wetu hupenda kuziita hoja kama hizi kuwa ni "Conceptual & Conspiracy Theories" lkn ukweli ni matukio makubwa ambayo hutokea duniani huratibiwa kwa usiri mkubwa na makundi ya watu hawa.

Katika kitu ambacho kiliwandisha kwa muda mrefu ni suala la muundo wa dini moja. Na kipo kitu ambacho siku zote kimekuwa kikiwazuia kufaniksha jambo hili ni uweza wa kimungu, ambao kwa wale wenye imani ya Kikristo huiita uweza huu Roho Mtakatifu.

Tunasikia kilio chenye kutaka kuondoa ama kupiga marufuku mikusanyiko ya kidini ktk kipindi hiki cha janga la Corona. Na tena suala siyo wafanye hivyo kwa kuzingatia masuala ya kiafya kwenye nyumba na sehemu za ibada kama vile "social distancing" bali wasikubaliwe kutenda kazi zao kabisa.

Hakika hawa wacha Mungu ndio walengwa haswa wa ujio wa gonjwa hili. Kila uchao tutasikia masharti mapya na hatimaye suala kuendesha ibada litaonekana kuwa ni tishio kubwa la "Community transmission". Kwa mazingira haya nguvu hii ni wakati wake maalum uliopangwa kutokea na sasa utafanikiwa.

Ni muda rasmi umefika wa uweza huu wa kimbingu kuondolewa duniani katika duniani Advocaters na mashabiki wa mpango huu kilio chao sasa kimesikika. They asked for some, now they have to come and take some. The game has just begun, and we are all in it. Kila asikiaye na azingatie haya.


Sent using Jamii Forums mobile app
Watashindana sana lakini hawatashinda, Mungu atabaki kwenye enzi yake milele na milele!
 
Mmetenda wema gani kwa Mungu hata asikie maombi yenu! mnadanganya..mnapoteza watu...mnachukia wenzenu Mungu yupi atasikia labda mungu baali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu Mwenenzi Muumba wa mbingu na nchi huwahurumia watu na kuwasamehe dhambi zao! Hasikilizi Kwa sababu ya matendo yetu Mema, bali Kwa sababu ya Wema wake! Kinyume chake “mungu baali” huwashinikiza na kuwatesa wafuasi wake!!
 
Na Tundu Lisu na majeraha yake ya risasi za wasiojurikana!
Kama aliye fanya tukio hilo yumo humu atubu pia! Toba yake aelekeze kwa Mungu na kwa Tundu Lisu, alafu baadaye Mungu atamwelekeza kutubu kwetu, sisi wapendwa wa Tundu Lisu. Mimi kama mmoja wa wanao mpenda Tundu Lisu, namsamehe ili maombi yangu yapokelewe.
 
Mkuu, wapingaji mbona wako hapa Tu, wakitumia vidole vyao kuchapisha Mandiko ya kupinga na kukataa maombi, lakini mbona tunakutana vizuri huko kwenye nyumba za Ibada!!

Wacha wapinge, lkn Giza la mauti lijapotanda miongoni mwa jamii zao, Jeuri yote itawakimbia, mwenye jeuri ya kumdhihaki Mungu hajawahi kuzaliwa hii Dunia, farao na Ujinga wake wote, alikubali kuwaachia Wana Israel wsondoke mikononi mwake

Wanasahau wakizani hili nalo ni kama Upinzani wa CCM na Chadema, wakidhani wanamkomoa Mbowe na Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania, uwabariki na viongozi wetu wa kisiasa,

Kipekee Mbariki Raisi wetu JPM
Una maana gani kusema kipekee ambaliki Mh.Rais. Hivi kwa akili yako mkuu unadhani Mungu anabagua katika baraka na kuponya.
Mwisho,tujiulize ni kitu gani kimetufanya watanzania tugawanyike huku adui yetu akiwa mmoja? Sitaki kwenda mbali bali tujifunze kua sote tu halali mbele za Mungu..
 
Una maana gani kusema kipekee ambaliki Mh.Rais. Hivi kwa akili yako mkuu unadhani Mungu anabagua katika baraka na kuponya.
Mwisho,tujiulize ni kitu gani kimetufanya watanzania tugawanyike huku adui yetu akiwa mmoja? Sitaki kwenda mbali bali tujifunze kua sote tu halali mbele za Mungu..
Nakuelewa sana mkuu, pia Upo sahihi kabisa, mbele za Mungu watu wote ni Sawa!
 
Kuna kauli inabidi zitoke mahala husika..., Hivi wewe ukiwa kitandani hoi hospitali alafu daktari akasema tunamuachia Mungu si utakata tamaa au kujaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji...,

Kuomba kila mtu aombe (iwe mizimu, mababu zake au hizi dini..), ila kauli inayotoka kwa Amiri Jeshi Mkuu iwe ni mikakati.., Kauli ya madaktari iwe ni wamefikia wapi kwenye kupima na kutafuta chanjo au madawa yapi yanapunguza symptoms as well as ushauri wa kujikinga...,

Kauli za Kuomba na kututia moyo na Imani zibaki kwa viongozi wa roho, kila mtu kwa nafasi yake..., sio nifike hospitali badala ya Daktari kuanza kuangalia medical chart aanze kufungua kitabu na kusoma vifungu...
 
Kuna kauli inabidi zitoke mahala husika..., Hivi wewe ukiwa kitandani hoi hospitali alafu daktari akasema tunamuachia Mungu si utakata tamaa au kujaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji...,

Kuomba kila mtu aombe (iwe mizimu, mababu zake au hizi dini..), ila kauli inayotoka kwa Amiri Jeshi Mkuu iwe ni mikakati.., Kauli ya madaktari iwe ni wamefikia wapi kwenye kupima na kutafuta chanjo au madawa yapi yanapunguza symptoms as well as ushauri wa kujikinga...,

Kauli za Kuomba na kutitia moyo na Imani zibaki kwa viongozi wa roho, kila mtu kwa nafasi yake..., sio nifike hospitali badala ya Daktari kuanza kuangalia medical chart aanze kufungua kitabu na kusoma vifungu...
Hii kitu ni ngumu sana mkuu, hata wale wenye utaalamu wa hali ya juu, wamekwama! Sisi tunaomba, madaktari wapige kazi, pamoja tutaitokomeza corona!
 
Hii kitu ni ngumu sana mkuu, hata wale wenye utaalamu wa hali ya juu, wamekwama! Sisi tunaomba, madaktari wapige kazi, pamoja tutaitokomeza corona!
Nani amekwambia wamekwama ? Mkuu research takes time muda bado, virus hawajamjua vizuri ili kutengeneza chanjo.., Virus haina dawa ni mwili ndio unatengeneza kinga ya kupambana na virus..., na kupata chanjo ni kuwezesha wale ambao hawajapata ugonjwa ili mwili uweze kutengeneza kinga kabla ya kupata ugonjwa..., sadly all those things takes time...

Time ambayo watu wasipofuata ushauri ili ugonjwa usisambae zaidi huenda wakawa ni historia by the time chanjo imepatikana..., Kumbuka pia sidhani kama kifo ni adhabu, na kama kila mtu atakufa na kwa imani yako unaamini Mungu anajua muda na saa, sasa kwanini umpangie akuache uendelee kukaa duniani (au nimekosea Imani yako haisemi hivyo ?)
 
Kuomba kwa siku tatu kama alivyo agiza mheshimiwa Rais Magufuli Siyo: kuacha kuzingatia maelekezo yote ya kitaalamu, siyo kukubali kwamba serikali ipo sahihi kwa kila kitu! Siyo kuunga mkono juhudi, siyo kufumbia tatizo macho!

Kukubali kuomba ni kukubali kwamba janga hili ni kubwa, ni kuona jinsi ambavyo, hata nchi zenye maendeleo makubwa ya kitabibu na utaalamu, wamekwama! Ni kuamini kwamba mwenyenzi Mungu anaweza kutusaidia, kutokomeza ugonjwa, kutupa hekima ya kukabiliana na ugonjwa na kutulinda! It is a high time that we work together in unity, because we have a common enemy!

Tunatofautiana itikadi, imani na mambo mengi kimtazamo, lakini tuna adui mmoja anaye tushambulia kwa sasa, tuungane kumkabili! Kila Mtu kwa imani yake, Mh. Godbless Lema ametuwekea mfano.
Kipindi mmemshambulia Lisu tulitaka kufanya maombi ya pamoja mkatukataza. Leo hii mnajifanya malaika mnaotambua umuhimu wa maombi wanafki wakubwa nyie.
 
Fuata kanuni za wataalamu wa afya including social distance,epuka mikusanyiko ya hovyo,ndo Mana tukapewa akili Sasa ukisema usali bila kuchukua hatua mwishowe utakuja kulaumu Mungu bure kumbe unakuwa hukutumia akili ndogo hata za kuvukia barabara.

N.B Mimi napenda kusali Sana Ila saa nyingine wakristo huwa tunatumia maandiko vibaya hata vitu vya kutumia akili ya kawaida tuna mchosha Mungu, mwishowe maombi hayajibiwi tunakuwa ka wale manabii wa baali. Tuchukue tahadhari corona is real

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakristu wa Afrika wanaongoza duniani kwa uvivu wa kufikiria
 
Back
Top Bottom