Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Je, hili ni ombi rasmi la rais?

Binafsi nasikitika. Imani ikizidi inakuwa ni tatizo ktk maisha ya watu. Corona haitatoweka kwa maombi. Ningetegemea serikali itoe maelekezo kwa makanisa na misikiti ili viongozi wa dini wasaidie kusambaza maelekezo.

Tukiwadekeza viongozi wa dini, nchi itaangamia. Hili ni jambo la kiafaya siyo la kiroho na haliwezi kutatuliwa kiroho!

Historia haioneshi kwamba kuna magonjwa yanatoweka duniani kwa maombi.
 
Kwa hiyo wewe kumwomba Mungu ni kukata tamaa? Hivyo wewe huomba Mungu tu ukishakata tamaa?
"Corona ni ugonjwa Mdogo sana..kuna magonjwa yanauwa kuliko corona..Watanzania tusitishane"..Alisikika akisema Kenge mmoja hivi akiwa amelala kwenye mawe.
 
Kwa hiyo wewe kumwomba Mungu ni kukata tamaa? Hivyo wewe huomba Mungu tu ukishakata tamaa

Maana yake kuwa umeona options zote za kibinadamu hazikusaidii hivyo unarudi kwa muumba wako as a last resort!! Ndio kukata tamaa huko.
 
Wabongo bwana yaani sisi kila kitu tunapinga tu..kwani mh kakosea wapi???!!..hiyo hatua ya kututaka wananchi tuombe,si yeye tu!.hata Trump,waziri yule wa italy,uingereza wote wanawasisitiza wananchi wao waombe kwa MUNGU..hili dude hakuna serikali Afrika inayoweza kutunisha misuli kupambana nalo,ni MUNGU tu!
Mnaposema tumuachie Mungu au tumuombe Mungu atusaidie, mbona hamsemi atusaidiaje..?? Labda ufafanue vizuri

Isije ikawa ndio yale yakujifungia ndani unasali Mungu akupe utajiri au akupe chakula, huo utakua ujinga wa kiwango cha SGR.

Tumuombe Mungu atupe maarifa na akili za kupambana na huu ugonjwa maana sisi akili zetu ndogo saana, kila mtu mtaalamu viongozi wanabonga bonga tu kama wendawazimu, wataalamu wa tiba na madawa wamekaa kimya kama hawapo vile utadhani walisomea kilimo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo bwana yaani sisi kila kitu tunapinga tu..kwani mh kakosea wapi???!!..hiyo hatua ya kututaka wananchi tuombe,si yeye tu!.hata Trump,waziri yule wa italy,uingereza wote wanawasisitiza wananchi wao waombe kwa MUNGU..hili dude hakuna serikali Afrika inayoweza kutunisha misuli kupambana nalo,ni MUNGU tu!
Yaani ajifanye jeuri...asichukue hatua za tahadhari mapema za kulinda RAIA wa Tanzania, watu wameanza kuugua na kupoteza maisha

Ndio anamkimbilia Mungu...!??

Nasema kwa uzembe wake...Atawajibika kwa Mungu

Kilio chetu kwa Mungu nipamoja. na kumuomba Mungu atende kwa kadiri inavyompendeza...atufute machozi na wote walizembea na kusababisha ugonjwa kuenea...tunawakabidhi mikononi kwa Mungu...yeye ndiye Msemaji wa Mwisho

Naamini atatenda.....Tufunge Tusali kwa umoja wetu Mungu anakwenda kujibu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG-20200416-WA0006.jpg
 
Handsome Rob,
Akusaidiaje kwani MUNGU ni mjomba wako???.. mwenyezi MUNGU husaidia vile impendezavyo,na si vile utakavyo!.. anyway,sisi ulimwengu tumeukuta wacha tumuombe,tuna imani atatusaidia
 
Back
Top Bottom