Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Enzi za Musa na wana wa wa Israel akisafiri jangwani miaka mingi ,mambo mazito mapigo mazito kama haya ya magonjwa,tauni n.k

Alikuwa akipanda mlimani na kufunga na kusali sana akiwaombea msamaha wakosaji na Mungu aliwasamehe ,basi nasi twendeni mlimani yaani kusali na kujutia Dhambi zetu.
 
Kuna kipindi cha awamu ya 4 waziri mkuu aliongoza maombi na sara za kitaifa kuombea mvua baada ya ukame wa muda mrefu. Nikajua ilikuwa ni kukwepa majukumu ya serikali, iliyotakiwa kuweka miundombinu ya umwagilaiji. Tangu lini mvua ikaletwa kwa maombi? Baadaye akaja mzee wa Loliondo. Wanasiasa wakatoa support hadi magari ya kusafirisha watu na kumsaidia mganga kuvuna miti ya kikombe. Yaonekana hatujifunzi chochote kwa hayo ya nyuma na hata hivyo madhara ya kuombea mvua, hayakuonekana.

Sasa ni Corona. Ni uzembe unaoungwa mkono, ukweli unabaki pale pale. Nchi hii haiwezi kuwa ya kwanza kuondoa magonjwa kwa sara. Tukubaliane kwamba tuko njia potofu tena potofu kuliko kipimo. Dar inaongoza kwa maambukizi, lakini tunaruhusu watu kunywa pombe, kusafiri kwa mabasi kwenda mikoani na kusambaza ugonjwa. Badala ya kufuata njia zinazotumika kwingine duniani, tumegundua makanisa na misikiti yetu ina miujiza saaana!

Viongozi munapoanza kuheshimu miujiza, ni tatizo kwa raia. Nchi inaangamia.
 
Neno Insernity linasema mengi kuhusu TZ na waafrica kwa ujumla
  1. Insanity Meaning-the state of being seriously mentally ill; madness
  2. "The definition of insanity is also "doing the same thing over and over again, but expecting different results." This was established by Albert Einstein.
 
Wana akili za kijinga wanafikiri Mungu yuko kwa ajili ya watanzania tu na sio waitali, wachina, waamerika, wahispania, nk Tuna tatizo la kujimilikisha Mungu kwa kila kitu ndio maana huwa hatufanikiwi. Ukija kwenye mpira ni hivyo hivyo utaona wanasema watanzania waiombee timu ishinde. Ni ujinga mtupu tena ina kuwa ni wendawazimu zaidi unapoona wanaojiita madokta na maprofesa ndio wanaosema tumwombe Mungu eti haka ni Kagonjwa!
 
Wewe ndio mjinga biblia inasema amellaniwa MTU yule asiyependa Wa kwao .first duty in kwa nchi yako kwa watu wako
 
Mleta mada kama huwa huombi mafanikio yako hayawezi kuwa endelevu utashangaa wewe akili zimo watoto Hamna kitu hata uwekeze kwao vipi Wewe una kazi mitoto Hamna kitu

Na Wewe na tu mafanikio twako koko TWA sasa utatamba gamba NATO Sikh mbili tatu lakini kama husali nakuhakikishia mbeleni utajikuta chalk kama mende ukiwa choka mbaya sababu maombi na sala za ulinzi huna
 
Mimi mpaka niambiwe aliye mshambulia
Tundu lisu
Aliyemua ALPHONSO mawazo
Aliyemteka kagoye
Aliye mteka na kumpoteza ndugu ben sanane
Na wengine woote waliopatwa na madhira ndo nitaomba mungu.
Vinginevyo siwezi kujiunga na mashetani kwa mambo ya kishetani
UNAMUOMBA MUNGU KISHA KESHO UNAMWEKEA MTU SUMU NDO NN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binaadamu huwa tunapenda sana kujiona sisi ni special mbele za Mungu wakati Mungu ana viumbe kibao hadi vingine hatuvifahamu

Wakati sisi tunamuomba Mungu atuondoshee hivi virusi na vyenyewe navyo vinamuomba Mungu tushindwe kuvidhibiti ili viendelee kuponda raha za dunia wao raha yao ni kuingia katika mapafu ya binaadam

Yawezekana Mungu akapokea dua ya corona virus kuliko dua ya binaadam maana sidhani kama corona virus wanatenda makosa mbele za Mungu kama tutendayo sisi binaadam

Na nilicho gundua kimbe kimoja kukiua kiumbe kingine hilo kwa Mungu sio tatizo na ndio maana sisi binaadam kila siku tunachinja kuku , mbuzi na tunavua samaki hivi vyote ni viumbe vya Mungu lakini sisi tunavisababishia vifo vyao

Hivyo tuendelee kusikiliza ushauli wa raisi wetu mimi binfsi sijui yupo kwa sasa tuendelee kuomba dua na kunawa mikono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si vikakae kwa CEO & Founder wao Mr. Popo.
 
Sisi wenyewe ndio tumevitoa kwa popo na kuvileta kwetu labda vimegundua kuishi kwa binaadam ni raha zaidi kuliko kwa popo
 
Virusi sio viumbe mkuu. Havina sifa ya viumbe hai.
 
Sisi wenyewe ndio tumevitoa kwa popo na kuvileta kwetu labda vimegundua kuishi kwa binaadam ni raha zaidi kuliko kwa popo
Kwa popo hakuna bata la kutosha maana muda mwingi analala...ila binadamu ni 24 season zote yupo macho na mikusanyiko kibao
 
Back
Top Bottom