Coronavirus: Safari zote za Hijja zapigwa marufuku kwa muda Saudi Arabia

Coronavirus: Safari zote za Hijja zapigwa marufuku kwa muda Saudi Arabia

Soma hii mistari ya moto

Kumbukumbu la Torati 4:35: “Wewe ulionyeshwa mambo haya ili upate kujua ya kuwa Bwana ni Mungu; badala yake hakuna mwingine.” Kumbukumbu 6:4 “Sikieni, enyi Israeli, Bwana Mungu wetu Bwana ni mmoja.” Malaki 2:10a, “Je, sisi zote hatuna Baba mmoja? Je, si Mungu moja alituumba? 1 Wakorintho 8:6 “Hata hivyo kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka na kwa ajili yake sisi tunaishi; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye kupita kwake vitu vyote vinatoka na ambaye kwa njia yake sisi tunaishi. Waefeso 4:6: “Mungu Mmoja na Baba wa vyote, ambaye ni juu ya yote na katika yote na ndani ya wote.” 1 Timotheo 2:5: “Maana yuko Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, amabaye ni Kristo Yesu.” Yakobo 2:19: “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja. Ni vyema, hata mapepo wanaamini kwamba kuna Mungu mmoja na hutetemeka kwa hofu.”
Kama kulikuwa na Mungu zaidi ya mmoja, ulimwengu ungekuwa katika machafuko kwa sababu ya wabunifu wengi na mamlaka, lakini siyo katika machafuko, kwa hiyo, kuna Mungu mmoja tu.

Tangu Mungu ni kiumbe kamili, kamwe hakuwezi kuwa na Mungu wa pili, kwa sababu wangekuwa tofauti katika baadhi ya njia, na kuwa tofauti kwa ukamilifu hiyo ni kuwa chini ya kamilifu na kukosa kuwa Mungu.
Hujathibitisha Mungu yupo, unahubiri.

Thibitisha Mungu yupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata mimi kuna muda huwa najiuliza kwa nini inakuwa hivi yaani baadhi ya vitu Mungu anashindwa kuzuia na uwezo anao.

Bado nasoma kile kitabu uliwahi weka hapa siku nyingi

'Philosophy of religion. An anthology'

Kwa kweli nimejifunza vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiulize nawewe kwanini umeshindwa kuacha dhambi? Siku ukiacha dhambi hakika Mungu atakukingeni na majanga haya. Kucha kutwa unaenda kinyume na mafundisho yake halafu ukipata majanga ndio unamlilia? Una reasoning capacity ndogo sana kijana.
 
Unakubali Mungu ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba Peke Yake". (Mathayo 24:36)
"Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mmema". (Mithali 15:3)
"Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu, Naye huiona miendo yake yote. Hapana weusi, wala hilo giza tupu, Wawezapo kujificha watendao udhalimu". (Ayubu 34:21-22)
"Je! Huoni kwamba Allah (Mwenyezi Mungu) anajua vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini? Haupatikani mmong’ono wa watu watatu ila yeye huwa ni wanne wao, wala wa wachache kuliko hao wala zaidi ila yeye huwa pamoja nao (kwa ujuzi wake), popote walipo; kisha siku ya kiama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Allah (Mwenyezi Mungu) ni Mjuzi wa kila kitu". (Qur. 58:7)
"Yeye ndiye Allah (Mwenyezi Mungu) ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu. Anayeyajua yaliyofichikana na yaliyo dhahiri. Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo". (Qur. 59:22)
"Na hakika Mola wako atawapa hao wote malipo ya vitendo vyao sawa sawa. Bila shaka Yeye anazo khabari za (yote) wanayoyatenda". (Qur. 11:111)
 
Mungu kashindwa kuwanusuru watu wake na janga hili?

Hata wanaokwenda Hijja?

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi za watu tu?
Mungu amewaleta duniani akakupeni muongozo wa maisha, ikiwemo nini cha kuliwa na nini kisiliwe, na akawausia mule vyakula vizuri..mkajitia wajuaji mkaanza kula supu ya popo na uchafu kama huo, halafu mnataka awanusuru... Kisha mnamlaumu..atawanusuru lakini baada ya kuwadiscipline kwanza akili irudi mahali pake...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu - Makka na Madina.

Mamilioni ya watu huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija.

Tofauti na Hija, Umra hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.

Bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo pamoja na kusambaa kwa Virusi vya Corona duniani.

Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.

Mpaka sasa Saudia bado haina mtu ambaye amethibitika kuambukizwa virusi hivyo.

Makka, ndio mji ambao Mtume Muhammad alipozaliwa, na kuna msikiti mtakatifu zaidi. Madina ndipo alipofariki na kuzikwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia inasema marufuku hiyo ni ya muda - lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa.

Watalii ambao si wa kidini ambao wanatoka katika nchi ambazo virusi vya corona vimethibitisha kuingia pia watakataliwa kuingia Saudia.

Saudi Arabia imeeleza kuwa toka mwezi Oktoba imetoa viza zaidi ya 400,000 za watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema wiki hii limeonya kuwa dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.

WHO japo imesema kuwa ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".

Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia.

Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa mengi zaidi ya Uchina mabapo ndipo ulipoanzia.

Mpaka sasa zaidi ya watu 2,700 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Toka Virusi vya Corona viripotiwe mwezi Disemba, zaidi ya watu 80,000 duniani, kutoka katika mataifa takribani 40 tayai wameshaambukizwa virusi hivyo. Wengi wao wakiwa nchini Uchina.

Iran (ambayo imetenganishwa na Saudia kwa mkondo mwembamba wa bahari) mpaka sasa imesharipoti vifo 19 - ambayo ni namba kubwa zaidi ya watu kwa mataifa ya nje ya Uchina.

Hata hivyo vifo hivyo vinatokana na wagonjwa 139, hali ambayo inawafanya madaktari wa magonjwa ya kuambukiza kuhofia kuwa nchi hiyo inaweza kuwa na wagonjwa wengi zaidi inaowaficha.

Barani Ulaya hali ni mbaya zaidi nchini Italia ambapo mpaka sasa watu 400 wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo kutoka watu 80 siku ya Jumanne. Watu 12 tayari wameshafariki nchini humo kutokana na mlipuko huo.

Kwa Afrika ni nchi mbili mpaka sasa zimethibitisha kuingia kwa ugonjwa huo. Algeria na Misri kila moja imeripoti mgonjwa mmoja.

Chanzo: BBC
Waje wafanye safari za HIJA huku Kilwa Kivinje kwenye ule msikiti wa kale
 
Mungu amewaleta duniani akakupeni muongozo wa maisha, ikiwemo nini cha kuliwa na nini kisiliwe, na akawausia mule vyakula vizuri..mkajitia wajuaji mkaanza kula supu ya popo na uchafu kama huo, halafu mnataka awanusuru... Kisha mnamlaumu..atawanusuru lakini baada ya kuwadiscipline kwanza akili irudi mahali pake...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa thibitisha Mungu yupo.

Unajuaje Mungu yupo, na kwamba habari za Mungu kuwepo si uongo ambao watu wamejitungia tu kama jibu la maswali ambayo hawana majibu yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpumbavu wewe unayetaka kunyamazisha watu katika forum ambayo kauli mbiu yake inajivunia watu kuongea kwa uhuru.

Siachi kuandika mawazo yangu, utafanya nini?

Thibitisha Mungu yupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo lako umestick katika mawazo hasi wakati kuwa flexible kimawazo kutakufanya ujue vitu vingi sana
Je wajua ni dunia pekeee kwa wanasayansi wamegundua ndio kuna maji pekee
Lakini siri ya mungu huenda kuna madunia mengine makubwa yapo mbali na sisi ila kwa upeo wetu hatuwezi kuwaza....
Kama kiranga unatumia internt iliyotengenezwa na watu
Simu zilizotengenezwa na watu
Magari yaliyotengenezwa na watu

Itashindikana vp wewe kukaa katika ulimwengu ulioyetengenezwa na kitu chenye uwezo mkubwa zaidi..na kibina damu tunakiita mungu.
Sasa binaadamu ndio wamekuja na tafsri zao kama hizi

Mungu ni allah
Mungu ni yesu kristo
Mungu ni masanamu 360
Mungu ni jua
Mungu ni ng'ombe
Mumgu ni mizimu
Hizo zote ni tafsri za kibina adamu ila haijalishi LAZIMA KUTAKUWEPO NA MMILIKI WA ULIMWENGU
 
Mungu kashindwa kuwanusuru watu wake na janga hili?

Hata wanaokwenda Hijja?

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi za watu tu?
Hizi statement (blasphemy) hata aliyemshoot Lissu akiziona atakasirika 🙂
 
Back
Top Bottom