Hakuna ajuaye chanzo cha ulimwengu.
Wote wanaojaribu kuelezea, wanafanya hivyo kwa kukisia tu.
Na ndo maana maswali kuhusu chanzo cha ulimwengu hayaishi.
Kuna mambo mengi mno hapa ulimwenguni ambayo hatuyajui.
Majuzi hapa James Webb Space Telescope imegundua galaxies ambazo zinafikirisha kuhusu dhana/ nadharia ya Big Bang.
Zaidi,
Inawezekana dhana nzima ya chanzo katika muktadha huu ni potofu, inabidi tuitazame upya, tunaisema kwa anthropic bias. Ni kama tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunafikiri ukitembea saaana utafika mwanzo wa dunia na ukiendelea utaanguka nje ya dunia.
Tunautafuta huo mwanzo.
Wakati dunia ipo kitufe zaidi na unaweza kutembea sana ukarudi ulipoanzia.
Ukisoma sana quantum physics utagundua kuwa kuna mambo mengi sana hatujayajua vizuri, dhana kama ya causal quantum loop, inayosema kwamba unaweza kuwa na A ambayo inaisababisha B wakati huo huo B nayo ikawa inaisababisha A kwa namna ambayo kati ya A na B huwezi kusema nini kinasababisha nini, inakuwa very counterintuitive tukiifikiria kwa scale yetu na models zetu za classical physics ambazo tumezoea kuona kuna mama anazaa mtoto, na mama ndiye anasababisha mtoto awepo.
Sasa hapo ukiambiwa kwenye quantum physics kuna kitu kama mama anazaa mtoto na mtoto naye vile vile ndiye aliyemzaa huyo mama, inachanganya.
Sasa kama quantum physics tu hatujaieleea vizuri (watu wote wa dunia bado hatujaielewa vizuri) hatuwezi kisema tunaeleza chanzo cha ulimwengu ni nini.
Yani hata dhana nzima ya chanzo , dhana yenyewe, hatujaielewa bado.
Tunaielewa katika classical physics tu. Tukienda katika quantum physics hatuelewi chanzo ni nini.
Zile virtual partickes zinazotokea out of the vacuum of spacetime hatujui chanzo chake ni nini, hatujui kama zinahitaji chanzo au zinaweza kuibuka tu randomly.
Hatujui chanzo cha quantum entaglement ni nini, inakuwaje particles zilizo million of light years away ziwe zinageuka pamoja kama mapacha alnost instanltly defying the soeed of light limit. How does this work?
Huo muda wenyewe hatujaweza kuu define vizuri.
Suala la chanzo ni suala la muda. Lakini muda ni nini?
Ukiondoa vyote katika ulimwengu, muda utakuwepo bado? Utakuwapo vipi?Muda ni relation ya vitu, unapimwa kwa movement ya vitu. Ukiwa huna kitu katika ulimwengu huna muda, au hata uki freeze kila kitu huna muda. Au kwa kitu kinachokwenda at the speed of light muda unasimama.
Sasa kama hatujaweza kueleea hayo mambo mengi vizuri, tutasemaje tunaelewa hata dhana ya chanzo maana yake ni nini na ni ya msingi kwa kiasi gani?
Kwa nini ulimwengu katika upana wake wote usiweze kuwa ulikuwepo tu daima na sisi tunaposema hapa ukimwengu ukianza, kwa mfano kwa Big Bang Theory, pasiwe ni cycle moja ya sehemu moja tu ya ulimwengu? Kuna sheria gani ya kisayansi inayozuia hilo?