COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Kwani wewe unasubiri lockdown ya serikali? Yaani utakuwa mbumbumbu wa kufa. Serikali ilishatoa tahadhali siku nyingi sasa wewe ni juu yako kusuka au kunyoa.
Kenge wewe,nani kasema nasubiri serikali itangaze?Mimi nilimuiga JPM kitambo,familia yangu iko kijijini nimeipeleka huko mapema sana!Nimebaki mjini napambana mwenyewe huku nikuchukua tahadhari!Sasa wewe jidanganye umeambiwa upige kazi na usitishike wakati anayekuambia hivyo kakimbia na familia yake kujificha kijijini!Za kuambiwa changanya na zako!Period!
 
Duuuuh! Tunaongoza EA kwa sasa! Wacha tu nchi majirani watutenge maana tunasambaza hili gonjwa makusudi sasa! Kama hatuchukui hatua proven na WHO na wataalamu wabobezi maana yake tunafanya makusudi mazima kulisambaza!

Hiki kiburi sijui kinatoka wapi! Ewe Mola wetu tuepushe na balaa hili.
Serikari yako ndiyo iliyowazi kuliko huko unakosema mkuu, huu ugonjwa, nchi zote kabisa wakiamua kusema ukweli kabisakabisa, na watu wengi wakapimwa, hakuna penye unafuu mkuu
 
Kiburi kinaanzia kwa yule aliyewadanganya eti wafanye maombi na kazi tuuu! Double standard nayo imechangia. Leo lisemwe hili kesho msitishwe, keshokutwa maombi, mtondogoo mask lazima. Lipi tuchukue.
Chagua unalotaka ass!
 
ohooo sawa.
Sababu hao ndo mawaziri wapya wa afya.
Wakiweka picha nyingine za makaburini usisite kutuletea huku.
mlikuwa mnalalamika serikali inaficha idadi ya wagonjwa haya sasa hao hapo 480.
ukitaka lia ukitaka cheka..
Ila habari ndo hyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kichwa chako kina kazi gani?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''

Waziri wa afya ni mjanja kaogopa lawama ya kutoa taarifa ya kupunguza idadi ya vifo kaamua kumwachia zigo waziri mkuu
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia April 23 hadi Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''
Mbona hii taarifa mkuu umeileta nusu au kwamba hukusikiliza hadi mwisho ukawahi kuja kuleta uzi.

Sijaona hapa taarifa ya wagonjwa walio pona 167 au hilo hukusikia kama PM alisema nalo?? Idadi ya Vifo pia siioni hapa ambavyo vimeongezeka vifo sita na sasa jumla ni ya vifo 16 hili hukusikia mkuu??
Wagonjwa walio baki kwa sasa jumla ni 296 na kati ya hao 283 wapo kwenye hatua nzuri za maendeleo kiafya, ni watu 14 ndio ambao wapo kwenye uangalizi wa karibu wa madaktari.

Hukutaka kuleta taarifa vizuri sijui kwa lengo lipi labda?
 
Vifo sita wakati kila kona ya nchi kwa kila mkoa na kwa kila siku watu wanazikwa kila siku? Huna macho? Huna masikio? Wewe ni mbumbumbu wa kung'amua mambo?Bosheni/danganya mach unaziita ni vifo?
ukiona maziko ya watu wasiozidi 10 pigia mstari
 
Sasa ni official, tunaongoza East Africa. Pia tumekuwa tuki-export cases mpya kwenda Uganda kupitia kwa madereva wa magari makubwa.
Pamoja na mafanikio haya ya kuongoza na kusambaza ugonjwa nchi za jirani pia tumeamua kuzika watu usiku kwa siri.

Wenzetu Uganda walioharakisha kufanya maamuzi magumu sasa hali ni nzuri na wanaanza phases za kuondoa lockdown.

Viva Tanzania
 
Da tumeisha 🤔🤔🤔 haka kagonjwa kanatisha 🙌🙌🙌
 
Kenge wewe,nani kasema nasubiri serikali itangaze?Mimi nilimuiga JPM kitambo,familia yangu iko kijijini nimeipeleka huko mapema sana!Nimebaki mjini napambana mwenyewe huku nikuchukua tahadhari!Sasa wewe jidanganye umeambiwa upige kazi na usitishike wakati anayekuambia hivyo kakimbia na familia yake kujificha kijijini!Za kuambiwa changanya na zako!Period!
Mimi napiga kazi hata hapa niko na Laptop naendelea na kazi kama kawaida halafu jioni naingia bar napiga bia zangu then narudi home kupiga usingizi. Unalo jingine?
 
Back
Top Bottom