COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Gallius,
Yaani im worrying for them kuliko hata ninavyojiworia mimi. Yaani acha tu. Hapa kila siku nawapigia simu nawasisitiza wabaki majumbani.

Ila tatizo unaweza ukabaki nyumbani ukaletelewa na hawa wanaokwenda mijini kutafuta mkate wa kila siku. It is complicated 😥.
 
Ukitoa total lockdown unashauri nini kifanyike?
 
Wawe wanataja kiwilaya ili.kujua wilaya IPI ina wagonjwa wengi ili hatua za kuchukua ziwe juu kwa wakazi Wa maeneo husika ya wilaya husika
 
Naamini huenda serikali iliamini kwamba kuwa na takwimu ndogo ya maambukizi ndio njia pekee ya kuuambia ulimwengu kwamba tanzania tuko vizuri kupambana na covid19

Kumbe sasa tafsiri imekuwa tofauti na matarajio yetu nadhani sasa tunaweza kuanza kuueleza ulimwengu kwamba tuna kasi ya maambukizi kubwa sana kuliko nchi zingine za afrika ya mashariki

Nadhani kwa rate hii na muendelezo huu na sisi tutaangaliwa kama wenzetu maana sasa tutaueleza ulimwengu kwamba nasisi tupo kwenye shida kuu
 
Hapa mjini dasalama ni shida sasa. Msongamano huu utamaliza wengi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
watu wa mikoani tujiandae kupokea ugeni muzito toka muji mukuu,hata wale waliowakana wazazi wao zamani sasa watarudi nyumbani kuomba misamaha,corona itawaleta watu karibu hatutasahau,tuchukue tahadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…