Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Kuna watu ni wajinga sana kwenye hii nchi, wanatia mpaka kichefuchefu
 
Halafu unaweza kushangaa huyu mlemavu wa akili naye ni sehemu ya serikali.
Haya yote kayataka Rais kupemda kusifiwa tu na kuteua, sasa amewafanya vijana na wapambe wa chama chake kuwa mazezeta na watumwa.
Kwa nchi inayoongozwa na watu wenye nia njema basi leo Musiba alitakiwa akalale central, jukumu la kutangaza watu hatari kwa usalama wa nchi sio la Musiba, ila jambo la kushangaza Amiri jeshi mkuu anaweza kumpongeza.
Musiba hatakiwi kuachwa aendelee kuyafanya haya, kama CCM wana akili zote basi wajue huyu kichaa anaharibu hata yale mahusiano madogo yaliyobaki kwa nchi kama America.
 
si alimpa siku 2 Tundu aombe msamaha la sivyo atamfungulia mashataka the Hague, sasa je keshafungua, naona kimya, mie naona anapoteza muda wa waandishi wetu
 
Hivi hiki anachofanya sio uchochezi?,,,vipi kama wangefanya upande wa pili, kesho si wangehitajika central?,,,,mwenzake murro aliongea wee lkn teuzi haikuwepo
 
nimeangalia youtube nimecheka sana,na waandishi wa habari muwe na akiri mnaitwa na kila mtu mnakwenda tu.shame on you.
 
Halaf FBI wanaweza kumuomba ushahidi huyu jamaa akaanza kutumbua macho. Halafu anavyoonekana hajielew, mwanzo anasema Mange anatumika na FBI then anasema hana kazi ni kahaba tu marekan sasa sijui akili yake kaisahau wap mpaka anafka kuongea na press.
 
Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
Du hii njaa sasa imekamata watu pabaya,hao FBI wakimtaka athibitishe madai yake anao ukweli?
Halafu hii ni dharau kwa mamlaka husika kwamba hazifanyi kazi ,ila yeye tu ndo anafanya kazi anatakiwa ahojiwe na ikibi ashitakiwe
 
amewatuhumu baadhi ya watu kuwa ni hatari kwa taifa mfano ni mbowe,mange kimambi,Maria sarungi,zitto,john Heche, na wengineo.
 
Waliomtuma wanaweza kumgeuka wakamteka wakamtesa na kumuua then ije ionekane CHADEMA kwenye maisha lazima uwe machale au akili.ya ziada

ajitafakari sana
maisha yako kasi sana
yuko wapi NAPE NNAUYE leo hii
yuko wapi RAMADHANI MAPURI

maishia hapo tu
 
WATU 10 AKIWEMO MANGE KIMAMBI WANAOTAJWA KUWA HATARI KWA USALAMA WA TAIFA
MTILAH BLOG / 42 minutes ago



MANGE KIMAMBI
Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba leo Februari 25, 2018 amezungumza na waandishi wa habarina na kuwataja watu 10 hatari kwa usalama wa Taifa.

Musiba amesema serikali inatakiwa kuwa makini na watu wao kwani wanaweza kusababisha machafuko nchini .Musiba amewataja watu hao ni.

1.Mange Kimambi-Musiba amesema mange kimambi anatumiwa na FBI(Shirika la kijesusi la marekani)

2.Freeman Mbowe-Musiba amesema CHADEMA imepeleka vijan 500 ujerumani kwa ajiri ya kuratibu ajenda za kiarifu katika Taifa

3.Mari Sarungi-Musiba amesema maria sarungi kazi yake ni kuongea negative juu ya serikali

4.Zitto kabwe-Musiba amesema Zitto anahamasisha vyama vya siasa viungane viandamane tyarehe 26/04/2018 ili walete vurugu.

5.Lissu

6.John Heche
7.John Marwa (Alikuwa mlinzi wa Salum mwalim wakati wa kampeni Kinondoni)
8.Evarist Chahari-Mtanzania anaishiu Uingereza


9.Julius Mtatiro
10.Janja wind-Kikundi cha wafuasi wa CUF


Cyprian Musiba ameiomba serikali na vyombo vya ulinzi kuwafuatilia watu hao

Zaidi msikilize kwenye video hii hapa chini
Kamsahau nabii tito
 
Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
Yaani anamtaja hadi Angela Markel...hivi balozi ya germany ikimwambia athibitishe atajibu nini
 
Huyu musiba na Jerry muro wana nafasi gani katika serikali hii mpaka Waite waandishi wa habari kuongelea masuala ya kitaifa au ni kujikomba kutafuta uteuzi
 
Huyu jamaa kweli hamnazo...hivi Chadema wanapata wapi pesa ya kupeleka vijana 500 wakapate mafunzo Ujerumani!?

Halafu kwa jinsi lilivyo tahira zaidi eti Mange anatumiwa na FBI,hivi hajui kama FBI inadili na Mambo ya usalama ndani ya Marekani pekee,Bora hata angesema CIA.

Halafu unawatuhumu hivyo FBI je serikali yao ikiomba uwape evidence wa hizo tuhuma zako uchwara,hapa tulipo tayari tuna mavikwazo bado waramba miguu ya Bashite wanataka kutuletea balaa lingine
Mkuu... Kwani waasi walitoa wapi silaha nzito nzito za kupambana na Gadaffi.... Ushaambiwa kuna wafadhili! Inawezekana pia Fbi na cia, maana wao ni kwa maslahi ya usa.
 
Kwanini tusijadili hoja... Vipi kama ni kweli hawa watu wanatumika? Au ndio watu 500wamejaaa humu JF kupinga kwa nguvu zote
 
Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
Maria Sarungi ameingiaje humo tena dada yangu huyu!!!!!??[emoji15][emoji15][emoji32][emoji32][emoji32][emoji33][emoji33][emoji33][emoji30][emoji30][emoji34][emoji34][emoji34][emoji20][emoji20][emoji20][emoji20]
 
Back
Top Bottom