Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

CIA ni Shirika la kijasusi la marekan, na mara nyingi linafanya shughuli zake nje ya mipaka ya marekani kwa masirahi ya marekeni, Kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, na FBI ni shirika la upelelezi la marekani.
upelelezi maana yake ni nini ?

utakuwaje mpelelezi bila kuwa jasusi?
 
WATU 10 AKIWEMO MANGE KIMAMBI WANAOTAJWA KUWA HATARI KWA USALAMA WA TAIFA
MTILAH BLOG / 42 minutes ago



MANGE KIMAMBI
Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba leo Februari 25, 2018 amezungumza na waandishi wa habarina na kuwataja watu 10 hatari kwa usalama wa Taifa.

Musiba amesema serikali inatakiwa kuwa makini na watu wao kwani wanaweza kusababisha machafuko nchini .Musiba amewataja watu hao ni.

1.Mange Kimambi-Musiba amesema mange kimambi anatumiwa na FBI(Shirika la kijesusi la marekani)

2.Freeman Mbowe-Musiba amesema CHADEMA imepeleka vijan 500 ujerumani kwa ajiri ya kuratibu ajenda za kiarifu katika Taifa

3.Mari Sarungi-Musiba amesema maria sarungi kazi yake ni kuongea negative juu ya serikali

4.Zitto kabwe-Musiba amesema Zitto anahamasisha vyama vya siasa viungane viandamane tyarehe 26/04/2018 ili walete vurugu.

5.Lissu

6.John Heche
7.John Marwa (Alikuwa mlinzi wa Salum mwalim wakati wa kampeni Kinondoni)
8.Evarist Chahari-Mtanzania anaishiu Uingereza


9.Julius Mtatiro
10.Janja wind-Kikundi cha wafuasi wa CUF
>>>BOFYA HAPA ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU


Cyprian Musiba ameiomba serikali na vyombo vya ulinzi kuwafuatilia watu hao

Zaidi msikilize kwenye video hii hapa chini


Visit website
Huyu anapaswq kushitakiwa ili athibitishe huu upuuzi wake hapo mpema kesho
 
Mbona chama cha wasiojulika sjaona mtu wake apo au tuzid kuwaombea?
 
Ile kesi dhidi ya Lissu ameahirisha??
 
Nimelazimika kuangalia hii video.

Kwanza nimecheka sana. Siwezi kumbishia Bwana Msiba maana anaweza kua na sababu zake hata kama ni za kipumbavu ila bado anaziamini kua ni sababu.

Nilichogundua elimu ndogo na uelewa mdogo bado ni changamoto katika jamii yetu, kama huyu alikua mtangazaji na mwandishi wa ha ari basi hii nchi ina matatizo makubwa.

Kwanza Musiba anaonekana hajui au hana ufaham kabisa tofauti kati ya FBI na CIA. Anaituhumu FBI lakini kimantini ni CIA kama kweli anachokisema kiko hivyo, FBI haifanyi kazi za ujasusi na haivuki mipaka ya Marekani, hawa ni polisi wa Marekani na sio taasisi ya kijajusi nje ya Marekani.

Pili, Musiba hata maneno ya kawaida tu yanamshida kuyasarufisha, Uasi yeye anasema ni Uhasi.

Little learning is very hazardous. Stupidity is still common among Tanzanias.
Comment yako imenifanya nami niifungue hiyo clip! Nikavutiwa zaidi na utangulizi wake:
"Napenda kuitangazaia dunia na Afrika watu hatari "
Ajabu anataja watu ambao hata afrika mashariki tu hawafahamiki..!
Anyway, sijui suala la diplomasia limekaaje!
 
Huyo MSIBA Kafanyeje?Naomba pia Kuuliza.Ndio Yule aliyekuaga MAGIC FM Michezo?Maana kuna Mijitu Inajitokeza Kipindi hiki kwa Kasi ya Hatari.Halafu Nyuma yana Makandokando Chungu Nzima
Huyo huyo!!
 
MTU hatari zaidi ni Musiba,
Huyu anahamasisha binadamu wenzake wang'olewe kucha ni kati ya wapuuzi wachache wanaofurahia wenzao wakipata matatizo,
Watu hawa Mungu huwageuzia kibao hapa hapa dunian.
 
Zee La Kujipendekeza Hilo, Bashite Usilipe Hata Mia Litaacha Lenyewe Kujikomba Komba
 
Kuchambua UEFA tu enzi zile Channel 10 ilikuwa kila kitu anasema 'kama alivyosema Dr'.

Kwani anaishi wapi maana njaa yake ni kali sana inaonekana.
 
Huyu jamaa kweli hamnazo...hivi Chadema wanapata wapi pesa ya kupeleka vijana 500 wakapate mafunzo Ujerumani!?

Halafu kwa jinsi lilivyo tahira zaidi eti Mange anatumiwa na FBI,hivi hajui kama FBI inadili na Mambo ya usalama ndani ya Marekani pekee,Bora hata angesema CIA.

Halafu unawatuhumu hivyo FBI je serikali yao ikiomba uwape evidence wa hizo tuhuma zako uchwara,hapa tulipo tayari tuna mavikwazo bado waramba miguu ya Bashite wanataka kutuletea balaa lingine
 
Watu kama hawa n wakuchuliwa hatua,pale serikali husika iliyotajwa kuchukua hatua wakongo usemaga utayamba mpepo
 
Ccm kweli wameishiwa!propaganda gani za kijinga namna hii!
 
Huyu mtu ukimuangalia vizuri ni kama katumwa...katumwa na nani sijui, kwanini nasema katumwa anavyoviongea hata ye mwenyewe anaonekana havijui kwasababu ama anavikosea ama anavichanganya, kutaja majina tu imekuwa tabu, chama cha CDU yeye anasema kirefu chake ni christian democraticy pary(uwongo mkubwa) jina la mange kimambi ndilo anaonekana ana hasila nalo kwasababu ndo kalitolea ufafanuzi mrefu kuliko majina yote, kashidwa kuwatofautisha kati ya john marwa na john heche...hapo hajajua yupi ni yupi..
 
Back
Top Bottom