Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Askofu Mwamakula ndio aliyetumwa na mtu huyu akamuombee radhi kwa Membe.

Askofu huyu sijui alikuwa upande gani wakati wa "utawala" wa mtu huyu. Askofu Mwamakula sijui alikuwa wapi mtu huyu alipokamatwa akiwa na silaha kali akiambatana na kundi la "wasiojulikana" kilometa chache kabla ya kijiji cha Membe.

Membe alipigana vita pekeyake na familia yake huku jamaa na rafiki zake wakimtenga kwa kuhofia maisha yao dhidi ya wasiojulikana. Hata huko upinzani ambako Membe alihamishia vita yake dhidi ya "Goliath" ambako Askofu Mwamakula yupo, Askofu huyu hakusimama na Membe katika vita yake dhidi ya utawala wa mwendakwake. Badala yake alishauri Membe avunje sheria ya uchaguzi ajiondoe ugombea.

Yaani tuna tuna askofu anayeshauri uvunjwaji wa sheria. Huyu hana moral authority ya kushauri kwenye suala hili maana amekuwa so biased from the word go.

Nafurahi kuona Membe anakaza uzi, hajawahi kurudi nyuma, hatetereki, na yupo tayari kulinda heshima na Uhuru wa mahakama yetu.

Tunaofurahia uamuzi wa mahakama tunaona umuhimu wa kesi hii katika mambo makubwa matatu. Moja, umuhimu wakuiamini mahakama yetu katika kutoa na kusimamka haki. Wengi kwa woga walishauri Membe asipeleke kesi mahakamani wakishindwa kuona na kuamini Uhuru wa mahakama. Kesi hii sasa inafundisha kwamba haki bado ipo mahakamani. Pili, kesi hii inafundisha vijana wanasiasa kuacha kutumika Kama disposable plates au mbwa wa kuwindia. Wapo wanaosema mtu huyu alitumwa na mwendakwake, wapo sahihi lakini wengine wengi walitumwa lakini hawakufanya kwa kiasi alichofanya mtu huyu. Kesi hii inatukumbusha msemo wa JK unaotutaka kila wakati tuchanganye na za kwetu. Tatu, kesi hii inatufundisha na kutukumbusha ufundi na ukuu wa Mungu aliye hai. Yaani Mungu wetu sote. Kupitia kesi hii mtu huyu aliyedhani mungu wake angeishi milele huko Chato na kwamba adui zake walistahili kifo na umaskini leo anakumbushwa uwapo wa the grand power. Basi kusitokee mtu anayejiita askofu akataka ku downplay mafundisho haya matatu.
 
Anazo muache alipe tu, haina shida.
 
Hivi huyo Jamaa alipotelea wapi? Hivi yupo kweli? Alisema Risasi alizopigwa Lissu ni "Branco".
 
Chokochoko kazianza zamani sana huyu, acha apambane na hali yake.
 
Wanakikundi wenzie wanamtelekeza hivi hivi, dah, mchangieni mwenzenu kuweni na upendo japo kidogo, na wale wa dada wa f/b aka #veronica, jitokezeni kuchanga japo million 100,kila mmoja maana mzigo ni mkubwa huu.
 
Hajafunguliwa mashitaka sio kwamba ni innocent ila bado analindwa na hii serikali haramu ambayo haina ridhaa ya wananchi.

Siku zinakuja huyo mjinga lazima atanyea tu debe kwani amefanya uovu mwingi sana ikiwa ni pamoja na kuunda genge la wasiojulikana ili kuua vichomi wa dikteta Magufuli. Bure kabisa.
 
Kama ni hivyo, ujue kuwa hawakuhuzunika kwa sababu ya kifo cha marehemu bali walihuzunishwa na kukoma kwa maisha yao waliyokuwa wamezoea.

Kwa hali ya kawaida, huzuni ya jirani haiwezi kuizidi huzuni ya wanafamilia.
Upo sahihi , ilikuwa ni huzuni kuhusu hatma za nyadhifa zao
 

Tatizo akitoroka atazidi kujiharibia. Pia ujue anaye mdai ni kachero hivyo anamfuatilia kwa ukaribu Sana, akitoroka tu , watamnyaka mapema.
 

Tatizo musiba alidharau mahakama. Hata Kama angeshindwa kesi kiasi kisingekuwa kikubwa kiasi kile.
 
Tatizo akitoroka atazidi kujiharibia. Pia ujue anaye mdai ni kachero hivyo anamfuatilia kwa ukaribu Sana, akitoroka tu , watamnyaka mapema.
Potelea pote , atimue mbio tu , naye Membe ni binadamu anaweza kumsamehe akiona mpaka ameamua kukimbia .

Ila namuonea huruma huyu bwana maana hata asipolipa simuoni kuishi kwa amani maana vitisho nje nje .
 
Ana Mali equivalent to that amount?

Watachukua Mali zake zote na kupingwa mnada na Madalali wa mahakama, Kama kiasi hakitoshi Basi, atatawekwa kizuizini mpaka pesa yote ilipwe. Nadhani Membe shida yake sio hiyo pesa bali anahitaji jamaa akae ndani hata Mwezi mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…