Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Mahakama Kuu ya Tanzania imempa siku 14 za kazi mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wenzake watatu kumlipa Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu, Benard Membe TZS bilioni 9.92 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vya habari.

View attachment 2588944

Mahakama imetahadharisha deni hilo lilipwe ndani ya muda vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.
Askofu Mwamakula ndio aliyetumwa na mtu huyu akamuombee radhi kwa Membe.

Askofu huyu sijui alikuwa upande gani wakati wa "utawala" wa mtu huyu. Askofu Mwamakula sijui alikuwa wapi mtu huyu alipokamatwa akiwa na silaha kali akiambatana na kundi la "wasiojulikana" kilometa chache kabla ya kijiji cha Membe.

Membe alipigana vita pekeyake na familia yake huku jamaa na rafiki zake wakimtenga kwa kuhofia maisha yao dhidi ya wasiojulikana. Hata huko upinzani ambako Membe alihamishia vita yake dhidi ya "Goliath" ambako Askofu Mwamakula yupo, Askofu huyu hakusimama na Membe katika vita yake dhidi ya utawala wa mwendakwake. Badala yake alishauri Membe avunje sheria ya uchaguzi ajiondoe ugombea.

Yaani tuna tuna askofu anayeshauri uvunjwaji wa sheria. Huyu hana moral authority ya kushauri kwenye suala hili maana amekuwa so biased from the word go.

Nafurahi kuona Membe anakaza uzi, hajawahi kurudi nyuma, hatetereki, na yupo tayari kulinda heshima na Uhuru wa mahakama yetu.

Tunaofurahia uamuzi wa mahakama tunaona umuhimu wa kesi hii katika mambo makubwa matatu. Moja, umuhimu wakuiamini mahakama yetu katika kutoa na kusimamka haki. Wengi kwa woga walishauri Membe asipeleke kesi mahakamani wakishindwa kuona na kuamini Uhuru wa mahakama. Kesi hii sasa inafundisha kwamba haki bado ipo mahakamani. Pili, kesi hii inafundisha vijana wanasiasa kuacha kutumika Kama disposable plates au mbwa wa kuwindia. Wapo wanaosema mtu huyu alitumwa na mwendakwake, wapo sahihi lakini wengine wengi walitumwa lakini hawakufanya kwa kiasi alichofanya mtu huyu. Kesi hii inatukumbusha msemo wa JK unaotutaka kila wakati tuchanganye na za kwetu. Tatu, kesi hii inatufundisha na kutukumbusha ufundi na ukuu wa Mungu aliye hai. Yaani Mungu wetu sote. Kupitia kesi hii mtu huyu aliyedhani mungu wake angeishi milele huko Chato na kwamba adui zake walistahili kifo na umaskini leo anakumbushwa uwapo wa the grand power. Basi kusitokee mtu anayejiita askofu akataka ku downplay mafundisho haya matatu.
 
Ni matatizo yake ya kujitakia Musiba kutotafuta mwanasheria wa kujitetea na kudharau mahakama, ata kama imetumika vibaya.

Ukisikiliza maelezo ya decision kwenye kesi ya defamation aliyofungua Nehemia kuna justification ya award alizopewa on loss of business, other income na kupeteza trustworthiness kama mfanyabiashara vitu alivyoelezea mahakamani. Sasa kama kweli alikuwa na huo ushahidi wa MoU wa hasara alizodai kupoteza ni swala lingine. Ila decision ina justification kwa kesi aliyofungua.

Mahakama aiwezi jiropokea tu umlipe mtu kiasi gani cha fidia, inatakiwa kuwe na ushahidi wa loss of income za kibiashara au kwa ma celebrities ni damage ya brand zao ambazo ndio msingi wa kupata kazi na hela.

Sasa ata kama kweli Musiba alimchafua Membe kuna justification gani ya kumlipa damages za tsh 9 billion, hizo hasara Membe alizopata ni zipi zenye kufikia hiyo thamani au Membe ni brand yenye thamani ipi kama superstar.

Ni decision ya uonevu kwa Musiba, ila ujinga zaidi ni yeye kudharau mahakama toka anaitwa na kukaa kimya ata decision ilipotolewa; huko sasa ndio kujitakia.
Anazo muache alipe tu, haina shida.
 
Magazeti yake yalikua yanawatuhumu watu kwa ushoga, nakumbuka kuna jarida moja aliandika kwa herufi kubwa,"SHOGA AWACHANGANYA MAALIM SEIF NA ZITTO ",Halafu katikati ya picha ya maalim Seif na Zitto akaweka picha ya Sufian eti ndio gasho mwenyewe[emoji2][emoji2]
Chokochoko kazianza zamani sana huyu, acha apambane na hali yake.
 
Wanakikundi wenzie wanamtelekeza hivi hivi, dah, mchangieni mwenzenu kuweni na upendo japo kidogo, na wale wa dada wa f/b aka #veronica, jitokezeni kuchanga japo million 100,kila mmoja maana mzigo ni mkubwa huu.
 
HIzi story za Makonda afungwe afungwe kwa kosa gani? Makonda anadunda tu mtaani. Na alifungwa Mbowe, Makonda hajawahi kaa hata mahabusu. Nyie mliaminisha umma kuwa Makonda ana makosa mengi sana. Kumbe wala si kweli. Mpaka leo miaka miwili toka Magufuli afariki Makonda hajafunguliwa kesi yoyote ile.
Hajafunguliwa mashitaka sio kwamba ni innocent ila bado analindwa na hii serikali haramu ambayo haina ridhaa ya wananchi.

Siku zinakuja huyo mjinga lazima atanyea tu debe kwani amefanya uovu mwingi sana ikiwa ni pamoja na kuunda genge la wasiojulikana ili kuua vichomi wa dikteta Magufuli. Bure kabisa.
 
Kama ni hivyo, ujue kuwa hawakuhuzunika kwa sababu ya kifo cha marehemu bali walihuzunishwa na kukoma kwa maisha yao waliyokuwa wamezoea.

Kwa hali ya kawaida, huzuni ya jirani haiwezi kuizidi huzuni ya wanafamilia.
Upo sahihi , ilikuwa ni huzuni kuhusu hatma za nyadhifa zao
 
Kwani pale Mutukula kwenye hii njia kama ya kwenda Izimbya hapapenyeki kuingia Uganda ?

Vipi Tunduma kwa kupitia hii njia ya kwa Mpemba nyuma ya stendi hapatupeleki Zambia?

Vipi Silari vijana wavushaji hawapo tena ili tufike Kenya ?

Ngoja kwanza kwani Kasumbalesa nyuma ya Kingdon bar hatuwezi kupita huko kufika Congo ?

Hapana Kirando tukifika kwa mtumbwi Congo ile pale no Visa no what

Kigoma pale hivi njia za nyuma huku Burundi hakuingiliki tena ?

Ngoja kwanza kwani Karagwe huko ndani kule Nkwenda zile njia za kuingia Rwanda zimejulikana tayari ?

Kwani vipi wazee wa fleeboat hapa uwanja wa Mwalimu Julius hawapo tena ? Hapana wapo mbona nasikia ni hela yako Vitengo wanakufikisha nje ya mipaka ?

Yaani haya yote nayawaza kabla ya siku 14 za Msiba mbona ni njia rahisi yeye kutokomea .

Labda ana hela ngoja niendelee kuhesabu siku alizopewa .

Tatizo akitoroka atazidi kujiharibia. Pia ujue anaye mdai ni kachero hivyo anamfuatilia kwa ukaribu Sana, akitoroka tu , watamnyaka mapema.
 
Ni matatizo yake ya kujitakia Musiba kutotafuta mwanasheria wa kujitetea na kudharau mahakama, ata kama imetumika vibaya.

Ukisikiliza maelezo ya decision kwenye kesi ya defamation aliyofungua Nehemia kuna justification ya award alizopewa on loss of business, other income na kupeteza trustworthiness kama mfanyabiashara vitu alivyoelezea mahakamani. Sasa kama kweli alikuwa na huo ushahidi wa MoU wa hasara alizodai kupoteza ni swala lingine. Ila decision ina justification kwa kesi aliyofungua.

Mahakama aiwezi jiropokea tu umlipe mtu kiasi gani cha fidia, inatakiwa kuwe na ushahidi wa loss of income za kibiashara au kwa ma celebrities ni damage ya brand zao ambazo ndio msingi wa kupata kazi na hela.

Sasa ata kama kweli Musiba alimchafua Membe kuna justification gani ya kumlipa damages za tsh 9 billion, hizo hasara Membe alizopata ni zipi zenye kufikia hiyo thamani au Membe ni brand yenye thamani ipi kama superstar.

Ni decision ya uonevu kwa Musiba, ila ujinga zaidi ni yeye kudharau mahakama toka anaitwa na kukaa kimya ata decision ilipotolewa; huko sasa ndio kujitakia.

Tatizo musiba alidharau mahakama. Hata Kama angeshindwa kesi kiasi kisingekuwa kikubwa kiasi kile.
 
Tatizo akitoroka atazidi kujiharibia. Pia ujue anaye mdai ni kachero hivyo anamfuatilia kwa ukaribu Sana, akitoroka tu , watamnyaka mapema.
Potelea pote , atimue mbio tu , naye Membe ni binadamu anaweza kumsamehe akiona mpaka ameamua kukimbia .

Ila namuonea huruma huyu bwana maana hata asipolipa simuoni kuishi kwa amani maana vitisho nje nje .
 
Ana Mali equivalent to that amount?

Watachukua Mali zake zote na kupingwa mnada na Madalali wa mahakama, Kama kiasi hakitoshi Basi, atatawekwa kizuizini mpaka pesa yote ilipwe. Nadhani Membe shida yake sio hiyo pesa bali anahitaji jamaa akae ndani hata Mwezi mmoja.
 
Back
Top Bottom