Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Kwaiyo unafurahi ujenzi kutokamilika kwa wakati, kwani hata usipokamilika we unapata faida gani?kwanza inabidi tumpongeze Magufuli kwa uthubutu pamoja na mdororo wa uchumi kwasababu ya corona, serikali ya Magufuli bado wanaendelea na miladi yote,nchi nyingi miladi mikubwa wamesimamisha, mpaka wanafikia kupunguza wafanyakazi.Maguri ni mwanaume wa shoka.
Hiyo kitu haipo na haija tuathiri,ipo kwa jirani zetu.
 
Hiyo reli ya Mpanda Hadi DRC itapitia wapi mkuu ?
Nadhani Kalemi, kwenye mwambao ya Ziwa Tanganyika, halafu inabebwa na meli hadi upande wa pili wa DRC unaoitwa Kalemie port. Baadaye sgr ya umeme itajengwa kutoka Tabora hadi kule Kalemi. Lengo ni kuiunganisha nchi yetu na utajiri mkubwa wa maliasili wa nchi ya DRC. Pale Kalemi upande wa Tanzania kutakuwa na soko kubwa la kimataifa la madini mbali mbali.
 
Kilichokupa utata kuelewa ni nini? Maana sio mtalaamu sana wa civil works. Lakini ana uzoefu wa kazi za za kikandarasi. Hapo umeshindwa kuelewa nini? gt au...
Atakuwa hataki upekenyue mapungufu hata haliyo wazi kwa wasio wataalamu,angehoji zaidi huenda ungemfahamisha asichoelewa.
 
Kwa jibu hili ulilopost ni dhahiri kuwe wewe uelewa wako ni duni. Sgr au narrow gauge zote zinatengenezwa kwa kujenga tuta kisha kutandaza reli. Kaa kimya maana unajiabisha.
Aache kukushambulia akitaka aje na utafiti wake hapa,vinginevyo anafanya utetezi kwa wengine usiokuwa na tija kwa taifa.
 
Hata usipokamilika ndani ya muda wake sisi hatuna shida watakuja kufaidi wajukuu zetu kwani shida iko wapi?Marekani anapanga mipango ya miaka 50 namna nchi yao itakuwaje sembuse sisi?
Sio kwa kukurupuka kibongobongo hata Bila mikakati inayoeleweka.
 
Bandugu sehemu pekee ya kuambiana ukweli hapa Tanzania imebaki Jf maana sioni gazeti, radio au Tv ambayo inaweza kujilipua na kusema ukweli au kutoa wazo lenye mantiki ya ukweli ili kuiambia ukweli serikali yetu.

Mfano ni dhahiri kuwa ujenzi wa Sgr toka Dar to Morogoro ulipangwa kukamilika 2019 na kipande hiki kina umbali wa km 202. Lakini leo hii tupo mwaka 2021 lakini nimezungumza na wadau ambao wapo site wanasema huu mwaka hawawezi kukamilisha.

Mmmoja wa wadau alie site japo kuwa sio mtaalamu sana wa civil works ila kwa uzoefu wake ameniambia kuwa kampuni ya Yapi merkez wapo slow katika kuchapa kazi. Maana anasema amefanya kazi za ujenzi kwa muda mrefu na haoni ugumu wa ujenzi wa reli maana kazi kubwa ni kujaza tuta na kisha kutandaza reli.

Kwa hiyo kukata udongo na kujaza tuta sio kazi ya kuchukua miaka minne,japokuwa kuna ujenzi wa madaraja,vituo na miundo mbinu ya umeme. Bora hii tenda wangepewa wachina tangu awali hizo km 202 zingekamilika.

Kuambia watu kuwa tutamilisha ujenzi wa Sgr ndani ya miaka 5 iliyobaki ya utawala wa JPM ni ndoto za mchana. Maana kwa kasi hii ya kampuni ya Yapi merkez ni kujidanganya kuwa vipande vya Makutupora to Moro,Dom to Tabora na Tabora to Isaka vitakamilika kwa wakati.

Inashangaza kwa nini PM Majaliwa haoni aibu kila mara kutuambia kuwa tupo karibu kuanza kupanda treni ya umeme wakati kiuhalisia bado sana.
Tatizo ukomo....
 
Nadhani Kalemi, kwenye mwambao ya Ziwa Tanganyika, halafu inabebwa na meli hadi upande wa pili wa DRC unaoitwa Kalemie port. Baadaye sgr ya umeme itajengwa kutoka Tabora hadi kule Kalemi. Lengo ni kuiunganisha nchi yetu na utajiri mkubwa wa maliasili wa nchi ya DRC. Pale Kalemi upande wa Tanzania kutakuwa na soko kubwa la kimataifa la madini mbali mbali.

Mawazo haya wana psychology wanaita intuition sawa na kupiga ramli au kufuata hisia yaani kurahishisha mambo bila kutumia juhudi za kujiuliza kwa kuhusisha kutumia fikra na bongo kujiuliza tunavyoona na kufikiri ndivyo au tunarahishisha kuwa DR Congo, Rwanda, Burundi lazima watatumia SGR reli yetu watake wasitake.

Inabidi tuende mbele na kujiuliza kwa juhudi kabisa/ effort wanavyosema wana-psychology kuhusisha mawazo, fikra, mdahalo kama huu hapa JF na bongo zetu bila kutumia mahaba ya kumpenda kiongozi/ chama kutumia "kuotea/intuition/ ramli".

Yaani tufanye juhudi / effort za makusudi kabisa kuachana na mtindo huu uliojitokeza sasa ktk mitano-mingine kutumia kuotea/kuamini na kuaamua kujiuliza tena na tena kweli SGR itegemee maamuzi ya jirani au wenyewe tujipange reli yetu 60% itegemee shughuli za kiuchumi za ndani ya nchi ndiyo ziendeshe kujenga mradi huu au la na kwa kiwango gani na wapi reli hii iende ndani ya nchi yetu.

Dunia hii ni chaotic / uwanja-wa-fujo kwa nchi yoyote ikiwemo Tanzania kutegemea kupitia intuition / maoteo bila kutumia fikra gonganishi ktk bongo kuamini majirani wa DR Congo, Rwanda , Uganda wataibeba SGR reli yetu na huku tunajua fika kuwa hatuwezi kuwalazimisha au kuwashawishi waitumie kwa miezi sita, mwaka au milele reli yetu.
Daniel Kahneman is an internationally renowned psychologist whose work spans cognitive psychology, behavioral economics, and the science of well-being. In recognition of his groundbreaking work on human judgment and decision-making, Kahneman received the 2002 Nobel Prize.

Explorations of the Mind: Intuition with Daniel Kahneman

Source : University of California Television (UCTV)
 
Report ya mwezi DEC hawajaweka Yapi ndio nakwambia vimebaki vipande vidogo vidogo ndio wanamalizia nimekuorozeshea. Wanaonyesha njia zima toka Dar to Moro wanarekodi kwa drone.Sasa unataka majaribio wakati hawajamaliza.Tupende vya kwetu hata kama kuna upungufu kidogo.Suala la kuchelewa kumaliza lilitolewa ufafanuzi ni sababu ya mvua nyingi zilizonyesha 2019 mwishoni mpaka 2020 April zilichangia pia
Kupenda vyetu,siishida shida nikutoambiwa hatauhalisia wachangamoto tulizonazo,kwa uhalisia,hata tusingekuwa tunazozana humu.
 
Ni kweli hauwezi kukamilika kwa wakati lakini Rais ajae lazima akamilishe maana itakua imebaki vipande vidogo sana,
Katika hili nipo pamoja na JPM
 
Uchambuzi wako hauna facts,na bahati umeeleza kuwa wewe sio mtaalamu,sasa kumbuka huo ni ujwnzi wa reli ya mwendo kasi,una yjenzi tofauti na reli ya kawaida,pia hiyo kampuni ni kampuni kubwa sana na imwjenga reli kuliko hiyo huki kwao uturuki,nenda kaone waluvyojenga instambul
Nimefika Istanbul, SGR yao walijengewa na Wachina na fedha walikopa Chinese Exim Bank
 
Bandugu sehemu pekee ya kuambiana ukweli hapa Tanzania imebaki Jf maana sioni gazeti, radio au Tv ambayo inaweza kujilipua na kusema ukweli au kutoa wazo lenye mantiki ya ukweli ili kuiambia ukweli serikali yetu.

Mfano ni dhahiri kuwa ujenzi wa Sgr toka Dar to Morogoro ulipangwa kukamilika 2019 na kipande hiki kina umbali wa km 202. Lakini leo hii tupo mwaka 2021 lakini nimezungumza na wadau ambao wapo site wanasema huu mwaka hawawezi kukamilisha.

Mmmoja wa wadau alie site japo kuwa sio mtaalamu sana wa civil works ila kwa uzoefu wake ameniambia kuwa kampuni ya Yapi merkez wapo slow katika kuchapa kazi. Maana anasema amefanya kazi za ujenzi kwa muda mrefu na haoni ugumu wa ujenzi wa reli maana kazi kubwa ni kujaza tuta na kisha kutandaza reli.

Kwa hiyo kukata udongo na kujaza tuta sio kazi ya kuchukua miaka minne,japokuwa kuna ujenzi wa madaraja,vituo na miundo mbinu ya umeme. Bora hii tenda wangepewa wachina tangu awali hizo km 202 zingekamilika.

Kuambia watu kuwa tutamilisha ujenzi wa Sgr ndani ya miaka 5 iliyobaki ya utawala wa JPM ni ndoto za mchana. Maana kwa kasi hii ya kampuni ya Yapi merkez ni kujidanganya kuwa vipande vya Makutupora to Moro,Dom to Tabora na Tabora to Isaka vitakamilika kwa wakati.

Inashangaza kwa nini PM Majaliwa haoni aibu kila mara kutuambia kuwa tupo karibu kuanza kupanda treni ya umeme wakati kiuhalisia bado sana.
HII SASA INAASHIRIA KUWA LAZIMA AONGEZWE MIAKA ILI MIRADI YAKE IKAMILIKE.MPENDE MSIPENDE[emoji41]
 
Aliyekwambia SGR inafika Tabora ndani ya awamu ya 5 ya miaka 10 nani?
SGR ndani ya awamu ya 5 inaishia Makutupora tu.
Ndio maana tunataka tumwongezee muda ili SGR ifike huko Tabora mpaka Isaka.
Umeelewa?
Siyo lazima amalizie yeye. Atakuja mwingine atamalizia kama jinsi yeye alivyomalizia Terminal III na Daraja la Nyerere la Kigamboni
 
Wewe mbweha kavute Bangi huna unachokijua zaidi ya chuki fitna za kishamba pasipo kujua kuwa Serikali ndiyo Tatizo kwenye malipo, tumeshakuja kuwa una masilahi yako huko ndiyo maana umeanza fitna za kishetani
Mbona tumekuwa tunaenda vizurj mnataka kuharibu hapa Bandugu,imekuwaje mnagombania fito,Tz ni moja nasi ni wamoja.
 
hakuna cha slow. pesa hakuna. na wafadhili mnawadhihaki na kuwakashifu kwa kuwaita mabeberu. mko against na dunia kuhusu korona afu mnataka kufanikisha miradi ya kiwango cha dunia? hata akiichezea Katiba kwa kuondoa ukomo hilo limradi halifanikiwi.

mnawataka wachina mtayaweza masharti yao au mnawachukulia poa?
Huu ndiyo ukweli halisi kabsa
 
Back
Top Bottom