Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Umeongelea kampuni tu ila logistic issues na political motives ujaziongelea, kumbuka muheshimia anapenda sana kutumia hiyo miradi kujinadi nakuomba aongezewe mda wa utawala wake ili akamirishe yote, kwahiyo usishangae kama kila kitu kimepangwa......
 
Ukitaka facts nenda site kashuhudie unachoona kwenye Tv kama ni kweli.

Kama ni kampuni mahili,cut and fill kisha kutandaza reli ndio ichukue miaka minne km 202?
 
Kwa kampuni kama Yapi merkezi hata akiongezewa muda haitakamilika.

Tatizo sio kampuni bali ni fedha. Mwanzo JK alikuwa ameshakubaliana mkopo wa ujenzi wa huo ujenzi na bank ya exim bank ya China ya $7.6b, kwa masharti ya kampuni ya ujenzi iwe ni toka China. Ilibaki hatua ya utekelezaji. Alipoingia mzalendo academia akaja na hadithi kiwa huo Mkata uko overestimated, ila yeye ataujenga kwa fedha za ndani, na ujenzi akampa huyo mturuki. Mpaka sasa ameshakopa zaidi ya $2b na mradi bado unasuasua, na dalili zinaonesha bei itakuwa juu kuliko aliyoikataa mwanzo. Ninadhani motive ya kukataa mkataba wa mwanzo asingepata 10%, ndio maana akaanza makubaliano mapya ambayo atapata 10%.
 
Na walivyotangaza nia ya safar dar to moro walijifikiria nin
 
Kama flow ya malipo haiko vizuri watawezaje kukimbiza Ujenzi??

Kumbuka Serikali ina miradi mikubwa miwili ya ujenzi wa bwawa la Umeme na hiyo sgr, kwahiyo wasiwasi wangu ni hiyo flow ya malipo kama inafanyika kwa wakati.

Sisi huku kwenye miradi midogo dogo ni kawaida kusubirishwa malipo kwa miezi 8 hadi 14 na zaidi

Tena unakuta unadai pengine milioni 400 tu lakini unatakiwa kusubiri muda wote huo, sembuse hizo sgr zenye gharama za matrilioni?
 
Huu mradi umeliingizia hasara kubwa Sana Taifa , umeblock ajira za vijana wengi Sana ili fedha zipelekwe kutimiza malengo ya ukurupukaji ya mtu fulan ,....!!! Hii nchi Mungu aihurimie tuu...
Huwez kukamilisha mradi kama huu Kwa kuunga unga hvi....
 
Hahahaa! Wanapangwa graduate kuanzia Dar hadi Igoma
 
Kwa kampuni kama Yapi merkezi hata akiongezewa muda haitakamilika.
Tusiwalaumu sana kwani hatuwezijua kama makubaliano kwenye mkataba Serikali inatekeleza. Malipo ya awali tunalipa kwa kiwango kile kile tulichokubaliana? Na je kwa wakati?

Nimewaza hivyo kwani sisi ni mabingwa wa kukiuka utaratibu tuliokubaliana. Kama Bunge ndiyo chombo cha kutunga Sheria lkn ndiyo Chombo cha kwanza kuvunja unategemea nn??
 
Huyu mbunge wa kideng’embe mkoani mjombe nafikiria, nilikuwa huko mwaka 2012 jamaa alikuwa ajui kusoma kabisa yani so tulipata tenda ya kumfundisha ili ajue kusoma.
Oops!! Na kwa bahati mbaya kielimu hicho ndio kigezo cha chini cha kuwa mbunge kwa nchi yetu (kujua kusoma na kuandika).

Asante kwa taarifa, kama mwaka 2012 alikuwa anajifunza kusoma, kwa mwaka huu kuwa na mitazamo ile aliyonayo sio bahati mbaya.
 
This week wamesema imekamilika kwa zaidi ya 90%, hebu nenda kaangalie kama ni kweli maana wabongo huwa wabishi mno.

Hilo neno la miradi kukamilika zaidi ya 85% ni kama wamelishana watendaji wote wa serikali hii. Jaribu kusikiliza ni kama kauli mbiu, ni nadra sana kusikia mradi uko chini ya 75%. Hicho kipande cha Dar-Moro kilikuwa kifunguliwe Novemba 2019, kila siku toka hiyo 2019 hadithi ilikuwa ujenzi umefikia zaidi ya 75%. Haya makodi yanayotozwa ya kukomoa ni ili kukamilisha hiyo miradi kwa shuruti.
 
Yapi wanafanyakazi kitaalamu na kuchunga ubora.Sio kuripua ripua kama wanavyofanya wachina.Nenda kwao Uturuki ukaone mareli na madaraja waliyojenga.Tukiwashinikiza watafanya haraka halafu madaraja yaporomoke mapema.
Tanzania sio nchi pekee au ya kwanza kufanya mradi wa SGR.

Kwa maneno yao wenyewe walisema itakamilika kwa muda fulani na hiyo ni baada ya feasibility study, wanachohoji wananzengo hapa ni uhalisia wa muda wa kukamilika na hatua tuliyopo sasa.

Na kuna vipande ambavyo so far bado hata havina mfadhili achilia mbali kuanza kazi ambavyo kimsingi ni virefu kuliko kinachoendelea na ujenzi.
 
Hzi akili hzi , kazi kwel kwel...ukurupukaji wa jiwe unaita uanaume .... Hyo hela si Bora ingepelekwa kuboresha sekta ya Afya ambayo ipo taabani na inakula maisha ya watz Kwa Kasi ya 4G , unasifia SGR ambayo kiuhalisia ni hallucination Tu Kwa nchi kama bongo ,....
 
Hii nchi imejaa wasomi waoga hawawezi kumwambia ukweli mkuu.
Mkuu huyu hambiliki. Unakumbuka wakati fulani akiwa site akikagua ujunzi wa jengo akamuuliza Mkandarasi kwanini hili hili jengo lina ngazi mbili? Yaani ya kawaida na lift. Mkandarasi akamjibu kuwa sisi tunafuata kilichopo kwenye mchoro/ramani. Alimuakia kweli kweli kudhalilisha taaluma yake. Mwisho akamwambia Mkandarasi ingekuwa nyumba yako ungeweka hiyo lift.
 
This week wamesema imekamilika kwa zaidi ya 90%, hebu nenda kaangalie kama ni kweli maana wabongo huwa wabishi mno.
Madam hawa jamaa hata wakikwambia "good morning!" kabla hujaitikia rudi ndani katazame muda kwanza, yawezekana ukakuta ni jioni. Uongo umeingia kwenye DNA zao.
 
Tatizo Bargain, mchina huenda alitaka mara 2 ya anachokula mturuki
Ile kusema angejenga mchina kulikuwa na upigaji, ulikuwa ni uwongo wa hali ya juu. Dhamira ya uwongo ule ilikuwa ni kutafuta simple political popularity ili waleWatanzania wajinga na wasioelewa chochote wahadaike na kuona Rais wa sasa ni mzalendo zaidi ya waliotangulia.

Ukweli ni kuwa ujenzi wa sasa utakuwa na gharama karibia mara 1.8 ya gharama ambayo angetumia mchina kwa kadiri ya makubaliano kati ya Serikali ya China na Serikali ya Kikwete. Kwa aibu kubwa Magufuli amelazimika kurudi na kuwaangukia Wachina.

Mpaka kufika Singida, gharama yake ni karibia 80% ya gharama ambayo reli ingefika Mwanza, kama angejenga Mchina.
 
Umeangalia update ya January? Ingia YouTube andika sgr tanzania update then rudi hapa ufute ulichoandika
 
Sawa mkuu, nimeshauri hivyo kwa kuzingatia tayari tuna miundombinu ya awali ( barabara), reli ni miundombinu ya kimkakati huwezi kuijenga kama huna cha kufanyia tayari.

Hata mkoloni aliimarisha kilimo kwanza kabla ya reli, alivyoona kuna rasilimali za kubeba ndipo akajenga reli ila kwa kuanzia alianza na barabara kufika maeneo ya kilimo.

Bado naamini hiyo sequence ya mkoloni ina mantiki hata leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…