Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Mtikisiko wa uchumi tokana na covid19 utayumbisha vingi. Siyo kwetu tu, hata kwao.
Tangazo la awali mradi kpande cha Dar - Moro kingekamilika Nov 2019. Kabla hata covid haijaanza. Hawana cha kusingizia covid hawa.

 
Mkuu unajishughulisha na ukandarasi?
 
Unajuwa siku hizi dunia imebadilika na kuna ushindani sana sababu ya maendeleo ya mitandao mpaka bandari zetu. Mashindano ya siku hizi ni kupunguza gharama operation cost. Barabara zetu kweli zipo lakini zinaharibika haraka sababu ya hii mizigo mikubwa na foleni inasababisha pia kuongeza gharama. Ufanisi ndio mashindano ya siku hizi, je nikitaka kufungua kiwanda itachukuwa muda gani, sheria zikoje, hapa ndio tunashida tunaweka mazingira magumu sana duka dogo tu utakuta vibali 20, ni mambo hayana gharama lakini tunayafanya magumu. Reli itawavutia wawekazaji kuwa gharama za usafirishaji zitapungua kwa sababu njia za transportation nyingi kuwafikia wateja au walengwa. Leo hii ukichukuwa eneno kubwa pori tu, safisha, weka lami, umeme, maji utauza eneo au viwanja mara kumi au zaidi. Miundombinu kwanza kwa maana tranpsortation za uhakika, communication, umeme, maji na mengine mengi plus sera bora utaona wawekezaji wengi.
 
Nimeacha Mkuu, baada ya kuona Tender nyingi wanafanya TBA na wenzao SumaJKT.

Saivi tunagombania kazi za kujenga vyumba vya madarasa ambazo wanatumia Force accounts hivyo naambulia kuwa Fundi tu😇😇
Industry imevurugwa sana
 
Hizo usd bil 7.6 toka China exim bank zilikuwa kwa ajili ya Sgr ya umeme? Lakini kwa kasi ya utendaji Wachina wapo vizuri kuliko mturuki.
 
Yapi Merkez nimewapita jana Dodoma,wako bize usiku wanapiga kazi,sijajua kama ni kila siku wanafanya vile au ni jana tu.
 
Unabisha huwek data kwa sasa stesheni ya Morogoro tayr na ya DSM tayr now kuna ujenzi wa daraja la juu kabla hujaingia Dodoma ambapo juzi juzi treni ilisombwa na maji daraja la juu DSM wameandika reli tayar na wameweka pembe za ndovu like.
Kwani nani hajui kuwa kuna reli imetandazwa? Madraja yamejengwa? Je itakamilika kabla JPM hajatoka madarakani?
 
Hili ni tatizo kubwa.
 
Nadhani pia tatizo letu hatuna "National Vision and Mission" ndio maana kila rais anayekuja anaweza kuacha aliyo yakuta na kuanza michakato yake binafsi.

Umegusia suala la urasimu pia, kweli ni kikwazo sana. Kukamilisha jambo dogo tu kunakuhitaji upitie ngazi nyingi tofauti na tozo/kodi za kero kila unapopita. Hii inatupotezea muda na kukwamisha maendeleo.

Issue ya technology ndio naona kama tumeipa kisogo kabisa, hadi leo unaenda ofisi za umma eti unaambiwa subiri labda baada ya wiki 2 tunatuma taarifa makao makuu, seriously?!

Pia awamu hii inaua sekta binafsi kwa kutaka ifanye kila kitu, hilo haliwezi zaa matunda ni suala la muda tu.

Unakazana kuua sekta binafsi then unafanya miradi kama SGR, Hydro power, Ndege sasa unajiuliza serikali huwa ina mizigo gani ya kusafirisha? Serikali itafanyia nini huo umeme wote kama sio sekta binafsi? Ndege ni mtumishi gani wa umma anayemudu huo usafiri ukiacha wachache wa ngazi za kati na juu?
 
Ni kweli, kuna kampuni ya kichina ilitaka kusaini na Jakaya kwa dau kubwa lenye mizengwe,lakini haikuwa sababu ya kuwanyima wachina kazi maana kampuni zipo nyingi.
Na Jakaya tena, hivi huu mradi ni ubunifu wa Jakaya eeh!! Sikuwa najua
 
Sielewi mantiki ya mada hii, kwani miradi mikubwa ya kimkakati huwa ni lazima imalizwe na Rais aliyeko madarakani. Mbona kila aliyeingia alikuta miradi ya awamu iliyotangulia inachofanya ni kuiendeleza, cha ajabu nii?
 
Huo mradi kwa wingi wa graduates mtaani wangetangaza dau mradi ungeisha ndani ya miezi 6 tu. Kupanga matofali na kufunga reli ndio iwe ishu hivyo? Waturuki wao wangejenga sehemu zenye madaraja tu

basi kama ni ivo watanzania wote ni maenginer wa reli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…