Mawazo haya wana psychology wanaita intuition sawa na kupiga ramli au kufuata hisia yaani kurahishisha mambo bila kutumia juhudi za kujiuliza kwa kuhusisha kutumia fikra na bongo kujiuliza tunavyoona na kufikiri ndivyo au tunarahishisha kuwa DR Congo, Rwanda, Burundi lazima watatumia SGR reli yetu watake wasitake.
Inabidi tuende mbele na kujiuliza kwa juhudi kabisa/ effort wanavyosema wana-psychology kuhusisha mawazo, fikra, mdahalo kama huu hapa JF na bongo zetu bila kutumia mahaba ya kumpenda kiongozi/ chama kutumia "kuotea/intuition/ ramli".
Yaani tufanye juhudi / effort za makusudi kabisa kuachana na mtindo huu uliojitokeza sasa ktk mitano-mingine kutumia kuotea/kuamini na kuaamua kujiuliza tena na tena kweli SGR itegemee maamuzi ya jirani au wenyewe tujipange reli yetu 60% itegemee shughuli za kiuchumi za ndani ya nchi ndiyo ziendeshe kujenga mradi huu au la na kwa kiwango gani na wapi reli hii iende ndani ya nchi yetu.
Dunia hii ni chaotic / uwanja-wa-fujo kwa nchi yoyote ikiwemo Tanzania kutegemea kupitia intuition / maoteo bila kutumia fikra gonganishi ktk bongo kuamini majirani wa DR Congo, Rwanda , Uganda wataibeba SGR reli yetu na huku tunajua fika kuwa hatuwezi kuwalazimisha au kuwashawishi waitumie kwa miezi sita, mwaka au milele reli yetu.
Explorations of the Mind: Intuition with Daniel Kahneman
Source : University of California Television (UCTV)