Uchaguzi 2020 Dalili zote zinaonesha anga limeikataa CCM

Uchaguzi 2020 Dalili zote zinaonesha anga limeikataa CCM

Haya ndio matokeo ya kufanya research kupitia coment za hapa jf na kwenye magroup ya chadema!

Tz ni kubwa jamani hawa walioko huku mitandaoni ni tone tu!

Kingine nmeona kwenye post za BBC kule facebook kuhusu Lisu, coment za raia wengi wa kule upepo haupo kwa Lisu kabisa.
Wakiandika vinyuzi vyao hapa, wanajiona wako peke yao
 
Walikuwa wanaroga watz kwa mwenge ... akili za watu mwaka huu zimerudi...walisema CDM inakubalika mijini tu sasa hivi vijijini wamecharuka kuliko mjini...
 
Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingu na mwanzo wa ngoma ni lele!

Kuelekea Oktoba 28 dalili zote zinaonesha CCM kukataliwa na anga la Tanzania.

Kutakua na matukio mengi mfululizo kuelekea Oktoba 28 ambayo yatabadili kabisa mwelekeo na upepo wa CCM dhidi ya upinzani.

CCM imeishiwa pumzi kabisa na kwa wataalamu wa alama za nyota tunaweza thibitisha hili kwamba upepo si mzuri kwa CCM na ile 'hewa' imeondoka kwenye paa la CCM!

Namba hazikubali kwa CCM na kwa mazingira haya Tanzania inakwenda kuandika historia mpya!
Mganga yupi anaweza kuwasaidia Gwajima Na Meko washinde kwenye nafasi zao ?
 
Sasa mbona we ndio umepanic kwa kumuita mtu usiemjua dada?

Nenda facebook kwenye page za BBC na VOA uone maoni ya raia kuhusu Lisu! Na wale ndio wapiga kura!

Au wewe unategemea maoni mnayopeana huko kwenye magroup yenu ya chadema?

Kura za kumuwezesha Lisu ziko huku field ambako Lisu hana ushawishi wowote.
Hata kura za Fb Magu haongozi acha kudanganya hapa. Mwanzo mlisema kuwa Lisu anaongoza Fb na JF lakini hivi sasa mmekuja na hoja kuwa Lisu anaongoza JF ila Fb anaongoza Magu. Fb watumiaji wengi ni vijana na mgombea wenu hana ushawishi kabisa kwa vijana kutokana na Sera sake mbovu za elimu, ajira, mikopo, mishahara, na afya. Kwa ufupi hakuna sekta yenye unafuu awamu hii
 
Maskini,

Ni i mpumbavu pekee anaefikri Lisu huyu ndio atashinda urais mbele ya Magu na ccm
 
Namba zipi? Huu upepo wa Lisu ndio namba?

Kwahiyo wewe ulitegemea katika huu uchaguzi wa vyama vingi huko upinzani kusiwe na purukushani zozote? Sasa ungekuwa uchaguzi wa vyama vingi huo?

Lisu atatoa tu changamoto ya uchaguzi lakini hataambulia hata 20% ya kura.
Hiyo 20% unayoiimba kila siku umeijuaje? Au ndivyo mmpanga huko Tumeccm? We are watching.
 
Zindiko la mwenge limekiukwa sababu ya ujio wa corona, mwenge uliokuwa ukizipumbaza akili za watz haukukimbizwa this year thus akili za watz zimefunguka
 
Maskini,

Ni i mpumbavu pekee anaefikri Lisu huyu ndio atashinda urais mbele ya Magu na ccm
Waliozulumiwa korosho zao
Walionyimwa nyongeza za mishahara
Walioliwa rambirambi zao
Waliochomewa nyavu zao
Waliofilisiwa
Waliobambikwa kesi
Walionyimwa mikopo
Waliokosa ajira
Ndio watakao mpigia Lisu.
 
Kingine nmeona kwenye post za BBC kule facebook kuhusu Lisu, coment za raia wengi wa kule upepo haupo kwa Lisu kabisa.
FB ni kwa wanafiki wanaotegemea kula yao kwa kuuza sura. Wanaoamini Tanzania inawezekana bila CCM hawapotezi muda kwenda FB kwa sababu vyombo vyote vya dola vinatumika kuwalinda wezi katika hilo bonde la kashfa. Nzi ukiwaona wanatua pahala kwa wingi, hapo lazima kuna dampo na CCM ni dampo ya kweli kweli.
 
Kuichagua CCM ni kuleta balaa jingine ndani ya miaka mitano.

Ni vizuri sasa wapishe ,wakae pembeni.
 
Zuio la mikutano 5 yrs plus manunuzi ya wanaopigiwa kura ccm tunaomba tathmini je lilikuwa ni wazo lenye faida au hasara
 
Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingu na mwanzo wa ngoma ni lele!

Kuelekea Oktoba 28 dalili zote zinaonesha CCM kukataliwa na anga la Tanzania.

Kutakua na matukio mengi mfululizo kuelekea Oktoba 28 ambayo yatabadili kabisa mwelekeo na upepo wa CCM dhidi ya upinzani.

CCM imeishiwa pumzi kabisa na kwa wataalamu wa alama za nyota tunaweza thibitisha hili kwamba upepo si mzuri kwa CCM na ile 'hewa' imeondoka kwenye paa la CCM!

Namba hazikubali kwa CCM na kwa mazingira haya Tanzania inakwenda kuandika historia mpya!
Tatizo ni moja tu mililo nalo, mnataka kubeti hadi kwenye Maisha yetu..
 
Back
Top Bottom