Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Kimenuka[emoji23]
 
Huyu waziri ni kichaa,kwani Tanzania ni police state?,kabla ya kutumia akili ya kuwashawishi watanzania wajitokeze kwa wingi kushangilia teams zetu yeye anatumia vitisho kama kenges wengine,vipi serikali ya ccm bila ya police hamuwezi kuongoza nchi
 
Hapo zamani za kale
IMG_0312.jpeg
 
Ndumbaro analeta mambo ya UJIMA (COMMUNALISM)

Na hulka ya binadamu Ni kufanya Yale yaliyo katazwa (Ngoja tuone)

Mtu anunue ticket kwa pesa yake alafu umpangie Cha kushangilia (siku zote binadamu hupenda furaha na ushindi)

Dunia ya Leo yenye football globalization huwezi kuwapangia watu TIMU za kuishangilia...
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
suala la uzalendo ni ni muhimu sana kulitilia maanani na kuliwekea utaratibu...
 
Ningependa viongozi wa Simba wajitokeze hadharani waonyeshe kutounga mkono kauli hii ya Waziri. Hata ukimsikiliza inaonyesha alikuwa anasisitiza zaidi Yanga na ndiyo wamemjaza huu ujinga, baadae anaitaja Simba kama kujalizia tu ionekane anaongelea game zote mbili.

Wanasiasa ndiyo wanaosababishaga nchi zinafungiwa kwa mechi za kimataifa kwa kauli na maamuzi kama haya ya kisiasa. Sidhani kama kuna kiongozi wa Simba yuko na wasiwasi wa mashabiki watakaovaa jezi za Al Ahly siku hiyo maana kuna mechi za Simba tunawaonaga mashabiki wa Yanga wamekuja wanashangilia timu pinzani na hakuna anayewabughudhi. Kama jezi ya mtani ni halali inakuwaje jezi ya timu pinzani iwe haramu?

Je atakayeamua kuvaa jezi ya Simba kwenye mechi ya Mamelodi itakuwaje maana afadhali hata jezi ya Mamelodi rangi ni zile zile tu kama za Utopolo.
 
Mheshimiwa aambiwe ukweli kuwa mpira sio uadui

Hawa Mamelody hawajatukosea kitu sioni sababu ya kuwanyima uhuru mashabiki zake
 
Back
Top Bottom