Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Nasubiri kauli ya Mwenyekiti wa Vilabu Afrika atoe maoni yake kuhusu kauli hii ya Waziri na kama hili suala lina tija kwa maendeleo ya mpira Afrika.

Hawa ndiyo wanasiasa ambao kesho wanasimama tena majukwaani wanakwambia habari za muungano kati ya Waafrika wakati kwenye mpira tu unasambaza uadui kati yetu.
 
Na uzalendo sio mavazi. Mwigulu anavaa bendera ya taifa lakini alitushawishi tuhamie burundi. Na bado hatendi chchote kinachodhihirisha uzalendo..
Uzalendo unatoka moyoni
ndio nani huyo ili arekebishwe kama anaenda kinyume na utaratibu...

nadhani hiyo ya moyoni ni kibinafsu na Mungu,

kibinadamu yaafaa kutengeneza utaratibu wenye sheria ndani yake wa kufuatawa na kila moja wetu bila upendeleo wala mbambamba...
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Kapoka uhuru.
Vipi kwa wale watakao washangalia hao wageni nao adhabu yao ni ipi?
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Ukiangalia umbo lake tu linakupa picha juu ya kile anachokisema.

Inamaana hakuna mashabiki wa Al Ahly au Mamelodi Tanzania hii?
20240319_191500.jpg
 
Wazir Ndumbaro mara nyingi amekuwa akionyesha uwezo mdogo Sana kwenye reasoning.
Inasemekana NI mwanasheria . Ajabu Sana hii.

Adhibitiwe mapema maana Kwa uropokaji huu na polisi tulionao inaweza kuwa vurugu kubwa siku ya mechi.

Suluhu ni Yanga na Simba kuhamasisha mashabik wao kununua mapema na Kwa wingi tiketi ili kutawala uwanja siku ya mechi.
Tena PhD
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Ushabiki na mapenzi havilamishwi, uzalendo haulazimishwi. wazir unashindwa kuja na strategy nzuri ya kufanya watu waipende tema yao? Wenzetu wanawezaje? Poor ideas
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Sasa washabiki wa Mamelodi na Al ahly mboni tinaonewaaa wajameniiii😢😢😢😢
 
Maskini, Afrika yangu sijui ina hazina ya viongozi wa namna gani! Yaani viongozi wakubwa, wasomi, wanaoongoza taasisi kubwa na wenye washauri wa kutosha, wanatoa maamuzi kama vile hawana vichwa!

Basi hapo waziri mzima na watu wake wamekaa chini wakaumiza na kukuna vichwa vyao haswa, wakala posho za kuwatosha zitokanazo na kodi zetu, finally wakatoka na uamuzi wa ajabu (na aibu huko nje) namna hiyo! Hao ndo tunatarajia watuamulie mambo yetu makubwa, pole yetu.

What if mtu ni fan wa kudumu wa Mamelod au Al Ahly?

Yaani Man City atakapokwenda Santiago Bernabeu kuchuana na Real Madrid kwenye UEFA quarter finals, waspain wakague kuhakikisha kila aliyevaa jezi ya Man City ana passport ya Uingereza, na kinyume chake pia game itakayofuata wiki moja mbele pale Etihad! Uzombie.

Kumbe kuna siku Chelsea itakuja bongoland kucheza mechi na Simba na/Yanga, nitalazimishwa kushangilia Simba na/Yanga!

Halafu kati ya ujinga unaoendelea nchi hii, mojawapo ni ile mentality ya kuwa kila mtanzania anayefuatilia soka either ni shabiki wa Simba au Yanga. Ukisema hushabikii timu yoyote kati ya hizo yaani huaminiki, utaonekana wa ajabu au unajificha. Mashabiki wa Yanga wataamini wewe ni shabiki wa Simba, na kinyume chake kwa mashabiki wa Simba. Naona huu upepo umewachota akili hadi viongozi.
 
Maelezo kutoka juu, nchi kwanza vaa upigwe uchakae usahau kwenu na tukikuweka ndan kukutoa buku50 kama huna mwaka mmoja jela mana utakuwa umehujumu uchumi, mikia mmesikia sio mnaleta tu ubish pumbv
 
Back
Top Bottom