Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Hilo bomu analolitengeneza atajuta

Kuvaa hizo jezi haitozuia Simba /Yanga kushinda,kufungwa au kusuluhu

Mchezo ni uwanjani, hizo jezi hazina cha kufanya na hata hiyo solidarity forever haipo basi tu

Kwa hiyo tuanze kukagua shabiki mmoja mmoja passport, like serious?

Waziri katoa boko, kama anataka kutumia hii platform kupanda chati kisiasa kafeli
 
B... Mi hili suala naunga mkono 100% tena tumechelewa sana. Tumekuwa kama wendawazimu kushangilia wageni.
Sawa, utani upo tutaniane (kama mimi ile siku ya Wydad japo najutaga sana) ila sio katika kiwango tulichofikia cha kuujaza uwanja kushangilia wageni.

Watakaokiuka wageuzwe mfano, na iwe serious maana nchi yetu hii utekelezaji sifuri.
Mpira haipo hivyo
 
Aiseee, huyu waziri kakurupuka

Nimevunja sheria ipi, kuvaa jezi ni kosa? What the..
 
Sasa jamani si unaona nimemquote mtu lakini? Huo ujumbe ni wake.
Anyways, kila mmoja yuko sahihi kwa upande wake na sikupingi.
Kushangilia mahasimu muda mwingine ni ili kuwafanya watani wafanye juhudi washinde, sio lazima iwe kukomoana.
 
Kushangilia mahasimu muda mwingine ni ili kuwafanya watani wafanye juhudi washinde, sio lazima iwe kukomoana.
Kwahiyo unataka kusema kuujaza uwanja kushabikia timu ngeni ambako kunawapa morali ya kuifunga timu ya nyumbani ndiko kuwafanya watani wafanye juhudi washinde?

Hivi umewahi kwenda uwanjani ukaona jinsi tulivyo wapumbavu kushangilia wageni wakiwafunga watani zetu? Hadi hao wageni wenyewe wanashangaa!
This has to stop!
 
Nadhani anakosea,hii ni nchi huru kila mtu yupo huru kufanya atakacho,pia uzalendo ni kitu kinakuja natural tu.......mimi hata unifanyeje siipendi Simba na wala sina sababu..........nakuja na Passport yangu ya Malawi haina shida
 
Kwahiyo unataka kusema kuujaza uwanja kushabikia timu ngeni ambako kunawapa morali ya kuifunga timu ya nyumbani ndiko kuwafanya watani wafanye juhudi washinde?
Yeah! Itawafanya wafanye juhudi ili 'to prove you wrong'.

Mkifufuliza kuwafunga hao wageni kwa vipigo vikubwa hao washangiliaji watapotea wenyewe kwa aibu.
 
Huyu Jamaa hii Wizara imemshinda..., Hii Serikali wanashindwa kufanya mambo ambayo tunawalipa wayafanye matokeo yake wanaingilia mambo ambayo yapo sawa na kuharibu...
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

View attachment 2939197
ana Pg
Putin.jpg
 
Huyu Jamaa hii Wizara imemshinda..., Hii Serikali wanashindwa kufanya mambo ambayo tunawalipa wayafanye matokeo yake wanaingilia mambo ambayo yapo sawa na kuharibu...
Ana PhD huyo
 
Hilo bomu analolitengeneza atajuta

Kuvaa hizo jezi haitozuia Simba /Yanga kushinda,kufungwa au kusuluhu

Mchezo ni uwanjani, hizo jezi hazina cha kufanya na hata hiyo solidarity forever haipo basi tu

Kwa hiyo tuanze kukagua shabiki mmoja mmoja passport, like serious?

Waziri katoa boko, kama anataka kutumia hii platform kupanda chati kisiasa kafeli
Ccm akili watoe wapi, mtu kabla ya kusifia timu zetu zenyewe anaanza kumsifia raisi, nchi imekua ya kiboya sana hii
 
Yaani sawasawa na Arsenal ije Bongo icheze na Yanga halafu ukataze mashabiki wa Arsenal Bongo wasiingie na jezi za timu zao. Hopeless kabisa.

MPIRA SIO VITA.
 
Yeah! Itawafanya wafanye juhudi ili 'to prove you wrong'.

Mkifufuliza kuwafunga hao wageni kwa vipigo vikubwa hao washangiliaji watapotea wenyewe kwa aibu.
Wewe hebu nyamaza usinikumbushe machungu ya mechi ya fainali Vs USM Alger, watu wamejazana uwanjani kuwashangilia bado tulivyotoka tumezomewa njia nzima na kutukanwa juu.

Tufanye hayo kwenye mechi zetu za ndani, kimataifa hapana.
 
Dish la dstv huku limeyumba upepo ni mkali sana,nashindwa kupata supersport
 
Wewe hebu nyamaza usinikumbushe machungu ya mechi ya fainali Vs USM Alger, watu wamejazana uwanjani kuwashangilia bado tulivyotoka tumezomewa njia nzima na kutukanwa juu.

Tufanye hayo kwenye mechi zetu za ndani, kimataifa hapana.
Word...
 
Back
Top Bottom