Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Nikivaa jezi yangu ya Manchester United nitaulizwa passport ya UK!
Kama Manchester United ndio inayocheza kwa Mkapa na timu ya Tanzania kwenye mechi ya mashindano watakuuliza passport ya UK hakuna shaka yoyote.
 
Huyu Waziri wa michezo kutumia jeshi la polisi kulazimisha watu wasishabikie timu zao kwa uhuru ni uzalendo wa kishamba uliopitwa na wakati.

Waziri huyu haendani na falsafa ya Rais Samia ya uhuru na utandawazi, haelewi kwamba kuna watanzania wengi wanafuatilia pia ligi za nje siku hizi na mtu unaweza kuwa mtanzania na ukawa shabiki genuine wa timu za nje.

kuwaacha watanzania wajiamulie mambo yao ili mradi wasivunje sheria za nchi.

Hatupo tena awamu ya 5, hii ni awamu ya 6.
 
Tunashangilia timu kwa kulazimishana?

Waziri kavunja katiba halafu kavunja haki za binadamu.

Kwenye kubeti nako atalazimisha watu wabeti upande upi? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kama vipi ampangie kanji odds za hizo game
 
Huyu jamaa sio mtu wa Mpira kabisa aisee pana Timu SA ndio walianzisha utaratibu wa Uwanja wao kutogawa mashabiki wa Timu ngeni na wao yaani walikua wanashangilia kwa kukaa pamoja ile Timu imeshuka daraja sasa hivi washabiki wengi huwa wanavaa ile jezi kuienzi ile Timu iliyoanzisha Ubuntu Botho kwenye soka leo hii huyu Mzala sijui katokea wapi na hii hoja yake na inaonekana kavamia mpira ndio maana TFF walimkataa na kumfungia ingawaje TFF nao ni wale wale wasiojua Mpira...
 
Viongozi waliochoka hawana vipaumbele ni kukimbizana na tuvitu tudogo tudogo twa kijinga.
 
Hizi siasa wapelekeeni familia zenu huko msituletee chokochoko kabisa. Tulipokuwa tunahangaikia hii league yetu mlikuwa huko matakomeni mnakunywa kahawa. SASA mpira wetu umekua mnaleta visheria vyenu vya kisiasa hapa.
Kwenye mpira wakusema ni mmoja Tu...mmiliki WA Azam TV. He knows how far he has brought this game.

Wengine kakojoe mlale na jezi tutazivaaaaa.....
Uzalendo kwani hizi timu ni taifa stars? Mmmmm
Supu ya jiwe🤔
 
Huu sio utaratibu ni kuingilia maamuzi ya mtu binafsi, na sio kosa kisheria una haki ya kushabikia timu yoyote

Sasa ule ustahamilivu wa 4 R za kiongozi wa nchi ina maana watendaji wake hawauishi??
Ukiwa nyumbani kwako uko huru kuvaa na kushangilia hizo timu utakazo, huko hajaweka utaratibu kwa kuwa anajua una uhuru wa kufanya maamuzi binafsi.

Ila kwenye uwanja ulio chini ya wizara yake amekataza hilo jambo. So unaweza kubaki kwako ili uutumie huo uhuru wako.

Ova
 
Maskini, Afrika yangu sijui ina hazina ya viongozi wa namna gani! Yaani viongozi wakubwa, wasomi, wanaoongoza taasisi kubwa na wenye washauri wa kutosha, wanatoa maamuzi kama vile hawana vichwa!

Basi hapo waziri mzima na watu wake wamekaa chini wakaumiza na kukuna vichwa vyao haswa, wakala posho za kuwatosha zitokanazo na kodi zetu, finally wakatoka na uamuzi wa ajabu (na aibu huko nje) namna hiyo! Hao ndo tunatarajia watuamulie mambo yetu makubwa, pole yetu.

What if mtu ni fan wa kudumu wa Mamelod au Al Ahly?

Yaani Man City atakapokwenda Santiago Bernabeu kuchuana na Real Madrid kwenye UEFA quarter finals, waspain wakague kuhakikisha kila aliyevaa jezi ya Man City ana passport ya Uingereza, na kinyume chake pia game itakayofuata wiki moja mbele pale Etihad! Uzombie.

Kumbe kuna siku Chelsea itakuja bongoland kucheza mechi na Simba na/Yanga, nitalazimishwa kushangilia Simba na/Yanga!

Halafu kati ya ujinga unaoendelea nchi hii, mojawapo ni ile mentality ya kuwa kila mtanzania anayefuatilia soka either ni shabiki wa Simba au Yanga. Ukisema hushabikii timu yoyote kati ya hizo yaani huaminiki, utaonekana wa ajabu au unajificha. Mashabiki wa Yanga wataamini wewe ni shabiki wa Simba, na kinyume chake kwa mashabiki wa Simba. Naona huu upepo umewachota akili hadi viongozi.
Siwezi shabikia hizi timu mbili
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

Unajua CCM wengi huwa hawana akili ya kuchanganua mambo kwa weledi. Ndiyo maana wanatuangusha katika kila nyanja. Sasa kwa kuingia na jezi alizozitaja kunasababisha nini? Ndiyo maana nchi yetu inasuasua kwenye maendeleo. Hivi watu wakiingia bila hizo jezi alizokataza halafu kwa mfano kwenye mechi ya Mamelodi halafu wakaishangilia Mamelodi hapo Ndumbaro atasemaje?

POOR NDUMBARO! POOR THINKING CAPACITY!
 
Kwamba kila mtu ana haki ya kutoa maoni na imeandika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi hata serikali ikisema jambo jema huyo kiongozi anakoga matusi kama mtoto mdogo, tena hata waandishi na wachambuzi ambao tunadhani wana elimu kidogo ya kuelimisha watanzania wajinga wajinga nao wamekuwa wachovu.

Waziri Ndumbaro amesema mtu yeyote atakayevaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly hatoingia uwanjani ama atachukuliwa hatua za kisheria.

Dhamira yake ni nini Waziri huyu ambaye ni nguli wa sheria?

Tanzania imejenga heshima kubwa barani Afrika kwa kuingiza timu mbili kwenye michuano mikubwa ya Afrika, hili sio jambo dogo.Mataifa makubwa kama Egypt, Tunisia, Congo, Morocco hawajafanya hilo.

Dhamira yake Waziri huyu ni kutaka kuona SImba na Yanga wanakwenda nusu fainali ili kuiheshimisha nchi.Afrika inajiuliza Tanzania ipi hiyo imepeleka timu 2 robo fainali? Nyie hamuoni kuwa wanatuonea gere Tanzania kwa mafanikio makubwa namna hii.

Sasa inakuwaje wewe Yanga anacheza na Mamelodi una jezi ya Ubuntu unaenda kushangilia Mamelodi uwanjani?

Hebu tuwe wakweli, nani amewahi kuona mashabiki wa Zamaleki au Prymids au Ismailia au Future kule Misri amevaa jezi za Simba wanakwenda uwanjani kushangilia Simba? Wekeni ushahidi humu wapi nyie mmeona Simba au Yanga wakiwa ugenini halafu kule kuna genge la waraabu au wakongo wamevalia jezi za Simba wanajiandaa kwenda kuiombea mabaya timu ya nchi yao ikicheza na SImba au Yanga?

Sisi watu wa aina gani jamani? Mimi pia siipendi Yanga kuliko maelezo lakini siwezi kwenda uwanjani nimevalia jezi za Mamelodi nakwenda kushangilia Mamelodi uwanjani, siwezi kufanya ufala huo.Ntashangalia nikiwa nyumbani na familia yangu lakini sio kwenda uwanjani kufanya uchale.Never.

Eti washabiki wakizuiwa kuingia uwanjani picha zitatumwa CAF na FIFA.Hivi nyie wachambuzi mna akili kweli? Nyie waandishi vipi lakini? Mbona mnadhalilisha taaluma.Nyie mnaona sawa kweli watanzania waende kushangilia Mamelodi uwanjani wakicheza na Yanga pale kwa Mkapa?

Yanga anakwenda kucheza na Mamelodi kule Afrika Kusini, hakutakuwa na msauzi yoyote atakeyavalia jezi za Yanga kushangilia Yanga, huyo anaweza kuwa marehemu.Kule hawana upuuzi huo kama tunaotaka kuufanya sisi hapa bongo.

Eti mtangazaji mmoja wa Clouds anasema tayari jezi za Ubuntu zipo Kariakoo na watu wanataka kufanya biashara, shame on him.

Vyombo vya habari vya namna hii vidhibitiwe, wenzenu huko south wanaongelea timu yao, wekeni media zao muwasikilize kama wanaongelea hofu kwa Yanga au Simba kule Misri.

Serikali imetoa kauli, tuiheshimu na sio kila mmoja anatoa kauli ili mradi tu eti ni uhuru wa kutoa maoni.Pumbavu kabisa.
 
Rais Samia tafadhali zuia hili Tamko kwani Askari wako Watapigika mno na Sisi Wengine wenye Mikanda myeusi ya Combat Kung Fu.

Uzalendo ni kwa Timu ya Taifa tu na kamwe siyo kwa Vilabu vya Matapeli / Wajanja Wajanja wa Juice na Magodoro.

Siwezi kamwe Kuishangilia Yanga SC na nawaonya Askari watakaothubutu kutaka Kutukamata tutakaozishangilia Mamelodi na Al Ahly kwani WATAPIGIKA na hawatoamini kabisa.

Sasa nyie semeni kuwa Ninatania tu. Na Combat Kung Fu yangu hii nimejifunzia kwa Netanyahu, Putin na Mapanki wa Korea Kaskazini.
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

GENTAMYCINE Wakurya wako wataarifu kabisa, tujue kama tutakusafirisha au tutakuzika Parokiani Kawe
 
Back
Top Bottom