Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Kinacho ipeleka timu kwenye mafanikio ni wachezaji bora na maandalizi mazuri ya timu ndio maana timu hata ikicheza bila mashabiki inashinda kuzomea au kushangilia ni haki ya shabiki wa mpira na hapangiwi timu ya kushangilia na mtu awae yoyote yule, labda utuambie hapa mtu akivaa jezi ya Mamelodi anakua amevunja sheria gani ya nchi?

jezi zitavaliwa na wageni watashangiliwa kama kawaida hio ni kawaida yetu na hakuna wakutupigia kelele kwenye hilo
 
Huyu timu ya taifa imemshinda kageukia kwenye vilabu.Mpira na matamko wapi na wapi.bado kidogo mpira wetu wa vilabu utaharibika.
 
Kazi Kweli
 

Attachments

  • IMG-20240323-WA0017.jpg
    IMG-20240323-WA0017.jpg
    185.4 KB · Views: 2
Kazi Kweli
Toka mwanzo nilisema hii issue inahusiana na mechi ya Yanga kuliko hata ya Simba, mmeona sasa wenyewe kwenye barua ya TFF.

Inawezekana Serikali ilikuwa na nia njema kukataza jezi za Mamelodi ili kuepusha vurugu maana mechi ya Yanga itakuwa sensitive sana (wataumia sana wakifungwa halafu Simba ishinde) ila mtindo wa muda mrefu wa serikali kukimbia majukumu yake ya kutoa ulinzi na usalama badala yake kutafuta njia za mkato za makatazo huku wakibinya uhuru na haki za raia ndiyo matokeo yake haya. Naamini kuna kitu watakuwa wamejifunza.

Raia tuna sauti na nguvu tukiamua kuzitumia. Ni suala la kujitambua tu.
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

Huyu ndiye anafanya watu wafupi wadharauliwe
 
toa maoni yako mwanasport je ni sahihi? na kama jibu ni ndio kwanini.hatukuanza kipindi inashiriki timu moja? au kipi kimepelekea kuanza awamu hii
kwanza hiyo tabia ya kuvaa jezi haijaanza hawamu hii imekua ni muendelezo kwa hizi timu mbili kubwa za serikali tokea miaka ya nyuma.

binafsi sioni kosa mambo ya soka hayo yapo hata ughaibuni huko.
images (10).jpeg
 
Kuvaa jezi ya timu ya nje na kwenda kuishangilia hiyo timu, kwa lengo tu la kuikomoa timu ya ndani; kwangu mimi naona ni uwendawazimu/uzwazwa.

Ifikie wakati Watanzania tujitambue ili hata hao wageni nao watuheshimu, badala ya kuendelea kutudharau na kutuona hatuna tofauti na nyumbu.
 
Toka mwanzo nilisema hii issue inahusiana na mechi ya Yanga kuliko hata ya Simba, mmeona sasa wenyewe kwenye barua ya TFF.

Inawezekana Serikali ilikuwa na nia njema kukataza jezi za Mamelodi ili kuepusha vurugu maana mechi ya Yanga itakuwa sensitive sana (wataumia sana wakifungwa halafu Simba ishinde) ila mtindo wa muda mrefu wa serikali kukimbia majukumu yake ya kutoa ulinzi na usalama badala yake kutafuta njia za mkato za makatazo huku wakibinya uhuru na haki za raia ndiyo matokeo yake haya. Naamini kuna kitu watakuwa wamejifunza.

Raia tuna sauti na nguvu tukiamua kuzitumia. Ni suala la kujitambua tu.
Ya muhimu umeyaandika para ya mwisho.
 
Sasa kama mimi ni raia wa Tanzania lakini makazi yangu kwa muda mrefu yamekuwa huko Misri mtanikataza kushangilia timu nayoikubali?
Onyesha tiketi Yako ya ndege na passport ya Tanzania pamoja na nyaraka za makazi huko misri tupe hata bili za maji na umeme traveling documents and working permits
 
Ni swala la muda tu watarudi hapa jukwaani na vilio baada ya izo mechi.
Bahati mbaya wengi hawajui jinsi mpango wa kudhibiti wapuuzi ulivyo pangwa katika mechi hizo.
Wao wanaamini wakiguswa nchi itafungiwa na caf/ fifa ndipo unapata picha namna katika mpira kuna ma zuzu wengi.
 
Ukishabikia sana Simba na Yanga kichwani zinapungua Lazima.

KUNA VIJANA WENGI MNO AKILI ZIMERUKA KABISA, HAWANA FUTURE WAO NI KUWAZA SIMBA NA YANGA TU.....

MSIPOTEZE MUDA NA UPUUZI WA SIMBA NA YANGA.

MY MESSAGE
MWENYE SIKIO NA ASIKIE.
 
Simba na yanga
Ccm na chadema

Singo maza.

Sungura na dabo kiki.

Kubeti.

MTU yeyote anayejihusisha na haya mambo bila kulipwa mshahara ajue yeye anatumika hapa duniani ili kuwapatia watu faida kupitia ujinga wake.
 
Back
Top Bottom