GenuineMan
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 7,885
- 18,636
uwongo ×DP wapo dar tu,acheni uwongo
Ni uwongo na si uongo,uongo uongozi au?uwongo ×
Uongo
Kwa uchumi upi mjenge hiyo refinery? Mchina anataka fedha mbele na siyo longo longo!Sahihi, Tanzania na Uganda wamtetemeshe kwa kutafuta mwekezaji mwingine. Hata refinery yake ya Nigeria mkandarasi mkuu alikuwa ni kampuni ya China, CNCEC
Na walimtumia Mchina kwa sababu mataifa ya Magharibi hayakuwa tayari kuona Afrika inamiliki refinery kubwa.
Wao Magharibi walikuwa wanataka mafuta ghafi yatoke Nigeria yaende kwao yasafishwe yarudi kuuzwa tena Nigeria/Afrika
Nchi kadhaa za Afrika kwa sasa zimeamua kutumia makampuni ya Kichina inapohusu masuala ya nishati kupunguza bureaucracy za Magharibi na mashirika yao ya kifedha kama IMF na WB
Na yeye tumfanyie kama alichowafanyia Wazungu kule Nigeria. The game is brutal but still fair
UwongoNi uwongo na si uongo,uongo uongozi au?
Waache wapige kelele za wanasiasa kama Kasuku, Watakuja kushituka wakati refinery inafanya uzalishaji wa mafuta na lita ya mafuta wananunua elfu nane.Hivi wanajua Nigeria anakotoka Dangote moja ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani? Ni kipi kiko totfauti kati ya Nigeria na Tanzania kwenye maisha ya watu? Je ni kipi kipo tofauti kati ya Nigeria na Finland nchi isiyozalisha mafuta kama Nigeria? Hoja yangu hapa ni kuwa ajenge, asijenge, hakuna kitakachobadilika. Afrika matatizo yake ni zaidi ya viwanda vya kusindika mafuta.
Wameanzia Dar, lakini haiwaishii Dar tu.DP wapo dar tu,acheni uwongo
Bandari ya Tanga ilko chini ya dp worldTajiri ataamua mwenyewe.akajenge kiwanda sehemu ambayo hakuna malighafi au Akajenge sehemu ambayo kiwanda chake kitapata malighafi.
Hiyo kuwa na hali mbaya kwa wananchi wa Nigeria ni ujinga wa viongozi wao kishindwa kutumia rasilimali ambazo kama nchi wanazoWaache wapige kelele za wanasiasa kama Kasuku, Watakuja kushituka wakati refinery inafanya uzalishaji wa mafuta na lita ya mafuta wananunua elfu nane.
Labda hawajui Nigeria mzalishaji mkubwa wa mafuta na gas ila umeme na mafuta huko bado ni anasa kwa raia wengi, wana hali mbaya kuliko hata sisi.
DP world ni UAE, UAE ana plan ya kumiliki bandari muhimu duniani, mipango yake nje ya mafuta na gas(diversification Yao) ni bandari,dhahabu,ndiyo wanaofadhili bwana dagalo kule Sudan,muwe mnaacha uzushi na walau chimbeni chimbeni mamboWameanzia Dar, lakini haiwaishii Dar tu. Isitoshe hao DP World sio waarabu bali ni watanzania wenzetu wameingia mkataba wa kihuni kwa kuhodhi bandari zetu. Kadiri wanavyotanuka wao na familia zao ndio mkataba unazidi kutanuka.
Umeongea upumbavu wa hali ya juu sana na kwa bahati mbaya viongozi wa kiafrika wana mawazo kama yakoPopote refinery itakapojengwa itapata malighafi. Singapore, India na nchi nyingi za Ulaya wana refineries kubwa kuliko na hawana mafuta. Dangote atakachonufaika nacho zaidi kwa Tanzania labda ni ardhi ya bure.
Lete documents zinazoonesha Hilo au walau ofisi moja ya DP hapo TangaBandari ya Tanga ilko chini ya dp world
Kama tumeshindwa kunufaika na makaa yetu ya mawe, gas, Almasi , dhahabu na Tanzanite zetu wenyewe tutawezaje kunufaika na mafuta ya Uganda na refinery ya Dangote hadi tutokwe na mishipa hivi shingoni kupambana na Wakenya?? It doesn't make sense.Hiyo kuwa na hali mbaya kwa wananchi wa Nigeria ni ujinga wa viongozi wao kishindwa kutumia rasilimali ambazo kama nchi wanazo
Refinery itatoa ajira,maana hapo patazuka viwanda vingiKama tumeshihdwa kunufaika na makaa yetu ya mawe, Almasi , dhahabu na Tanzanite zetu wenyewe tutawezaje kunufaika na mafuta ya Uganda na refinery ya Dangote hadi tutokwe na mishipa hivi shingoni kupambana na Wakenya?? It doesn't make sense.
Yes, but pamoja na yeye kutokuangalia hayo still haifuti fursa kwa mwananchi mmoja mmoja so asipowekeza ni fursa imepotea.Muwekezaji mkubwa haangalii umuhimu wa biashara yake kwa raia bali soko lenye faida kubwa zaidi, upatikanaji malighafi, miondombinu, nishati na sera za kibiashara.
Hili linawezekana, it all depend na namna gani huo uwekezaji utatwist supply.Kuhusu bei za mafuta usiweke matumaini kwamba refinery itashusha bei kwa sababu kwanza hayo mafuta ghafi ya Uganda ni kidogo sana kwa hiyo bado tatendelea kuagiza mafuta mengi nje ya nchi, pia sio ajabu ukakuta hata gharama za uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ya Uganda ika sawa au zaidi ya kutoka kwingine tunapoagiza kwa meli sasa hivi.
Tusilalamike, tuna uongozi mbovu, mipasho, ubabe, viongozi kushupaa na kuiba rasilimali na maliasili! Na wakiiba hela za mlipa kodi wanapeleka Dubai, znz na kujenga apartments au majumba ya kifahari!Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.
Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.
View attachment 3586367
Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?
Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.
"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.
Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.
Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.
Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto
Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.
Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya
"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."
Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.
"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."
Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.
Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos
Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.
Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.
Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.
Nini maana yake kwetu Tanzania?
Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.
Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.
Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?
Karibuni kwa mjadala.
Ila unaakili fupi kwahiyo refinery tumiliki kama nchi ndo tunafaikeKama tumeshindwa kunufaika na makaa yetu ya mawe, Almasi , dhahabu na Tanzanite zetu wenyewe tutawezaje kunufaika na mafuta ya Uganda na refinery ya Dangote hadi tutokwe na mishipa hivi shingoni kupambana na Wakenya?? It doesn't make sense.
Ni kweli DP world wapo, lakini hawa waliokuja hapa ni affiliation ya majizi ya huku kwetu. Ndio maana mkataba ule huku kasaini rais, lakini kule sio mtawala wa UAE. Yaani serekali ya Dubai haijui lolote kuhusu huu mikataba, bali ni wa wafanya biashara wezi na viongozi wetu hasa Samia, Kikwete, Rostam nk. Huu utapeli ni kama ule mkataba wa Richmond.DP world ni UAE, UAE ana plan ya kumiliki bandari muhimu duniani, mipango yake nje ya mafuta na gas(diversification Yao) ni bandari,dhahabu,ndiyo wanaofadhili bwana dagalo kule Sudan,muwe mnaacha uzushi na walau chimbeni chimbeni mambo